Mabadiliko Jeshini: Mpambe wa Rais apandishwa cheo na kupangiwa kazi nyingine, Kanali Mulunga awa mpambe mpya

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, Jenerali Mabeyo amefanya teuzi kadhaa ndani ya Jeshi la wananchi. Kanali M.E. Kaguti ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe, Kigoma amepandishwa cheo na mkuu wa majeshi, Jenerali Mabeyo amemuomba Rais amtumie kwa kazi nyingine.

Mabeyo amesema amefanya teuzi 28 na kwa ujumla wao na amemuomba Rais awatumie ili aimarishe safu ya uongozi katika Jeshi na anaamini kwa viongozi waliopo safu ya uongozi itaimarika.

Sambamba nao hao, Mabeyo amemuomba Rais aridhie kupandishwa cheo Luteni kanali D.P.M Mulunga kuwa Kanali na kwa cheo hicho Rais ameridhia awe mpambe wa Rais kuanzia leo.

Meja Generali PP Masau amepandishwa kuwa Ruteni generali atakuwa Mkuuwa Mafunzo Chuo cha Monduli

HS Kamunde amepandishwa kuwa Meja Generali na atapangiwa kazi baadae.

Pia Makanali 28 wamepandishwa vyeo kuwa Mabrigedia Generali ambao ni;

J.J Maseba, Madugu,

A. S Mwami aliyekuwa Mwambata India,

R. K Kapinga,

C.D Katenga,

Z.S Kiwenge,

M.A Mugambo,

A.A Alfonsi, alikuwa Mwambata Zimbabwe

A.P MUTA, alikuwa Mwambata Marekani

A. Chakila,

M.G Mhagama,

V.M Kisiri,

C.E Msola,

S.M Mzee,

C.J Njiege,

A. Muhona,

R.C Mumbi

SJ Mkande,

Sibuti,

M.M Mwanga,

I.S Ismail.

Mwingine ni M.N Mkelemi ambae kwa sasa ni mpambe wa Rais na kwa cheo hicho Jenerali Mabeyo amemuomba Rais ampangie kazi nyingine.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali.

Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.

Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.

Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1 kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu, J.J Mwaseba, A.S Mwamy, R.K Kapinda, C.D Katenga, Z.S Kiwenge, M.A Mgambo, A.M Alphonce, A.P Mutta, A.V Chakila, M.G Mhagama, V.M Kisiri, C.E Msolla na S.M Mzee.

Wengine ni C.J Ndiege, I.M Mhona, R.C Ng’umbi, S.J Mnkande, A.C Sibuti, M.M Mumanga, I.S Ismail, M.N Mkeremy, G.S Mhidze, M.A Machanga, S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E Gaguti.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Luteni Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Kanali na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais (Aide de Camp – ADC)

Kanali Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka Naziad Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

12 Aprili, 2018

Soma: Mpambe wa Rais Magufuli abadilishwe
 
Kanali mkelemi sio tena ADC wa mukulu,anakuja kanali mwingine" sawa, kwani ukiwa brigedia general huwezi kuwa ADC wa presidar?
Wanaofahamu mambo ya inteligencia watujuze
cc. Brother GENTAMYCINE,na wengineo
Brigadier kimsingi anaongoza brigedi au kikosi-jeshi or equivalent na sio kuwa mpambe wa kiongozi. Mtu mzito sana huyo.
 
Kwa hyo mkuu wa wilaya alitolewa jeshini, akapewa a political post, kisha amerudishwa jeshine with high range military post aendelee kutumika kama mtumishi wa jeshi?

Mtu akidema jeshi letu lishakua compromised na wanasiasa bado watu wanapinga.

Nchi masikini haziendelei kwa sababu nyingi sana.
Hahahaaaa!!!Mkuu wee acha tu huu ni uoga wa serikali
 
Back
Top Bottom