Mabadiliko haya TRA aliyoleta Rais Magufuli hata aondoke leo yatadumu milele

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
825
246
Kwanza kabisa nianze na swali, Kwa kasi hii ya mabadiliko katika mifumo mbali mbali hasa TRA, BRELA, BOT je kipindi cha nyuma tulikuwa hatuna watanzania wenye akili ? ama watu waliamua kuwa vipofu.

Kama msomi na mchumi katika vitu ambavyo amefanya Raisi Magufuli ambavyo sitasahau ni

1. MABADILIKO TRA
a) Asikuambie mtu sasa hivi TRA kuna vijana wadogo makini na wenye uchu wa kuimarisha uchumi wa nchi, MFUMO WA DIGITALI umerahishisha ukusanyaji wa kodi. Mfano sasa ukienda TRA lazima wahitaji mkataba wako, hapo inaamana direct mwenye nyumba nae atatafutwa kuhakiki amelipa kodi.


b) Process za Control Verfication ya VAT imemaliza tatizo la fake receipt na watu kutokulipa VAT

C) Process za Examination of returns and account ni kitu kilikuwa kinafanyika kwa makampuni makubwa naona sasa limerudi kwa makampuni yote Tanzania. Hii imesaidia sana TRA kupata pesa na wale wategaji, haya mabadiliko yatasababisha hata vijana kupata ajira sasa.

LAKINI BADO TRA MNA HAYA YA KUFANYA KUIMARISHA UKUSANYAJI WA KODI NCHINI
  • NINI KIFANYIKE KUKUZA TAX DATA BASE
Tanzania kwa sasa ina TAX BASE 12.8 kwa idadi ya watu 50m, ukilinganisha na Kenya in TAX BASE 18.5 kwa idadi ya watu 40m tu. Nini kifanyike

  • MFUMO WA UGAWAJI TIN KWA WATU WOTE WENYE MIAKA 18 NA KUFILE RETURN KILA MWAKA HATA KAMA MTU HAJAANZA BIASHARA
Nchi za wenzetu pale tu mtu anapofikia umri wa miaka 18 anapatiwa namba ya utambulisho wa mlipa kodi kipindi akipatiwa kitambulisho cha utaifa. Hii ni muhimu tuanzishe hapa Tanzania itasaidia sana ukusanyi wa kodi lakini pia kuleta hamasa kwa generation ijayo kujua kodi ni nini na ni lazima.

Kwa sasa hapa Tanzania unaweza ukakuta mtu aan mali za mpaka TSH 5 Billion lakini hana TIN number au analipa kodi ndogo sana au hajawahi kulipa kodi, hii inakuwaje chukulia mfano hapo chini wa MR X.

MR X amemaliza chuo lakini hajaingia kwenye ajira rasmi, ameachiwa mashamba na nyumba za kupangisha na baba ake, mashamba na nyumba zipo eneo ambalo halijapimwa, MR X anaweza amua uza mashamba kwa million 100 hadi 200 bila kulipa kodi, MRX atakuja kuchukua TIN number kwa ajili ya umiliki wa gari tu na sio TIN ya biashara. MRX atajenga nyumba atapangisha na ataendelea kuchukua kodi za wapangaji bila (WT) kwa kuwa ni ngumu kumpata. MRX anaweza akawa Tajiri bila kuwa na TIN ya biashara.


Lakini TRA ikianzisha mfumo wa kila mtu kuwa na TIN na kufile Return mwisho wa mwaka, ni rahisi kwa MRX kusema kwamba kwa mwaka huu nilipata pesa hiikutokana na kuuza shamba au kupangisha nyumba, nah ii inaweza kuwa rahisi TRA kuuliza MR X kama unaweza miliki gari na matretka mbon hulipi kodi.

Chukulia Mfano pia MRX amemaliza chuo amepata ajira isiyo rasmi, MRX anaweza fanya kazi kwa miaka 2 akapata mpaka million 30 akaamua kununua gari na kujenga nyumba lakini bila kulipa kodi yoyote, swali ni Je amewezaje kupata million 30 bila kulipia kodi, jibu ni rahisi, labda alifanya kazi akawa analipwa bila (WITHHOLDING TAX) au kulikuwa na WT sema yeye hajafile return za kila mwaka kuonesha sources za income.

Mwisho, Tax base itaongezeka endapo tutaweka mfumo wa kila mtu kufile return hata kama ni NIL return, hii itapelekea mapato mengi yakusanywe ambayo yalikuwa yanapotea.

Kwa kifupi ile notion kwamba hii ni TIN ya leseni tu sio ya Biashara lazima iondoke, mtu kama ana TIN lazima afile return kila mwaka hata kama ni NIL returns.

Kurahisha hili mfumo huo unaweza kuwa online.

  • MFUMO WA RETURN UWE HATA KWA WAFANYAKAZI WANAOLIPA PAYE
Ni desturi imejijenga kwamba kama mtu anafanya kazi ya ziada mapato yake anakuwa hayatolei taarifa kwa kuamini kwamba tayari analipa kodi PAYE kupitia kwa mwajiri wake. Mfumo wa kufile Return lazima uwe kwa wananchi wote hata kama mtu analipa PAYE, hii itarahisha mtu kuweza kulipa kodi kwa mapato ya ziada anayopata nje ya mshahara, mfano kama anapokea kodi ya nyumba au kama amefanya consultancy etc.

