Mabaa Ovyoovyo: Serikali Inavyokera Wananchi wa Tabata Shue

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
KATIKA kipindi kifupi tu cha sehemu ya pili ya mwaka 2010 eneo la Tabata Shule 'limezawadiwa' kwa hisani ya chama tawala na serikali yake baa zaidi ya 10. Na baa zote hizi hivi leo zinakuwa ni kero kubwa kwa Wananchi ambao si washiriki wa mambo ya kilevi na umalaya unaoendeshwa waziwazi katika maeneo hayo.


Baa hizi zimejengwa katika eneo lenye mahospitali, shule kadhaa na nyumba za kuishi za wananchi. Kama ilivyo kawaida kwa baa yoyote potelea mbali inaitwa Klabu au Cafe au Grocery au Pub na kadhalika tabia na athari zake ni kelele, ulevi na fujo katika eneo husika.


Mafisadi wameamua kuhamishia umalaya uliopo Kinondoni na Mwananyamala hapa kwetu Tabata kwa sababu wanazozifahamu. Wakati baa hizi zina promosheni zake za makelele haitokei hata siku moja umeme kukatika. Lakini wakati wa Uchaguzi Mkuu ilishindikana kuhesabu kura kutokana na umeme kukatika usiku mzima kwa siku kadhaa. Hii inaonesha tu upo uhusiano wa karibu sana kati ya mafisadi hao na mtandao wao wa kichama na kiserikali kuhakikisha kazi yao ya kukiharibu kizazi chetu sawasawa inafanyika bila tatizo lolote ndani na nje ya uwezo wao!

Inaelekea inakuwa ni rahisi kwa baa hizo kujengwa na kufanya kazi kwa sababu baadhi ya wanamiliki ni wanasiasa na maofisa wa jiji.

Serikali yetu ingelikuwa inaongozwa na watu wastaarabu na inasimamia mambo yake ipasavyo isingekuwa inaruhusu baa, magesti na vilabu vya pombe kujengwa ovyo katika makazi ya wananchi.

Serikali hii ndiyo iliyofanikisha kuhakikisha kila mwananchi anakerwa na tatizo la kukosa maji; kisha ikatuongezea tatizo la kukatika umeme ovyo; haikukawia kuhakikisha kuwa usafiri wa kwenda na kurudi kazini na makwetu unakuwa ni kero na mateso makubwa na ndiyo inayoruhusu rushwa maofisini na barabarani kuendelea mtindo mmoja.

Baada ya kuona imefanikisha vyema mambo haya sasa imeanza kutuingilia katika makazi yetu ili kuhakikisha kwamba mabaa, umalaya, takataka, vibaka, makelele, kukosa ustaarabu na ndugu wa kuzikana wa mambo hayo yanakuwa ndiyo majaliwa ya wakazi wa Tabata Shule kama ninavyoamini makazi ya wananchi wengine wa mkoa huu uliolaaniwa na usio na ubinadamu wala utu unaoitwa Dar es salaam

Ingefaa tuiulize serikali kama inajua eneo lenye hospitali (Hospitali ya Tabata na ile ya Prince Ali Farouk) kweli linastahili kelele za kawaida na zile za promosheni.

Je, ni wagonjwa wangapi wanaoteseka kutokana na hali kama hii. Katika majumba yetu kuna vikongwe na malaika ambao sasa hawalali kutokana na fujo za mabaa hayo.

Tunapenda kuiuliza serikali pia je, wanajua, katika eneo hili kuna misikiti na makanisa kadhaa. Je, tutafatiliaje ibada zetu kama kelele zinatoka kila upande na kuvamia nyumba za ibada bila huruma au aibu. Hivi kweli tunaweza kuwalaumu hao wenye mabaa aui wanaostahili kuwalaumu ni wanasiasa na watumishi wa serikali ?

Tunaamini kwamba Watanzania wamekuwa wapole sana kiasi cha kuingizwa vidole machoni na kunyamaza kimya. Lakini serikali isije ikashangaa kero na maudhi haya yatakapopita mipaka na wananchi wakaamua kufanya watakalolifanya. Ikiwa bado kuna watu wenye akili na fahamu zao tunashauri kwamba waanze kulishughulikia tatizo hili haraka kabla nyongo haijaitumbukia serikali na chama tawala.

Leo ni Jumapili ya tarehe 19 mwezi wa Disemba na siku nzima eneo la Tabata Shule linarindima kwa makalele ya promosheni ya kwa mara nyingine baa mpya ya watukufu wanasiasa na mafisadi wetu.

