Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Mahakama nchini yaingia enzi mpya
Monday, 06 December 2010 21:52
Makamu wa Rais,Dk,Mohammed Gharib Bilal,(wa pili kushoto walioinama) na Jaji Mkuu,Augustino Ramadhani,(kushoto) wakiangalia Kompyuta wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa kurekodi mashauri Mahakamani kwa Kompyuta na Tovuti ya Mahakama Kuu Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani. (Picha na Yusuf Badi)
THE Vice-President, Dr Mohammed Gharib Bilal (second right), gestures during the inauguration of the High Court website which will contain information on various court proceedings in Dar es Salaam on Monday. He is flanked by the Chief Justice, Mr Augustino Ramadhani (left), and the Secretary of ICT, Mr John Kahyoza (right). (Photo by Yusuf Badi)
James Magai
HATIMAYE Mhakama ya Tanzania imeanza rasmi safari ya matumizi ya teknolojia kuendesha shughuli zake, hususan uendeshaji kesi, baada ya kuzindua mfumo mpya wa kuweka kumbukumbu za mashauri mbalimbali mahakamani kwa kutumia kompyuta.
Mfumo huo ambao kwa kitaalamu huitwa mfumo wa digitali ulizunduliwa jana na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, katika ukumbi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam, huku wadau wakielezea manufaa na changamoto mbalimbali zinazoambatana na mfumo huo mpya.
Pia, Mahakama imezindua tovuti yake ambamo taarifa kama vile sheria mbalimbali zinazotumika nchini, hukumu za kesi mbalimbali tangu mwaka 1979 na nyingine kuhusiana na kesi zinazoendelea mahakamani zitakuwa zinapatikana humo.
Kutokana na kuzinduliwa kwa mfumo huo, sasa Majaji wa Mahakama Kuu na wa Mahakama ya Rufani, hawatalazimika kuchukua kumbukumbu za mwenendo wa kesi mbalimbali kwa kuandika kwa mikono, badala yake, kazi hiyo itafanyika kwa kutumia kompyuta maalum.
Katika mfumo huo mwenendo wa kesi utakuwa unaingia kwenye kifaa maalumu cha kuhifadhia sauti kwenye kompyuta, kisha baada ya dakika tatu sauti hizo huanza kuchapwa na wataalumu na kuwekwa katika maandishi.
Kwa kuanzia mfumo huo utaanza kutumiwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Dar es Salaam, kabla ya kuziunganisha kanda nyingine 14 ikiwamo mahakama za chini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Dk Bilal alisema matumizi ya teknolojia hiyo kuweka kumbukumbu za mashauri mahakamani, sio tu kutasaidia kuharakisha usikilizaji wa kesi, lakini kutajenga mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.
Dk Bilal alisema ingawa ni matakwa ya haki na Katiba ya nchi kuwa kesi zinazofikishwa mahakamani zimalizike muda muafaka, lakini Mahakama zimekuwa zikilalamimiwa kwa kuchelewesha kumaliza kesi mbalimbali.
Alitaka mahakama kutumia sheria kwa ufanisi na kwamba, kasi katika kuhitimisha kesi humaanisha upatikanaji wa haki badala ya kuzua mashaka.
Badala ya kuahirisha kesi mara kwa mara, Dk Bilal alitaka mahakama kuhakikisha zinaendeshwa kwa kasi, kwa wakati ikiwamo kuhitimishwa kwa haki na usawa.
Alisema matarajio ni kwamba kampuni ambazo zina matatizo ya kisheria katika shughuli zake za biashara, lazima ziweze kutatuliwa haraka ili kuwezesha uzalishaji wa bidhaa na utoaji huduma.
Dk. Bilal alisisitiza kwamba haki za binadamu na Katiba yetu zimejenga mazingira ya haki na usawa katika usikilizaji mashauri na kwamba, Mahakama ndio yenye jukumu hilo.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi, Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, alisema Mahakama imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchelewa kumaliza mashauri kutokana na kutumia zaidi mfumo wa uchukuaji kumbukumbu unaotegemea kuandika kwa mkono.
Jaji Ramadhani alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo mpya, kutawawezesha majaji kuepukana na mfumo huo wa kizamani jambo ambalo litawezesha kuharakisha usikilizaji mashauri.
Alisema faida kubwa ya mfumo huo ni kumwezesha Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi, kujua kila kinachofanywa na kila Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu.