Mabadiliko hata ndani ya ccm yanawezekana...

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
313
7
Ni katika utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua wengi sana tunahitaji mabadiliko ya hali ya kisiasa,kiuchumi,kijamii na hata ya uongozi katika nchi yetu ye Tanzania.
walio madarakani, na wale walioko nje ya madaraka wanakubali kweli ipo haja ya mabadiliko lakini wengi wetu ni waoga wa kujitokeza na kuonyesha njia au kuanzisha mabadiliko hayo....wengi ni waongeaji wazuri,washauri wazuri tena hat hapa JF tuna watu very competent when it comes to need for change...lakini tunaishia kuandika tu na ku-comment tu...ni wachache wajasiri ambao hata ID zao wameziweka wazi.

hata viongozi wetu, wawe wabunge, mawaziri, makatibu wakuu, viongozi wa dini bado hawajakuwa na ujasiri wa kujitokeza hazarani na kuonyesha njia japo kwa wale wachache waliojaribu hivyo wamejikuta katika upinzani mkubwa sana....

Je tatizo ni CCM kama chama, Uongozi? wanachama? sera?
kwa utafiti wangu mdogo...CCM ni chama kilichojidhatiti sana katika kila kona ya nchi, ina matawi active mengi sana na wanachama hai na wasio hai wengi sana...lakini kikubwa zaidi ni kwamba watu au wananchi sehemu nyingi hawaoni kwamba kuna haja ya mabadiliko na wanamuona yeyote yule anayekuja na kitu kingine zaidi ya CCM ni msaliti na hawamuungi mkono...wapo watu vijijini na sehmu nyingi za nchi wanaakiamini sana chama cha CCM na wapo tayari kumuunga mkono mgombea yeyote atokanaye na CCM bila kujali wasifu wake au historia yake...

Na hili ndio litakuwa kikwazo kikubwa sana kwa wale wote wapenda mabadiliko ambao wameona wanataka kuleta mabadiliko kutoka nje ya nyumba ya CCM, watakumbana na upinzani mkali kwakuwa wapiga kula wengi vijijini hawana mwamko wa mabadiliko....ipo sehemu moja ambapo waumini wa dini moja waliamua kumchagua mgombea wa dini nyingine kwakuwa yule ambaye ni dini yao alikuwa yuko chama kingine cha siasa na sio CCM...hapa si maanishi kuingiza udini ila nikuonyesha kwamba ni jinisi gani CCM ilivyomioyoni kwa wananchi....hii hali itawafanya wale wanamabadiliko wana mitandano washindwe kufanikiwa kufikia azma yao pamoja wasifu wao mzuri na nia njema waliokuwa nayo ya kulea mabadiliko....

CCM si jiwe au mti, ni chama kilichoanzishwa na watu, na hivyo basi mabadiliko yanawezekana ndani ya CCM, wakitokea viongozi wanaoona hali ilivyo na kuonyesha muongozo basi wakiwa wengi wanapewa....wakati mwingine mabadiliko hayaji kutoka nje...huanzia ndani...Kinachotakiwa tu ni kwambwa watu wawe wajasiri, waache unafiki wa ndio wakati ni hapana,na tuamini kwamba tupo kwenye demokrasia kwahiyo tuwe huru Kwa kutoa mawazo yetu wazi na wale wanaotuongoza wajue sio miungu bali ni binadamu ambao wanakosea, wawe tayari kusikiliza na kutumia busara zao kupokea Ushauri mbalimbali....sio kama ilivyo sasa wakiongea wananchi inaonekana ni ni uchocezi na wanakemewa na viongozi waliokuwepo madarakani...

ni ushauri wangu kwamba tukiwa kama wanachama wa CCM tunaweza kuleta mabadiliko kupitia ndani ya chama chetu na sio kusubiri watu wa-nje kuleta mabadiliko...kwa wale wapiganaji wenzangu mi ninawashauri kwamba tukiwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko.....tena ndani ya chama....CHANGES ARE FOR THE BETTER AND ARE INEVITABLE...CHANGES BEGIN WITH YOU....

HALELUYAH..
ni mtazamowangu tu...
 
Back
Top Bottom