Maazimisho ya miaka 50 na gharama zisizo na tija | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maazimisho ya miaka 50 na gharama zisizo na tija

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 28, 2011.

?

yes

 1. yes

  0 vote(s)
  0.0%
 2. yes

  0 vote(s)
  0.0%
 3. yes

  0 vote(s)
  0.0%
 4. yes

  0 vote(s)
  0.0%
 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Asalam aleykum wanachama wa kisima hiki cha fikra,
  Nikiwa mdau na mzalendo wa taifa hili la Tanzania nimepatwa na mstuko mkubwa kutokana na maazimisho ya miaka hamsini ya uhuru wetu,naomba nieleweke vizuri kwa mimi ni mzalendo kwa vitendo,naamini dhamira yangu itanisuta nisipoliweka swala hili bayana.Dhana ya maazmisho hayo si mbaya kimantiki,lakini kinachotia kasoro ni gharama kubwa inayotumika katika maandalizi ya maazimisho haya.hainingi akilini nchi yetu kutumia gharama kubwa kwaajili ya maazimisho wakati watoto wetu wanakaa chini ya sakafu madarasani,dawa hospitalini ni msamiati,mfumuko wa bei umepanda kwa asilimia 16.8%.Mara utasikia maazimisho haya yana fanyika kiwilaya,yakiisha kiwilaya yatakuja kitaifa,hivi taifa hili tunalipeleka wapi?

  Watanzania tuwe macho na tupinge kwa nguvu zetu zote matumizi yasiyo na tija katika taifa letu.Tuna changamoto ngapi zinazotukabili katika nchi yetu?hatuna mashule bora,hatuna waalimu wenye sifa,lakini taifa hili linatumia gharama kubwa kwaajili ya mazimisho haya.Nafikiri ingekuwa ni busara kama tutatathimini matumizi mabaya ya raslimali na pesa za taifa hili kwa kubana matumizi yasiyo na tija.Ingependeza sana kama wananchi hawa wangeshirikishwa katika kutekeleza kazi za umma kwa pamoja ,kuonyesha miaka hamsini baada ya uhuru ni mkakati wa kujikwamua kutoka utumwa mamboleo kwa tabaka la wachache kutumia rasilimali za taifa kujinufaisha binafsi.ili kuwa ni wakati wa wana wa nchi hii kujitolea katika kujenga nguvu zao katika kusafisha miji yetu,kutengeneza barabara zenu kuonyesha ile dhana ya ujamaa na kujitegemea kama ilivyoainishwa katika katiba yetu.

  shime ndugu zangu tupinge matumizi haya kwa vitendo kwa kukata kwenda kujumika na wakubwa hawa wanalipwa posho kwaajili ya kuhudhuria wakati wananchi wa kawida hawana uhakika na mlo mmoja wa siku.Tuseme inatosha kughilibiwa akili na watawala kwa maslahi yao binafsi.Naomba kuwakilsha


  By Sammosses-Mnyonge nyongeni haki yake mpeni
   
Loading...