Ni muhimu serikali ielewe kwamba kuna mambo ambayo kwa wengine ni nyama na kwa wengne ni sumu. Jambo linaloendelea hivi sasa ni thibitisho dhahiri kwamba viongozi wetu hawajali mazingira wanayoishi raia zao. Wao huwa wanajali na kutaka tu mazingira yao ndiyo yalindwe. Lakini haitochukua muda kama tabia hii itaacha kuendelea kuona vikojozi wakianza kukojoa pembeni ya Ikulu na baa na magenge yakianza kuenea huko Magogoni.

Ustaarabu na uungwana katika jamii hutokana na utawala wa sheria kutoruhusu starehe ya mtu mmoja au wachache kuwa maudhi kwa wengi. Ni kitu cha kusikitisha kuwa serikali na wanasiasa wetu hadi wa leo wameshindwa kutuwekea utawala wa kisheria utakaohakikisha wananchi walio wengi hawasumbuliwi kwa sababu ya nafasi za kisiasa na fedha walizonazo mafisadi wetu watukufu.

Hali kadhalika, tunauliza je, kweli kuna usalama kwa watoto wetu wanaosoma katika shule za msingi tatu na sekondari tatu zilizopo katika eneo hilo la Tabata Shule ? Na ni kwa namna gani watoto wetu watajizatiti katika masomo huku wamezungukwa na mabaa, kulia na kushoto, nyuma na mbele ?

Labda ni kwa kuwa wananchi mara nyingi wanakuwa wavumilivu na wenye subira kwa kero na maudhi mbalimbali. Lakini niwaulize wakazi wenzangu wa Tabata, je, hivi tunajua kimya chetu kina maana gani kuhusiana na kero na maudhi haya yanayozidi kila siku?

Je, wakati haujafika wa kuepusha watoto wetu na yale yanayotokea katika wilaya ya Kinondoni- umalaya, matumizi ya madawa ya kulevya, vilabu vya ngono huru, ufuska, ulevi wa kupindukia, ushoga na vijana kukosa chembe ya uoga kwa yule aliyewaumba. Matokeo yake ikiwa ni kwa wilaya hiyo kuongoza katika Ukimwi. Je, tunataka Tabata baada ya miaka michache iwe ndiyo inayoongoza kwa Ukimwi jijini. Au tunaweza kuja na kusimama pamoja na kuzikataa balaa zinazoletwa na wanasiasa walioko madarakani leo katika majimbo yetu ya uchaguzi ambao hawakupata ridhaa yetu bali wamechaguliwa na hao waliowachagua juu kwa juu !

Serikali inayoshindwa kudhibiti maingiliano ya watu, iwe ni baina ya walevi na wasio walevi, malaya na wasio malaya, wapigaji kelele na wapenda staha na ukimya, wanaosali na wasiosali, wapenda dunia na wajali akhera sio serikali makini. Ni serikali yenye walakini mkubwa na haiwezi kamwe kufanikisha suala la kulinda umoja, amani na mshikamano wa kijamii.
 
samahani mkuu, naomba kupingana na wewe. Mi nadhani baa, maduka, grocery, migahawa, hospitali, shule nk zote ni huduma muhimu kwa watu. Kama baa zisipotengenezwa kwenye makazi ya watu, zikatengenezwe kwenye makazi ya nini?
 
Hapo zamani nilikwishaishi eneo lenye kero kama hizi. Kelele zilikuwa kubwa hazina mfano!
Tulijaribu kufuatilia intervention ya authority ikashindikana.

Tukaamua kupambana wenyewe. Tukanunua king'ora chenye kelele kali sana kikawa kinapiga pale kuanzia saa 12 jioni hadi baa zinapofungwa! Baa zikaanza kukosa wateja as a result.

The owners eventually opted to settle for a peace talk with their affected neighbours (us). Tukawaambia kero zetu zote na tukawapa masharti kadhaa. Amani ikarudi mtaani, lakini pia baadhi ya vijibaa vikajifia kifo cha asili!

Try that one for size my friend!
 
Tabata Shule kuna mtatizo sana kwa kweli,
Pale Kuna SWISS NIGHT CLUB yaani iko Karibu Kenton High School pamoja na Christ The King Primary&Secondary SchooL,
Sasa mi huwa najiuliza kwa nini wameruhusu huu ufilauni ufanyike tena Karibu na Nymba ya Heshima kiasi hicho!!!
 
Tabata Shule kuna mtatizo sana kwa kweli,
Pale Kuna SWISS NIGHT CLUB yaani iko Karibu Kenton High School pamoja na Christ The King Primary&Secondary SchooL,
Sasa mi huwa najiuliza kwa nini wameruhusu huu ufilauni ufanyike tena Karibu na Nymba ya Heshima kiasi hicho!!!

