Mabadiliko mahakamu kuu kitengo cha kazi; tusisubiri kukamilika kwa mchakato wa kupata katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko mahakamu kuu kitengo cha kazi; tusisubiri kukamilika kwa mchakato wa kupata katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Aug 5, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,973
  Likes Received: 37,548
  Trophy Points: 280
  Kwa nyakati tofauti kumekuwa na hoja kutoka kwa watu na wadau mbalimbali kutaka mabadiliko ya tume ya uchaguzi yafanywe kabla ya kukamilika kwa mchakato wa kupata katiba mpya.Hii ni kutokana na unyeti wa taasisi hii pamoja na athari zinazotokana na utendaji wake wa kazi.Kwa maneno mengine hii ni taasisi muhimu ambayo mabadilko yake hayaitaji kusubiri kupatikana kwa katiba mpya 2015.

  Kwa kuzingatia vigezo na sababu kama hizi,ni mawazo yangu hata upande wa mahakama hasa mahakama kuu kitengo cha kazi kinahitaji kuvunjwa haraka iwezekanavyo na utaratibu wa kupata majaji wanaounda kitengo hiki upitiwe upya na tuondokane kabisa na utaratibu wa sasa ambapo majaji hawa wanateuliwa na raisi.

  Katika mazingira haya ni vigumu haki kutendeke hasa pale mwajiri ambaye ni serikali anapohusika katika kesi mbalimbali.Hivi kweli kuna siku mahakama hii inaweza kuamuru kuwa mgomo huu ni halali kwa mujibu wa sheria?Hivi kuishitaki serikali katika mahakama hii kuna tofauti gani na ule msemo wa kesi ya nyani kuipeleka kwa ngedere?

  Wakati umefika watanzania tupaze sauti kudai mabadiliko ya haraka kwani ni sisi ndio tunaoumia na kusubiri mpaka 2015 ni jambo la hatari kwa haki na maslahi ya wafanyakazi.Serikali siku zote haina hofu na mahakama na ndio maana hukimbilia haraka mahakamani kujinusuru na wakati huo huo kukandamiza watumishi wake.Ile dhana kwamba kila mhimili wa dola unajitegemea katika nchi yetu ni kiini macho.

  Haki siku zote haiji kama sadaka bali inapiganiwa.
   
Loading...