Mababu zetu walitangulia mbele za haki kabla ya Wamisionari na Waarabu kuleta dini wanahukumiwaje?

Mpanda nyangobe

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
709
1,558
Ni swali hili. Kama tujuavyo wageni weupe wameanza kuja Tanganyika kwenye karne ya nane.

Ikumbukwe hawa wageni ndio wameleta ustaarabu wa dini hizi tulizonazo sasa ambazo tunaambiwa zitatufikisha mbinguni kwa baba.

Swali: Je, ambao wameshafariki kabla ya kuja dini hizi watahesabika kama wasioamini au inakuaje?
 
Watahukumiwa kulingana na kile walichokuwa wanadhani ni sahihi kwao. Hapo zaman pia kulikua na mila na desturi kun jambo ulikua ukifanya unaonekana umekosea..so sheria zao ndo zikazokua zinahukumu. Ushawah jiuliza kama hiki tunachoamini sio sahihi itakuaje pia. Je, kama sisi ndo tunakaidi na wenywe ndo walikua sawa
 
Sio mababu tu mpaka leo kuna jamii huko misitu ya Amazon azijui kuna binadamu tunaishi kama sisi kwaiyo ukijichanganya huko unaweza kuta ukawa mboga.
 
Watapotwezwa maana utawahukumu vipi wakati hawajui chochote watatoweshwa kama hawakuwahi kuwepo duniani...kimbembe kwa kina sie maisha magumu huku unatakiwa kuwa mwema Bora wazungu kwao mteremko hata wakiukumiwa ni sawa tu ila hii haipo fair.
 
Hivi mna uhakika gani kwamba hizi dini zilizoletwa na weupe ndio sahihi. Maana ukiangalia hao waliozileta na mazingira ya kuzileta kuna maswali mengi. Kwanza walikuja kikatili , wakazitumia kutulainishi ili tuwatii kirahisi lakin na kutuuwa na kutuibia. Je una uhakika gani mtu aliekuletea dini kwa mazingira haya kwamba alikuletea kitu sahihi.
 
Na imeandikwa " Mimi ni njia na uzima, ukipitia kwangu umemuona Baba (Mungu)" Sasa mababu zetu walipitia kwa nani? Ina maana wapo motoni?
 
ALLAH SW ahukumu mtu ambaye hakufikishiwa ujumbe,yeye si Kama wale ambao hawafikishi elimu ya Sheria kwa watu Kisha huwahukumu kwa makosa ambayo hawakujua no makosa
 
Na imeandikwa " Mimi ni njia na uzima, ukipitia kwangu umemuona Baba (Mungu)" Sasa mababu zetu walipitia kwa nani? Ina maana wapo motoni?
Neno la Bwana linasema “utahukumiwa kulingana unavyojua sheria na kuto kujua sheria “hukumu ipo pale pale kwa babu zetu

Hata Mtoto mchanga au aliye tumbona mwa mama anaweza kwenda Motoni kuhukumiwa.

Mtoto anapokuwa Tumbo mwamama au Mtoto Mchanga anaweza kufundishwa uchawi, anaweza kupangiwa majukumu ya kuua na akayatekeleza na roho yake inaongea kwenye vikao vya kichwi na kupanga uharibifu na kunywa damu ya binadamu.

Neno la bwana linasema Mbinguni wataingia kitakatifu. Kama Mtoto kaua kwenye ulimwengu wa kichawi rohoo yake imepoteza sifa za kuwa kitakatifu

Mwanamke anapopata mimba aende kwa mchungaji wa kweli apeleke sadaka mimba iombewa kuzuia uchawi na mapepo ,akizaliwa pia utaratibu huo.

Mtu atahukumiwa kulingana anacho kijuwa na hasi kichuwa
 
Kama baba zetu walihukumiwa kwa kutokumjua Yesu, acha niendelee kufuata mila zao na kuachana na huu utamaduni wa kizungu ili nikakutane nao huko motoni. Nasikia huko motoni unaumia siku za mwanzo tu na unazoea. Utatamani hata uwe kiranga wa kukata Kuni ili moto usipungue.
 
ALLAH SW ahukumu mtu ambaye hakufikishiwa ujumbe,yeye si Kama wale ambao hawafikishi elimu ya Sheria kwa watu Kisha huwahukumu kwa makosa ambayo hawakujua no makosa
Kwa hiyo wakristo wote ambao kiuhalisia hawana elimu ya Allah SW wanaepushwa na hukumu yake sio?
 
The divine laws are universal. Hata hao mababu enzi zao uzinzi,wizi,uongo nk.vilikuwa haviruhusiwi,,so amri na mafundisho mazuri vilikuwepo Africa tangu mwanzo!
 
The divine laws are universal. Hata hao mababu enzi zao uzinzi,wizi,uongo nk.vilikuwa haviruhusiwi,,so amri na mafundisho mazuri vilikuwepo Africa tangu mwanzo!

vipi kuhusu kuuwa maalbino kwenye jamii kama wamasai kwao ilikuwa sawa zamani vipi hapo wataenda wapi wao
 
ni swali hili...kama tujuavyo wageni weupe wameanza kuja Tanganyika kwenye karne ya nane...ikumbukwe hawa wageni ndio wameleta ustaarabu wa dini hizi tulizonazo sasa..ambazo tunaambiwa zitatufikisha mbinguni kwa baba..swali...he ambao wameshafariki kabla ya kuja dini hizi watahesabika kama wasioamini au inakuaje
Bwana mkubwa. Hakuna dini ya ukweli baba. Dini ni imani yako. Hao waarabu na wazungu walitulazimisha hayo madini waweze kutuchota akili watutawale waibe wawafanye vibaya mabibi zetu na mababu. Juu yako kushobolea lipi. Tumia akili badala ya mihemko na kukurupuka. Period mkuu
 
12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.
Warumi 2:12

14 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
Warumi 2:14

15 Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
Warumi 2:15
 
Back
Top Bottom