  • NIN KIFANYIKE KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI
  • UJUZI WA WAFANYAKAZI NA MAFUNZO YA MARA KWA MARA KATIKA FIELD ZINGINE
Katika kila ofisi ujuzi wa wafanyakazi ndio tija muhimu katika kila jambo, kwa muda ambao nimefanya kazi na kuengage na wafanyakazi wa TRA nikiri kwamba kweli baadhi wana uelewa wa masuala ya kodi lakini wengi wako limited, mfano mfanyakazi wa department moja ukimpa scenario ambayo sio yake hawezi kukujibu. Swala la kodi ni swala Mtambuka ni vyema watumishi wa TRA wakawa na uelewa mtambuka pia, hii itawezakana kama kutakuwa na mafunzo ya mara kwa mara ya mwendelezo katika masuala tofauti mfano Corporate management and law, Land law and real estate, tourism etc.

Katika utafiti wangu katika baadhi ya ofisi, nimegundua baadhi ya watumishi kuwa wazuri lakini uelewa mpana wanakosa na hii ni kutokana na Mfumo ulivo TRA.

Mfano: Nilienda ofisi moja nkakutana na afisa senior tu, nkampa scenario kwamba nafanya Biashara, muda huhuo nafanya consultancy na muda huo huo na pokea kodi za nyumba za kupanga, nkamuuliza sasa je baada ya kupokea kodi ya nyumba na mpangaji amesha WT 10% mimi na haja ya kureporitia TRA, akajibu mpangaji akishalipa 10% ndo mwisho.

Ni muhimu sana kwa wafanyakazi waliopo na ambao wanaanza kupewa crach program kuhusu mambo mtambuka ya kodi, hii itawarahishia kuweza kufanya uchambuzi wa mambo.

Pia TRA ianzishe Continous learning programe mfano wafanyakakazi kujifunza mambo mapya kama Transfer pricing, Trade mark and royalties, land law and taxation, company management and Taxation etc. Na katika hili ni vyema wawezeshaji wawe ni watu kutoka private sector kuweza kubadilisha ujuzi.

  • KODI ZA MAJENGO HASA WITH HOLDING NA FINAL TAX
Tanzania hasa Dar es Salaam na mikoa iliyoendelea kuna nyumba nyingi sana za kupanga, lakini ni watu wachache sana wanalipa With holding Tax kama wapangaji na kama wenye nyumba kulipa final tax kutokana na mapato anayopata.

Kwa Dar mfano mtu anaweza akawa na nyumba za kupanga 20 zote anapokea kodi cash na hakuna WT wala final return anazofanya. Na wengi baada ya kuona ukimiliki nyumba kama individual hakuna wa kukusumbua wengi hawawezi kuanzisha kampuni ya real estate utakuta ana nyumba 10 zote amepangisha na hakuna mpangaji analipa WT wala yeye kufile final return, hili ni eneo ambalo TRA wakitilia mkazo na litaongeza Tax base na mapato.

ASANTENI
 
Ushauri wako mzuri lakini kumbuka kuikumbusha na serkali yako inayopokea kodi zetu kuwa kodi nizetu sote tunalipa kwa usawa lakini mgawanyo wa keki hauendi sawa ndiomaana unakuta mkoa mmoja uko mbele kimaendeleo na mwingine uko nyuma sana.

Pili rudi kwenye mambo ya msingi kama afya ambayo nimatokeo ya kodi zetu hospital hakuna madawa tunatozwa pesa nyingi tunaambulia vidawa vya kutuliza maumivu.

Kwanini kodi ikikusanywa huduma ya afya isiwe bure?

Tatu rudi "Elimu" inayotolewa iko chini ya kiwango kiasi ambacho vijana wanaliza Elimu ya secondary hawawezi kujitegemea kutokana na mitaala mibovu isiyoendana na mazingira matokeo yake mlipa kodi analazimika kulipa pesa nyingi kumpeleka mtoto Privet school,

Mtoa mada twambie moyo wa kulipa kodi tutautoa wapi?

Mwisho nikukumbushe unafurahia kukusanywa kodi lakini hutaki kujielekeza zinapokusanywa zinaenda wapi? Tumeshuhudia CAG akihoji upotevu /matumizi yasiyojulikana kwa zaisi ya Tilion 1.5 matokeo yake alitolewa kwa mbinde mpaka leo Bunge linaelekea kuvunjwa wamekaa kimia

Lakini pia tunaona matumizi ya kodi zetu zinavyotumika kuimarisha chama kimoja kwa kununua wapinzani ushahidi uko wazi, tunashuhudia serkali inavyotawanya kodi zetu kwa kuwafungulia wakosoaji wake makesi yasiyonakichwa wala miguu matokeo yake mawakiri wanalipwa fedha lakini wanabwagwa mahakamani.

Kana kwamba ilo dogo vijana wetu vyuo vukuu wananyimwa mikopo ambayo ni haki yao, ata tukiwalipia kwa kuuza mashamba na mifugo yetu bado wakimaliza ajira hakuna wanarundikana mitaani.

Afu wewe jamaa huna haya nipate wapi moyo wa kulipa kodi ambayo sikutani nayo katika maisha yangu ya kila siku?

Kodi nitalipa nikibananishwa sivinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani mwanzo tulikuwa watumwa kwa mkoloni ccm sasa tumepata uhuru kutoka kwa magufuli au unamaanisha vipi hapo
 
Ushauri wako mzuri lakini kumbuka kuikumbusha na serkali yako inayopokea kodi zetu kuwa kodi nizetu sote tunalipa kwa usawa lakini mgawanyo wa keki hauendi sawa ndiomaana unakuta mkoa mmoja uko mbele kimaendeleo na mwingine uko nyuma sana...
TARATIBU TUTAFIKA

MAWAZO MAZURI
 
Safi kabisa, unapongeza,unakosoa na unashauri. Wewe ni kati ya watu wachache walioelimika.
 
Back
Top Bottom