Mababu zetu kabla ya wazungu na waarabu hawakuwa wakristu wala waislamu...je walikwenda motoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mababu zetu kabla ya wazungu na waarabu hawakuwa wakristu wala waislamu...je walikwenda motoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by matunge, Apr 11, 2011.

 1. m

  matunge JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu!! hivi sasa nchi yetu imnusa harufu ya udini; ukristu na uislam.Kila mtu anaona dini yake ndo sahihi, na anaamini ndo itampeleka mbinguni. Naomba kuuliza je mababu zetu kabla ya kuja wazungu wala waarabu...walipokufa walikwenda wapi?? motoni ama mbinguni..maana hawakuwa na dini kati ya nilizozitaja.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Dini ni tamaduni. Wazungu na waarabu wanatujaza ujinga na kutulisha kasumba za tamaduni zao. Mtu anaitwa Michael au Mohamed anamcheka mtu mwenye joina la Anyelwisye.
  Je ni nini fahari yetu? Utumwa wa fikra ndio moto wetu wa milele na hii umetolana na sisi kulkumbatia tamaduni za wakoloni.
  India wamepata uhuru wao mwaka 45 lakini utamaduni wao haujaarithika kama wa kwetu, sijui ni nani aliye turoga?
   
 3. E

  ELLET Senior Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hukumu yao ita base Kwenye ile nuru ndogo waliokua nayo kuhusu Mungu. wapo wengi sana tutawakuta mbinguni lakini wakati wa uhai wao hawakusikia jina la Yesu wala Mohamed, ila matendo yao yalikua mazuri mbele za Mungu na jamii waliokua wanaishi. Kuna wale waliokuwepo wakati wamissionari wanaleta injili na hizi dini tulizo nazo, walikua hawajui kusoma wala kuandika na waliamini kila walichoambiwa na kama walikifata kwa hofu ya Mungu na wao watakuwepo. ILA hatari ipo kwangu na kwako, unaye jua kusoma na kuandika, usifuate iman ya babu zako, bila kuchunguza kilicho andikwa kwenye Biblia, Qoran au vitabu vingine.
  Kwa mfano, babu yangu alifundishwa mtoto mdogo lazima abatizwe kwa kumimina maji usoni, ila mimi baada ya kuchunguza niligundua kwamba ni uongo. Je hukumu yangu itakua sawa na ya Babu?
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Yaani swali zuri sana, nimekuwa nikijiuliza nami!
  Kwa maoni yangu, walioishi vyema wanapeta mbinguni; ingawa najua wakristu wengi wataniambia kuwa mtu hawezi kwenda kwa baba bila kupitia kwa mwana ambaye ndio njia'.

  Sio mtaalamu wa dini or biblia, lkn nakumbuka pale Mungu alipowaambia waislaeri kuwa anavunja agano na anatengeneza lingine, ambapo Amri zitaandikwa kwenye mioyo ya watu. So hauhitaji dini yoyote kujua wizi, uongo, uzinzi, uuaji kuwa ni dhambi; hivyo basi wazee wetu walienda mbinguni wale waliofuata Amri za Mungu zilizochorwa kwenye moyo wa kila mwanadamu.
   
 5. k

  kituro Senior Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nashukuru watangulizi wangu kwa michango yeno, mimi nami nakuja na wakwangu!
  kuhusu yesu na muhamadi hawa wote mtu kama ibrahimu na musa hakuwajua wala elia hakumjua yesu ila walienda mbinguni. sababu iliyowapeleka kwa mungu ni kuwa na tabia iliyompendeza mungu na imani au hofu ya mungu. biblia inasema enzi za ujinga mungu alijifanya haoni, lakini sasa mimi na wewe kazi tunayo. ila kwa upande wangu hata ukimjua mhamadi bila kumjuwa Yesu umeliwa au imekula kwako. Yesu ndiye aliyetabiliwa na manabii kama vile isaya. usipompokea yesu awe bwana na mwokozi wa maisha yako imekula kwako!.
   
 6. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Haya mambo kama hamyajui muwe mnauliza tu.... Sio kueleza!! Tazama hapo kwenye nyota!
   
 7. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Mbona mnaulizana majibu uisilamu na ukristo na utamaduni tu na uliletwa na nguvu za kiuchumi na kiutawala .Akili mukichwa! Kama wewe unasoma BIBLIA kasome Yakobo ......Dini safi ni kuwalea wajane yatima.....!
  Hayo mengine mnayo abudu ni utamaduni u na kujilisha upepo ndio maana kanisa siku hizi linanyumbuka kwa kufuata upepeo wa kiuchumi na kisiasa!heabu tafakari ...matukio ya babu kuoteshwa mti ambao unatumiwa siku nyingi,leo kuna watu wanahubiri kwa kutoza viingilio.
  Waafirka tunalazimika kuamka kwenye huu usingizi wa pono
   
Loading...