Maazimio ya kamati kuu ya CHADEMA chini ya mwenyekiti Mbowe kesho lazima yatakuwa haya

endelea kupiga ramli,chuki zako hazitokusaidia kitu na teizi utaendelea kuzisikia tu kwa uharo huu
 
Kwa sisi tunaoijua CHADEMA ya sasa na aina ya viongozi wake hasa washauri wa Mwenyekiti na Kamati Kuu yake, na kwa kuzingatia maudhui ya taarifa ya Makene naweza kutabari maazimio ya Kamati Kuu ya kesho kama ifuatavyo:-

CHADEMA itajitoa kwenye uchaguzi huu wa marudio unaokuja.

Mbowe na vijana wake washakubaliana hilo ili kukwepa uwajibikaji kwa matokeo ya Buyungu. Na kwa Kamati Kuu hii hakuna wa kupinga wala wa kumwajibisha ni kulindana mwanzo mwisho. Makene ameanza kutuandaa kisaikolojia kwenye taarifa yake. Isome kwa makini utaona.

Sababu kwa Wanahabari itakuwa

Zile zile za uminywaji wa demokrasia na matumizi ya nguvu za dola.

Ila Sababu halisi na za kweli

1. Hakuna fedha. Chama hakina fedha za kuunganisha Chaguzi mbili za marudio tena kwa majimbo manne na kata zaidi ya 80. Hii ni kutokana na matumizi mabaya ya ruzuku.

2. Chama kimeshindwa kupata wagombea wazuri, imara na wenye nguvu ( Strong Candidates) watakaoweza kushindana. Mfano angali mgombea wa Buyungu wa Chadema na wa CCM. Huko ukonga kapatikana binti mmoja, Korogwe huenda asipatikane kabisa, Monduli sijasikia ila Fred Lowassa nasikia kakataa.

Chadema ya sasa chini Mbowe imepoteza mvuto kwa watu wenye uelewa na kamwe haiwezi kupata watu strong tena. After all watu strong walimwamini Dr Slaa sio Mbowe.

Wakati ni sasa wa viongozi wa chama, Wabunge na Wanachama kufanya mabadiliko ya uongozi. Tunahitaji fikra mpya, mbinu mpya na utendaji mpya unaoendana na nyakati ndani ya Chama. TUUNGANE kwa manufaa ya Taifa na Upinzani nchini.

Benson Mramba
We mpare usiejitambua unajifanya unaijua chadema kuliko chadema yenyewe, kila siku unalia na chadema unalipwa? si uende ccm ukapumzike kwani hakuna vyama vingine, Ni aibu kila siku mwanaume unalia Mara mbowe Mara chadema Fanya kazi ujitafutie kipato siasa chafu hazitokupatia kipato,ulivyo ungekuwa una impact lumumba wangeshafika bei lakini zaidi wamekuona Ni mbea tu na mnafiki. Jitambue kuna mambo mengi ya kuchangia kuhusu taifa sio kila siku unaongelea watu badala ya issues japo ndio SIFA ya wenye upeo mdogo wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom