Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

The same old story.

Ninawaasa wananchi masikini kutokuwa mbele kwenye hayo maandamano ili na wao viongozi wapeleke misiba kwenye nyumba zao. Iweje wajiite wapigania ukombozi lakini wanaouwawa na kujeruhiwa ni masikini tu na sio wao viongozi?

Huo ni utahahira wa hao polic ccm kuua raia wasio na hatia.
 
Kweli mmeazimia kuwa "CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano naye ya kiofisi" ?

Tupo watu tunaoangalia mbali:

Ukweli ni kwamba hilo azimio namba 5 (mnaweza kuwa mmechomekewa bila kujua) ebu lisomeni na mlitafakari. JE CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA HATA CCM KINAWEZA KUVUNJA MAWASILIANO YA KIOFISI NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA?

Haya ngoja tusubiri tuone siku za mbeleni nikija hapa na kuuliza tena juu ya taarifa ya utekelezaji juu ya hili azimio!
 
This is absolutely true. Thank you for bringing forth this quote.
Timely justice for all! Hapo kwenye kuisusia TBC mimi nilishaanza tangu aondoke Tido.
Kuhusu Tendwa Ukurasa wa 107 wa Kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu kuna maneno haya "Mabadiliko yana tabia yake. Yakiamua kuja, huja. Huwa hakuna mjadala wala mbadala.Ni mwenye busara tu ndiye huyapokea mabadiliko kwa amani"
Mwandishi anaendelea ..."Nyakati za kukosoa utawala mbovu ukaitwa mchochezi zimepita. Nyakati za kuomba kura kwa wananchi kwa kuwapigia zumari, gitaa au kunengua viuno kwa taarabu zimepita. Nyakati za kumwona mtu mwenye mawazo ya kisiasa tofauti na wewe kuwa ni adui wa nchi au ni hatari kwa usalama wa Taifa zimepita"
 
Ni maamuzi makini, yanayoonesha ukomavu mkubwa na uthabiti wa kisiasa. Heko kamati kuu, mmeonesha kuwa mnaweza kudumisha dira yenu hata katika mazingira ya kutishiwa isiyumbe. Kazeni mwendo, nasi tunawaombea, nchi hii inahitaji wapambanaji hodari, tupo mahali pabaya kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya taifa hili. Ombwe la uongozi nchini ni kubwa kupindukia.
 
Haya ni maamuzi magumu yenye mantiki. Ni lazima tujenge chama chenye uwezo wa kuwajibishana pale mtu anapokosea na sio kulindana kwa kuogopa kuwa atahamia upinzani. CDM tukaze uzi.
 
Chagulani pole sana, cdm Kama usipomramba miguu mbowe na padre slaa Ndio basi tena. Owner wa Chama cdm ni mbowe kwa hiyo hata slaa anamramba miguu mbowe kwa hiyo , chagulani ninakufahamu sana kaka jipe Moyo utashinda. Ni kijana mwenye msimamo wewe una MAWAZO Huru endelea na msimamo huo. Siku za mbowe na puppet wake slaa zinahesabika. Mwenyezi mungu akupe nguvu NYINGI ktk kipindi hike kigumu mi nakuamini TOKA udsm. Nenda cuf, adc au ccm. Angalizo. USiache siasa.
 
Hivi haya matamko ya Chadema huwa yanasaidia nini katika utendaji wa serikali, kama wasipoyafuata CDM mtachukuwa hatua gani.
 
Nawaunga mkono sana, nilazima watanzania na serikali iliopo madarakan tujiandae kwa mabadiliko. Mabadiliko makubwa yanakuja hakuna chama,jeshi, mabomu na mitutu ya bunduki Ak47 havitoweza kuzuwia, watanzania wameamu, na Mungu ameamua, cc BIG OUT. God bles united republic of Tz and people of Tz.
 
Mie naangaliaga TBC alhamisi kwa sababu ya Ze komedi kopi na kupest zaidi ya hapo hata wakiifunga kabisa poa tu.

Mi kwa hapa bongo naangalia star tv, labda na channel ten, mara nyingi naangalia Aljazeera manake wanaijua siasa za tanzania kuliko hata media za hapa!
 
Chagulani pole sana, cdm Kama usipomramba miguu mbowe na padre slaa Ndio basi tena. Owner wa Chama cdm ni mbowe kwa hiyo hata slaa anamramba miguu mbowe kwa hiyo , chagulani ninakufahamu sana kaka jipe Moyo utashinda. Ni kijana mwenye msimamo wewe una MAWAZO Huru endelea na msimamo huo. Siku za mbowe na puppet wake slaa zinahesabika. Mwenyezi mungu akupe nguvu NYINGI ktk kipindi hike kigumu mi nakuamini TOKA udsm. Nenda cuf, adc au ccm. Angalizo. USiache siasa.

kubwa jinga naona post ina harufu ya pombe ya udini pombe hii mbaya sana utajinyea hovyo chunga sana utatia aibu.
 
View attachment 64495


  1. Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi
  2. RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka
  3. Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
  4. chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.
  5. Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.
  6. TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC
  7. Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni,pia kupata habari na taarifa
  8. Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)
  9. Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.


Imesomwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa
Kutoka mjengwablog
Mwnyekiti salam kwako!
hapo namba moja ongeza katibu mkuu wako maana anastahili kuwapo hapo (he is a very weak link!) pia ongeza kiongozi wa operesheni M4C kwani pia anatakiwa ku-predict out come ya mikutano kwa kutumia intelijensia ya CDM.
 
wenye digital receivers (decoder au receiver za dish za kawaida) mni-PM niwaelekeze jinsi ya ku-delete channel maana nilijifunzia wakati nai-delete TBC1 na TBC2 kutoka kwenye Startimes Decoder na receiver ya dish sebuleni kwangu kama miezi 8 iliyopita.

Halafu ukidelete utawaonea wapi Ze Comedy.
 
ukweli kuhusu tbc nikwamba hata huku vijijini inadhalaulika wa2wamesha susia habari zake,inaonesha wanawake tena wachache ndo wanaiunga mkono kwenye vpindi vyake vya bango na cheleko cheleko.kipind mkurugenz wake akiwa tido hapakuwepo vipind vyaajabu ajabu kama vya sasa,shaban kisu na uchaguz majimbon anajua matokeo yake japo kilak2kilikuwa waz akaonwa mbaya.tbc anakula kwenu mazma
 
Nipo Singida tangu jana.Leo,majira ya mchana, katika pita pita zangu mitaani, nilikutana na dogo mmoja maeneo ya Kanisa la Roman Catholic,akiwa amevaa kofia yenye rangi ya bendera ya CHADEMA.Baada ya kumwita,na kuanzisha mazungumzo,nilimuuliza ikiwa yeye ni mwana - CHADEMA ama la.Baada ya kusita kidogo-bila shaka kwa sababu za kiusalama-na baada ya kumweleza kuwa aondoe shaka kwa kuwa nami ni mwana CHADEMA, akakiri kuwa ni kweli yeye ni mwanachama wa CHADEMA na kw

a msisitizo zaidi alitoa kadi yake mfukoni na kunionyesha kwa kujiamini kabisa.Akanieleza kuwa anatoka jimbo la Iramba Magharibi na kuwa huko atokako vijana wamehamasika na wako tayari kwa maabadiliko.Akinieleza''Kaka ,ikiwa wewe ni kiongozi katika chama zungumza na viongozi wenzako ili mje Iramba kufanya mikutano mtuongezee hamasa maana kule kuna mwamko mkubwa na CCM ina wakati mgumu''
Nikiisha kumfahamisha kuwa mimi si kiongozi katika chama na kwamba ni nilikuwa napita tu hapa mjini nilimsihi awe na subira maana M4C ipo karibu na kuwa tungepata jawabu la uhakika baada ya kupata maazimio ya Kamati Kuu.
Sina shaka kuwa dogo mwana-CHADEMA amefurahia sana azimio namba 8.

[/SIZE][/FONT][/COLOR][/QUOTE]

We ulitegemea nini na umeshasema ulimkuta kanisani tena Roman catholic.
 
Hili ni tamko la 70 toka mwaka uanze lakini hakuna hata moja linalofanyiwa kazi na serikali imekuwa kama ngonjera, sasa mtajuaje kama wafuasi wa Chadema hawatazami TBC 1.

Mkuu TBC1 ilikuwa chanzo kikuu cha mitafaruku kwenye sensa? Maana hata shek ponda juzi ali-delete TBC1 so inabidi na ss tumuunge mkono.
 
Chagulani pole sana, cdm Kama usipomramba miguu mbowe na padre slaa Ndio basi tena. Owner wa Chama cdm ni mbowe kwa hiyo hata slaa anamramba miguu mbowe kwa hiyo , chagulani ninakufahamu sana kaka jipe Moyo utashinda. Ni kijana mwenye msimamo wewe una MAWAZO Huru endelea na msimamo huo. Siku za mbowe na puppet wake slaa zinahesabika. Mwenyezi mungu akupe nguvu NYINGI ktk kipindi hike kigumu mi nakuamini TOKA udsm. Nenda cuf, adc au ccm. Angalizo. USiache siasa.

we juha hivi unadhani zile siasa za DARUSO ndio ziwe applicable kwenye ukombozi wa TZ!


Uzuzu wako upeleke mabibo hostel na sio humu ndani kwa makamanda waerevu.
 
Back
Top Bottom