Mabadiliko kamati ya Bunge: Spika Job Ndugai amefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
SPIKA.jpg

Dar es Salaam.
Spika Job Ndugai amefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Machi 12,2018 inasema Spika amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo imesema ibara hiyo imeweka wazi kwamba, Kanuni za Kudumu za Bunge zinafafanua muundo wa shughuli za Kamati za Bunge.

“Kwa msingi huo Kanuni ya 118 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 imeweka Kanuni za Kudumu za Bunge zenye muundo na majukumu mbalimbali kama yanavyofafanuliwa katika nyongeza ya nane. Uteuzi wa wabunge kwenye kamati mbalimbali unaonekana utaratibu katika Kanuni ya 116.”

“Kanuni ya 116(1)inaweka utaratibu kwamba, ujumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge,” anasema Spika Ndugai.

Katika uteuzi huo, wajumbe mbalimbali wamerejea katika kamati zao, wengine wakibadilishwa huku baadhi ya wenyeviti waliokuwa wakiongoza baadhi ya kamati wameondolewa.

“Kwa mamlaka niliyopewa na Kanuni ya 115(3) na kwa kuzingatia vigezo vilivyoanishwa katika Kanuni ya 116(5) nimefanya uteuzi mpya wa ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge. Wajumbe wa kila kamati wanawajibika kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni ya 116(10) kuwa viongozi wao,” amesema.

Mwananchi
 
Attachments

  • majina ya wajumbe wa kamati.pdf
    1.7 MB · Views: 224
Majina yakowapi sasa..by the way kashapona hadi anatengua na kuteua? Mungu mkubwa
 
Uandishi mwingine wa ajabu. Hivi interest ya msomaji ni kujua kwamba Kanuni za Bunge zinazompa Spika mamlaka hayo zipo na zinatambuliwa kikatiba na kwamba Spika ameamua kuzitumia au interest ya msomaji ni kujua mabadiliko husika? Yaani ni kamati zipi na nani kaingia na nani katoka?
 
Labda alizidiwa kabla hajamaliza teuzi zake akiwa huko india apolo hospital
 
Uandishi mwingine wa ajabu. Hivi interest ya msomaji ni kujua kwamba Kanuni za Bunge zinazompa Spika mamlaka hayo zipo na zinatambuliwa kikatiba na kwamba Spika ameamua kuzitumia au interest ya msomaji ni kujua mabadiliko husika? Yaani ni kamati zipi na nani kaingia na nani katoka?
Kwa faida ya wengi sahihisha uandishi huo hapo juu....
Andika hapa alivyotakiwa kuandika ujumbe huo ili na wengine tulioshia vidudu tuelimike na tusikosee kuandika sikunyingine
Jf ni Darasa la maarifa kwa wengi
Ni vema kila mkosaoaji akosoe na kutenda yeye kwa usahihi ili kujenga.

Ukiwa na roho ya kukosoa bila kurekebisha kwa wema utapatwa na jini kisirani na mwisho jini kupinga
 
kateua akiwa kitandani India?
Huko iringa madaktari wakimjua mgonjwà ni mhehe hawangaiki kuchukua vipimo kuona kama amepona wanamuuliza tu Leo unapenda kula chakulà gani ? Siku atakayoagiza Ugali na nyama ya kuchoma basi hapo dokta anajua huyu kapona anamdisharge kabla ya SAA sits mchana akapambane na hali yake. Basi na huyu jamaà wangemrudisha tu tzn
 
Wewe jamaa huwa una busara sana despite of being Verified User...Hongera sana
Hahaha kuna siku moja petro uvumilivu ulimshindwa alirushiana Maneno fulani nkasema Huyu ni petro Au any way mwishowe wote waka cool dwn

Ova
 
Kwa faida ya wengi sahihisha uandishi huo hapo juu....
Andika hapa alivyotakiwa kuandika ujumbe huo ili na wengine tulioshia vidudu tuelimike na tusikosee kuandika sikunyingine
Jf ni Darasa la maarifa kwa wengi
Ni vema kila mkosaoaji akosoe na kutenda yeye kwa usahihi ili kujenga.

Ukiwa na roho ya kukosoa bila kurekebisha kwa wema utapatwa na jini kisirani na mwisho jini kupinga
Mkuu, heading ya habari iko very clear "Mabadiliko kamati ya Bunge: Spika Job Ndugai amefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge"; keywords hapo "mabadiliko", "wajumbe" na "kamati za bunge".

Context hapo ni mabadiliko ya wajumbe lakini hakuna mahali popote habari husika inapotaja mjumbe au kamati hata moja badala yake mwandishi anajikita kutuelezea "mamlaka ya spika"; hayo yanajulikana. Tusichojua ni hayo mabadiliko ya wajumbe na kamati zenyewe kitu ambacho habari husika haijakieleza ndio maana nikaita "uandishi wa ajabu". Ningekuwa na majina ya kamati na wajumbe waliohusika kwenye mabadiliko ningeyaweka hapa ila bahati mbaya sina.
 
Dar es Salaam.
Spika Job Ndugai amefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Machi 12,2018 inasema Spika amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo imesema ibara hiyo imeweka wazi kwamba, Kanuni za Kudumu za Bunge zinafafanua muundo wa shughuli za Kamati za Bunge.

“Kwa msingi huo Kanuni ya 118 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 imeweka Kanuni za Kudumu za Bunge zenye muundo na majukumu mbalimbali kama yanavyofafanuliwa katika nyongeza ya nane. Uteuzi wa wabunge kwenye kamati mbalimbali unaonekana utaratibu katika Kanuni ya 116.”

“Kanuni ya 116(1)inaweka utaratibu kwamba, ujumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge,” anasema Spika Ndugai.

Katika uteuzi huo, wajumbe mbalimbali wamerejea katika kamati zao, wengine wakibadilishwa huku baadhi ya wenyeviti waliokuwa wakiongoza baadhi ya kamati wameondolewa.

“Kwa mamlaka niliyopewa na Kanuni ya 115(3) na kwa kuzingatia vigezo vilivyoanishwa katika Kanuni ya 116(5) nimefanya uteuzi mpya wa ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge. Wajumbe wa kila kamati wanawajibika kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni ya 116(10) kuwa viongozi wao,” amesema.

Mwananchi
Mungu amempendelea zaidi
 
Huko iringa madaktari wakimjua mgonjwà ni mhehe hawangaiki kuchukua vipimo kuona kama amepona wanamuuliza tu Leo unapenda kula chakulà gani ? Siku atakayoagiza Ugali na nyama ya kuchoma basi hapo dokta anajua huyu kapona anamdisharge kabla ya SAA sits mchana akapambane na hali yake. Basi na huyu jamaà wangemrudisha tu tzn
Hahaaaa
 
Back
Top Bottom