Elections 2015 Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
Wanabodi,
attachment.php.jpg
MMGL2160.jpg


Kama ilivyo kawaida yetu jf, wewe kama mwana JF, una pata ile kitu inaitwa the jf advantage to "be the first to know" kuwa ujio wa Lawassa kujiunga Chadema, sio tuu utakipaisha Chadema to unimaginable dimentions kutokana na ufuasi mkubwa wa watu walio nyuma yake, bali ujio huo, unaandamana na neema kubwa na neema tele za mambo mengine mengi makubwa na mazuri kwa Chadema, na moja kubwa ni kwa Chadema kuhama kwa Makao Makuu yake toka kwenye kale kajumba kalichopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam, ambako hakuna hadhi ya makao makuu ya chama kikuu cha upinzani, yatahama kutoka hapo Mtaa wa Ufipa hadi kwenye eneo jingine lenye hadhi na nafasi zaidi ili angalau kufanania!.

Hii ni kufuatia idadi kubwa ya watu wanaotarajiwa kujiunga na Chedema kufutia ujio wa Edward Lowassa kwenye chama hicho.

Hali hii ni kufuatia hali iliyojitokeza jana, wakati Edward Lowassa alipofika Makao Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema, kufuatia umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema kufurika kwa wingi hali iliyoleta shida na kero kwa majirani mtaa mzima, kutokana na location ya ofisi hizo zilipo eneo lililozunguka ofisi hizo ni eneo dogo kufuatia ofisi hizo kuwepo kwenye eneo la makazi ya watu. Na hapo hao waliojitokeza ni wafuasi tuu wa Chadema, bado tsunami ya wafuasi wa Lowassa hawajatia timu!, wakitia timu kama hali ilivyokuwa uwanja wa Sheikh Amri Abedi, then Mtaa wa Ufipa, unahatari ya kudidimia na kuzama, huku nyumba zikipata nyufa hivyo sio tuu kuleta bughudha ya umati mkubwa wa watu bali pia ni hatari kwa maisha ya watu kuweza kusababisha janga la kitu kinachoitwa stampede!.

Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imekuwa ikipokea, ukajumlisha na zile fedha za Sabodo alizoipa Chadema kujenga ofisi za makao makuu zenye hadhi, na kulinganisha ruzuku hiyo imekuwa ikifanyia nini, utakubaliana na mimi, kuwa fedha hiyo, ingetosha kabisa kujenga jengo jingine la maana na lenye hadhi kwenye eneo la kutosha. Hali hii imetokana na upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hali iliyopelekea matumizi mabovu ya ruzuku, kama yalivyofafanuliwa kwenye ripoti ya CAG.

Mabadiliko hayo chanya ya ujio wa Lowassa sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, bali pia Chadema itamiliki media zake yenyewe kikiwepo kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki by proxy, familia kubwa ya media, yenye vituo vya Redio, TV na magazeti lukuki!, hivyo sasa pia vitatumiwa kuisupport Chadema kwa kuanzia tuu, wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.

Ama kweli mgeni njoo, mwenyeji apone!.

Hongera sana Lowassa!.

Hongera Chadema.

Ikulu 2015 ni ya UKAWA!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Source ya Taarifa hii ni observation yangu binafsi.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu nchini (CAG) amebaini mapungufu katika vitabu vya mahesabu ya CHADEMA na kuhitimisha kwa kuipa CHADEMA hati yenye mashaka &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Qualified opinion' kutokana na mahesabu yake ya mwaka wa fedha unaoishia Ju June 30, 2013.

1)Pamoja na mambo mengine, katika mwaka wa fedha uliomalizika June 30, 2012, CHADEMA ina akaunti zaidi ya 200, ikijumlisha akaunti za Makao Makuu, Kanda, Mikoa, Wilaya na Majimbo lakini Mkaguzi hakuona salio la kufungia kitabu likihusisha akaunti zote zinazotumia jina la CHADEMA.

2)Mkaguzi anasema katika ripoti hiyo kuwa Chadema kilionyesha kina mali zenye thamani zaidi ya Sh650 milioni, ambazo ni magari, mashamba, nyumba na pikipiki. Hata hivyo, CAG anasema hakuona kitabu cha usajili wa mali hizo.

3)Mahesabu ya mwaka unaoishia June 30, 2013 yalionyesha shilingi milioni 40 ambazo hazikuwa na vitabu vyenye mahesabu ya makusanyo yake.

4) CAG alihoji manunuzi ya magari 10 (Ford Ranger) yaliyofanywa bila kuhusisha Kamati ndogo ya chama inayohusika na utoaji wa zabuni za chama (Tender Committee).

5) CAG alihoji ununuzi wa generator yenye thamani ya shilingi milioni 27 bila kuhusisha mchakato wa zabuni.

6)CAG alihoji pia mahesabu yanayoonyesha deni la milioni 47 linalohusiana na vifaa vya ujenzi wakati hata havijawasili kutoka kwenye kampuni ya kichina.
NB. Japo Pakali ni mwanachama wa chama cha siasa, na ni kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, huyu ni kada mzalendo wa kweli wa taifa hili kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kazi yangu ni to tell nothing but the truth, with objectivity, impartiality and balance from all sides!.
 
Pasco

Mkuu Pasco unataka niamini kwamba ulikuwa hujui kuwa CHADEMA wanapanga pale ufipa au ndio michimbezo ya kumpata mgeni?
 
Last edited by a moderator:
Lowassa....Chademaaa, Ukawaaaaa....yaani tunabadili gia juu kwa juu...yaani Ukawa wamecheza game hili kama MESSI VILE... maana ushindi wa kishindo ni saa 2 asubuhii...

Maskini CCM hawa hawajui nn kinaendelea, wako ktk coma...butwaa...wanakanana wenyewe kwa wenyewe...daahh..!!
 
Pasco bhana,
Anyway,hata ukiongea common sense tu,nitakuheshimu,regardless ni fact or not. Kwamaana uyanenayo mengi huwa. Hivyo tutegemee jumba la HQ lenye hadhi ya El-premier!
 
Last edited by a moderator:
Chadema kilikuwa chama cha Ukombozi mpaka alipoingia Lowasa sasa kimekuwa Chama cha Matumaini! Kwa chama cha matumaini, ni vizuri wahamie kwenye magorofa marefu kule Samora ndo kwao. Wawaachie wakombozi ufipa yao!
 
Back
Top Bottom