Sasa hii si night club? na hizo shule vipi day and night pia? Ifahamike kuwa club hukaa sehemu za watu na sio makaburini. Pili kuna utaratibu wa kuzuia sauti na mwisho sheria inasema baada ya mita mia moja kelele ya muziki sii kelele tena. Habari ndio hiyo.
 
Biashara ya pombe duniani inatoa ajira kubwa sana .Tanzania ina makampuni ya bia makubwa 2 na huzalisha creti elfu 4 hadi 10 kwa siku . Unafikiri nani ataziuza kama sio baa maid na barmen kibao ? Bar ziongezwe tupte ajira na burudani .Sasa kama hakuna viwanda tufanyejeeee?
 
Tatizo la mabaa kujengwa karibu na makazi ya watu au watu kujenga makazi karibu na baa ni la kijamii zaidi - It is intertwined in the constraints of aur cultural legacy - Hata Anna Tibaijuka afanyeje - Hakuna authority yoyote inayoweza kuleta mabadiliko katika hili...

BTW: Jana maeneo mengi ya Dar es Salaam kulikuwa na kile wakristo wanahita ubarikio - Mtaani kwetu kulikuwa na familia mbili ambazo watoto wao "walibarikiwa" hiyo jana - Kila mtu nyumbani kwake (kwa wale waliokuwa na sherehe za ubarikio) alifungulia full muziki kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa mbili usiku jana - sijui tofauti ya hii na baa ndani ya makazi ya watu ni nini?
 
Hii kesi haina Hakimu,
Maana hata JK anaamini amesaidia kutoa ajira kwa kina mama!
 
samahani mkuu, naomba kupingana na wewe. Mi nadhani baa, maduka, grocery, migahawa, hospitali, shule nk zote ni huduma muhimu kwa watu. Kama baa zisipotengenezwa kwenye makazi ya watu, zikatengenezwe kwenye makazi ya nini?

Ziende kwenye maeneo ya biashara na burudani. Watu wengi hawapendi bugudha zitokanazo na hayo mabaa.

Usiku watu hamlali kisa burudani za wengine. No way bana. Funga tu hayo mabaa yote yaliyo katikati na kwenye sehemu za makazi ya watu.

Lazima kuwe na utaratibu mzuri na unaoeleweka wa kuanzisha hayo mabaa. Si kuyaanzisha popote tu pale. Hata uyoga haujiotei popote. Una sehemu zake.

Mijitu ya planning and zoning haifanyi kazi zao. Pambaaf
 
Hivi ile sheria ya baa mwisho saa sita, baada ya hapo ziwe ni night club tu ipo bado?
Maana nakumbuka kwetu K'nyama kuna kipindi walikuwa wanakamata tena kwa defender!
Pia night club ziwe sound proof!
Hizi sheria zipo au zilikuwa propaganda tu!
Nisaidieni, tumsadie mwanatabata!
 
Hivi ile sheria ya baa mwisho saa sita, baada ya hapo ziwe ni night club tu ipo bado?
Maana nakumbuka kwetu K'nyama kuna kipindi walikuwa wanakamata tena kwa defender!
Pia night club ziwe sound proof!
Hizi sheria zipo au zilikuwa propaganda tu!
Nisaidieni, tumsadie mwanatabata!

Nchi yetu hii inaendeshwa kwa sheria?

Na hizo sound proof night clubs zitoke wapi? Tehtehteh
 
Usiwe kama hujui siasa. Ilikuwa ni porojo tu. Kuanzia saa sita usiku, wateja wanahifadhiwa mpaka iishe. Na baadhi ya bar kubwa ndizo za hao tunaowapa kura.
 
samahani mkuu, naomba kupingana na wewe. Mi nadhani baa, maduka, grocery, migahawa, hospitali, shule nk zote ni huduma muhimu kwa watu. Kama baa zisipotengenezwa kwenye makazi ya watu, zikatengenezwe kwenye makazi ya nini?

Mzee pamaja na points zako nzuri tatizo liko palepale. Leseni za baa zinatolewa kiholela mno. Hivi kweli night club inapaswa kuwa kuwenye residential houses????...............I doubt!!! Hivi ni kweli baa ni huduma muhimu kwa watu??? Pombe ni starehe...na starehe ni gharama....hivyo sioni sababu ya hiyo huduma humfuata kila mteja kenye mtaa wake. Hamna haja ya kila area/location kuwa na baa 10 mpaka 20. Hapa tatizo ni halimashauri zetu kutoa vibali bila kuwashirikisha wakazi wa eneo husika.
 
Kinachoniuma maeneo kama Tabata,Sinza open space zote wameuza watu wamejenga bar na petrol station,watoto wa siku hizi wanacheza pool table viwanja hamna
 
Back
Top Bottom