Mabadiliko daima yanahitaji kujitoa kwa jasho na damu. CHADEMA eleweni kuwa hata Lowasa alikuwa anahubiri mabadiliko haya ndio maana karudi CCM

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Watu wanaombeza Rais Magufuli kwa kutuletea mabadiliko haya, uwa siwaelewi wanamaanisha nini hasa. Watanzania kama mna kumbukumbu nzuri, wagombea wote wa urais mwaka 2015 kupitia CCM na CHADEMA walitangaza mabadiliko na hata kufikia CHADEMA kuimba mabadiliko Lowassa kwa kuzungusha mikono.

Vyama vyote vilikuwa vinataka kuwapa watanzania mabadiliko na ndio ulikuwa msingi wa kampeni za 2015. Na ukweli ni kwamba mabdaliko ya kweli yanahitaji kujitoa kwa jasho na damu ili yapatikane. Je, ni mabadiliko yapi CHADEMA ambayo mlipanga kumletea mtanzania chini ya Lowassa kama angekuwa rais bila jasho na damu?

Maumivu ya kupata mabadiliko ni makubwa kuliko kuchomwa na msumari na Rais Magufuli anachofanya ni kuubadili mfumo mzima ambao ulikuwa unamcheleweshea mtanzania mabadiliko. Sisi kama mtanzania hatuna budi kumpongeza hata kama huo mfumo ulikuwa unatunufaisha kwa sababu kwa mfumo mpya anaotengeneza kila mtu anafaidika na ndio mabadiliko hayo.

Ndio maana mgombea urais wa CHADEMA 2015 kaamua kurejea CCM ambapo anaona mabadiliko aliyokuwa anataka kumletea mtanzania yanaletwa na Rais Magufuli. Haya ndio mabadiliko ya kweli ambayo hata Lowassa kaona hayawezi kupatikana CHADEMA, CUF au ACT ila CCM tu na kwa Rais Magufuli.

Daima nina Imani na CCM na katika hili la Mabadilko ya kweli nina Imani na Rais Magufuli na ninaomba watanzania wenzangu muwe na Imani na CCM na Magufuli kwa kuwa bado kitambo kidogo tu tunaingia Kaanani katika nchi ile yenye wingi wa Maziwa na asali. Hata wana wa Israeli walipokuwa wanaelekea Kaanani walivumilia mengi ila walifika.

Tuwe wavumilivu kwa kuwa dhamira, nia na uwezo wa kuvuka hapa ipo na rais Magufuli anayo, tumuombee tu uzima na kutuvusha hapa na pia, nawakumbusha kuwa Mabadiliko yananhitaji uvumilivu na kujitoa hasa hata kwa damu.
 
Back
Top Bottom