Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Daah jamaa yangu naish nae pamoja jana usiku katoka maskani kwao huko kavuta sijui msuba wa wapi
Cha ajabu badala ya kukaanga mayai akaanza kukaanga nanasi
Kitimtim chake hadi majirani waliamka


[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Ok, kwa leo nitakufundisha kupika tambi za nazi.
Kama hujui kukuna nazi, tumia hata nazi ya pakti ya Azam.Ila nazi yenyewe ya kukuna ndio nzuri zaidi.

Fuata step hizi:-
1. Katakata tambi zako size unayotaka, wengine hukata mara 2, 3 au werevaaa kisha ziweke pembeni.

2. Weka mafuta ya kula jikoni kwenye sufuria, yakichemka tia vitunguu maji, tia kitunguu saumu punje 3 au 4 zilizopondwa, tia iliki punje 3 zilizotwangwa, tia chumvi, kisha weka na ufuta au food color nusu kijiko cha chai. (ufuta na rangi si lazima ni katika kutia nakshi tu).

3. Endelea kukoroga mchanganyiko wako mpaka utakapoona umekolea na kila kitu kimewiva, kisha baada ya hapo tia sukari vijiko viwili na nusu.

4. Baada ya kutia sukari, sasa tia tambi zako ktk mchanganyiko wako na endelea kuzikoroga taratibu km dk 2-3.

5. Baada ya hapo tia tui la nazi, kama unatumia nazi ya Azam, chukua maji kiasi, tia nazi ya Azam yote, koroga kisha miminia jikoni kwenye tambi zako.
Kama unatumia nazi ya kukuna, tia tui la pili kidogo sana na acha ichemke.

6. Tambi zikianza kulegea, tia tui la kwanza la nazi ya kukuna, hapa wa nazi ya Azam ahusiki maana yeye keshatia kipakti chote awali.

7. Endelea kugeuza mpaka utakapoona tambi zako zimeanza kutoa udelele (urojo) ujue zimewiva.
Onja ili kujua kama sukari na chumvi vimekolea.
Hakikisha sukari na chumvi havizidiani, viwe na uwiano sawa.

8. Baada ya hapo, punguza moto ili zikauke.
Kisha epua na pakua tayari kwa kuliwa.

ANGALIZO:-
Kipimo cha chumvi na sukari inategemea na uwingi wa tambi zako.
Kama utatumia nazi ya Azam, koroga nazi yote na uiweke yote, ukianza kuweka maji halafu ndio tui, tambi zako hazitakolea nazi sawasawa

Tambi za kuliwa na nyama, samaki au mboga yenye asili ya nyama nyama, sukari haitakiwi kuizidi chumvi.
Ila tambi za kuliwa kavu au na chai, uwiano wa chumvi na sukari uwe sawa.
Tambi za kuliwa na uji, sukari isiizidi chumvi.
Tambi za kuliwa na chai yenye kahawa, sukari inatakiwa iizidi chumvi kidogo.

Epuka kukoroga koroga tambi zikiwa jikoni ili kuepuka tambi kurendemka (kurojeka).
Ukiona tambi zinashikana chini (kuungulia) punguza moto.
Naomba hiyo Saturday ukipika, ulete mrejesho, usi-google
Hee hee sante sana madam
Hapa nmekusoma sawasawa

Na ntaleta mrejesho hapa
Nikishapika

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Hee hee sante sana madam
Hapa nmekusoma sawasawa

Na ntaleta mrejesho hapa
Nikishapika

[Color= yellow]Triple A[/color]

Haya kaka angu.
Nitafurahi ukileta mrejesho hapa ili tupime uwezo wako wa kukarangiza
 
Chakula chochote ambacho kinachukua zaidi ya lisaa limoja kuiva
Muda kwangu ni bidhaa adimu sana

karma is a bitch
 
Sijawah pika pilau mzee sababu sijui hahaahha

Chapat napenda kichiz ila siwez pika gheto hata siku moja
 
Kitu ambacho mabachela wengi wanachokiweza ni kuchemsha chai ya rangi na kupika tambi tu.
Kataeni au mkubali.
% kubwa ya wanaomudu kupika baadhi ya vyakula ni aidha wale waliokulia kwa dada zao au walioondoka kwenda kuanza maisha wakiwa wametoka makwao (kwa wazazi wao) wakiwa 22-25+.
Waliobaki wote ni tambi na chai ya rangi tu
Hahahah fact
 
Nina imani mabachela tuko wengi sana humu.

Katika suala la kupika na kuosha vyombo huwa ni habari ingine. Vipi wewe mkuu ni msosi gani kuupika au kuuandaa huwa unakupa mawazo sana japo unaupenda. Na ukiula mahala unahisi umekosewa kupika sio kama ungeupika japo hujawahi kuutest geto.

Mimi bana WALI naupenda ila kuuandaa hadi utoke ni hatari sana. Halafu nikiwa nakula kitaa huwa mwepesi sana kuwalaumu wahudumu wali haujaiva au wamepika bokoboko au una mawe.

Wewe je msela wa geto nini kinasumbua jikoni?
Mimi Juzi kati nilivyatua pilau matata sana mpka nikaishia kuona aibu mana mshkaji aliniona nimetoka nje kidgo akaniulza vp shemeji yupo leo daah ikanibidi nipotezee ndio yupo mana kitu kiliita hatareee
 
Mimi Juzi kati nilivyatua pilau matata sana mpka nikaishia kuona aibu mana mshkaji aliniona nimetoka nje kidgo akaniulza vp shemeji yupo leo daah ikanibidi nipotezee ndio yupo mana kitu kiliita hatareee

Hahhahaha kwamba pua raia ziliwavimba baraaa
 
Ila kuna wakati mwingine ata wadada wali unawashinda. Maana mara nyingi sana nikiingia mgahawani naborekaaa.
Wali ni kuupika ni mtihani mkuu, yaan tangu kuupanda kwenye majaruba hadi kuupika ni mtihani!

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom