OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,021
- 114,380
Wakuu JF kama muhimili wa nne usio rasmi wa nchi, kuna haja ya kuja na maazimio na kupitia mtandao huu mamlaka zinazohusika ikiwepo Mh Rais aweze kuchukua hatua. Jambo hili limetuchikulia mda na resources nyingi sana hatuwezi kuacha likapita hivi hivi.
Hivyo ni busara wajumbe wote bila kujali hali na itikadi zenu tukatoa maazimio. Kupitia michango na maoni ya wajumbe ni dhahiri kwamba vita hii inaungwa mkono na sisi sote lakini tunatofautiana na namna ambavyo RC Makonda anavyolishughulikia jambo hili kwa kujimilikisha vita kwa kujibanza ubavuni mwa rais.
Pamoja na mambo mengine mimi naomba nipendekeze yafuatayo. Mods tunaomba mtusaidie kupandisha maazimio yatakayoonekana yana hoja nzito kutoka kwa wajumbe
1. Kwa kuwa imeonekana dhahiri kwamba Mh.Makonda amekiuka utu na haki ya watuhumiwa kwa yeye kama serikali kutuhumu watu katika namna isiyo sahihi.Kwa kuwa Mh.Makonda amekiuka mgawanyo wa majukumu na kuingilia majukumu ya mamlaka zingine. Kwa kuwa Mh.Makonda kwa kutaja majina hadharani kunaweza kufanya watuhumiwa kupoteza ushahidi.
Kwa kuwa Mh.Makonda ametuhumiwa na baadhi ya wajumbe kuwa anatumiwa kupeperusha drug dealers wenyewe hasa ukizingatia kuwa kuna baadhi ya watuhumiwa sana mahusiano naye na hakuwataja,na Kwa kuwa Mh.Makonda amefanya vita hii 'kihuni" kwa kutaja majina isivyo rasmi,kwa kutumia aka na kuorodhesha majina kwenye vijikaratasi.Kwa kuwa approach ya Makonda inaweza kuiletea hasara serikali kwa kulipa faini zitakazoweza kutokana na kesi za watuhumiwa dhidi ya mamlaka za serikali.
Tunaazimia kuwa mamlaka ya uteuzi itengue uteuzi wa Mh.Makonda kuwa RC wa Dar.
2. Kwa kuwa imekuwa ni utamadhuni kwa Wakuu wa wilaya na mikoa kukiuka taratibu na kanuni za umma kwa kupoka madaraka ya wengine, ikiwepo kusimamisha na kuweka watumishi mahabusu. Tinaazimia kuwa mamlaka husika ziandae miongozo na semina elekezo kwa wakuu wa wilaya na mikoa ili waweze kutambua mamlaka zao
3. Mamlaka sahihi na husika ziyafanyie kazi majina yote yaliyotajwa na Makonda na vyanzo vingine na watanzania na hatua kali zichukuliwe dhidi yao
Naomba kuwasilisha