Maaskofu Tanzania watoa Tamko, wakemea udini, ukanda na ukabila!

lakin bado mm nina maswali mengi kichwan mwangu,
je kwann hadi maaskofu waseme haya?? je ni kwamba hawana imani na hali ya amani iliyopo?? ni kwamba kuna kuonewa ambapo wamekuona ama ni nini?

je hivi kama wakristo wakikaa kimya wasijibu hoja hata moja ingekuwaje ama wasitoe tamko?? na je hivi mungu wa kikristo huitaj mtu kumtetea hadi wakawajibu waislam hoja zao??

Binafsi Askofu wangu Martin Shao hukukaa rohoni. Simbezi ila kwa wanaonielewa watanielewa tu, alichopaswa kusema ni kwamba sasa wakristo tukaze goti tusali Mungu aliye juu ya yote atajidhihirisha kwa wakati wake. tena angesoma habari za yehoshafati wala asingepotez muda kuongea hayo bali angeikabili madhabahu kwa sala za kumwita Mungu aonekane kwa wakati anaotaka.
 
Haya mambo ya udini kuyaongelea mara kwa mara ndio jambo baya zaidi kuliko udini wenyewe.

Hivi mtu unaweza kuendeleza malumbano ya jambo linalokukera!
 
Tunapoelekea hii nchi tutaigawana vipande vipande.

Ni kweli ukimya wa serikali ya CCM katika masuala nyeti na ya usalama wa taifa kumeingiza taifa letu katika hatari ya machafuko! Kuna bomu la uzanzibari na uzanzibara ambalo serikali imelikalia na inalipapasa papasa kama boga! watanganyika wanaoishi zanzibar wanaishi kwa mashaka sana.

Kila mara wanatishiwa kufukuzwa watoke waje huku bara. wananyimwa fursa za kumiliki ardhi na kuwekeza zanzibar. kinyume chake wapemba huku tanganyika wanamiliki ardhi na biashara.

Hakuna anayewabughudhi. serikali sikivu ya Rais kikwete imekaa kimya! Inaogopa suala la muungano kuguswa! watu wasihoji.

KIMYAA! ipo siku bomu hili litalipuka vibaya maana hawa watanganyika a.k.a wazanzibara watachoka na tabia za wazanzibar nao wata-react! kuhusu udini nani asiyejua kwamba umechochewa na kampeni chafu za CCM. ni dude lilotengenezwa katika maabara ya chaguzi na sasa limekuwa giant na liko out of control!

S
erikali sikivu ya Rais Kikwete imeshindwa kuliondoa na matokeo ndo makanisa yanachomwa moto! CCm wanaifanya Tanzania iwe kama Nigeria! very pity....
:bowl:
 
Tunapoelekea hii nchi tutaigawana vipande vipande.

Wala hujakosea Mkuu! CCM ndio mabingwa na manahodha wa hili kwa siasa zao za kuwagawa watu kidini, kikabila, na kikanda ili iweze kuwatawala vizuri. Kama kuna adui namba moja wa taifa hili basi adui huyo sio mwingine bali ni CCM.
 
Mbona hizo takwimu ktk makanisa ya RC sijazisikia? Hapo ndo huwa nawapa big up RC

Hili ni Tamko la maaskofu wote RC, Pentecost na SDA inclusive. Shao amelisema kwa vile ibada ya xmass kitaifa inafanyikia kwenye dayosisi yake. Makanisa mengine watatangaziwa kwenye ibada hii na zingine zijazo.In short ni tamko la wakristo wote na kama ww ni mkrosto basi ni lako pia
 
Men lie, women lie, numbers dont lie....

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • takwimu.png
    takwimu.png
    8.8 KB · Views: 9,678
  • takwimu 2.png
    takwimu 2.png
    13.8 KB · Views: 9,553
  • kodi.png
    kodi.png
    22 KB · Views: 10,021
  • takwimu 3.png
    takwimu 3.png
    5.3 KB · Views: 9,620

Wala hujakosea Mkuu! CCM ndio mabingwa na manahodha wa hili kwa siasa zao za kuwagawa watu kidini, kikabila, na kikanda ili iweze kuwatawala vizuri. Kama kuna adui namba moja wa taifa hili basi adui huyo sio mwingine bali ni CCM.

Kwa hiyo mapadri wote saizi wapo Chadema?

Mbona watuhumiwa wote wa kesi za kuchoma makanisa wameishafikishwa mahakamani.

Maaskofu wanataka serikali iwanyonge hadharani ndiyo wafurahi.
 
Hatua waliochukua sii mbaya... Ila inakuwa kama kurudisha nyumba na kuchochea kuni ambazo zilikuwa zimeanza kupoa. Ni wazi kuwa udini sasa upo; lililobaki ni kutafuta suluhu badala ya kujenga hoja na habari ambazo zinaamsha tena hisia 'hasi' za waumini na wasio waumini kwa makundi makuu husika. Hayo maubiri in a way kuwa "we have the right to get angry" na haijakaa kiusuluhishi. Kitu ambacho ni msingi zaidi...
AshaDii kama vile umewah kusoma biblia.
ngoja nikupe mfano wa kisa cha kweli kwenye biblia, mfalme wa Israel Yehoshefati aliwah kupata waraka toka kwa wafalme ambao ni Moabu, wameuni na amoni walikuja kupigana na Yehoshefati. sasa walikuja wajumbe kumletea ujumbe kwamba wanakuja watu kupigana na wewe. yehoshefati alichofanya alisimama madhabahuni pa bwana na kumwadhimisha Mungu akamsihi Mungu awasikie mabaya yasiwapate na awaokoe na upanga wa adui. basi Mungu toka patakatfu pake alisikia akamwambia nendeni mbele yako msibebe silaha ila muimbe na kusifu mtauona waokovu wangu. basi waliiskia sauti ya Mungu waakenda mbele kwa kuimba na kusifu wale maadui wakapigana wao kwa wao hadi wakauana na kupotea hakuna mwisrael aliyeuwawa ama kauumizwa.

sasa kwa mantiki hii napata hisia kwamba sio kwamba waisam ndio maadui zetu bali kikundi cha wahuni fuan ambacho sasa wakristo walipaswa waende mbele za Mungu kwa sala na kusifu Mungu awaondoe wale adui zetu katikati yetu. ila haya wanayoyasema ni kuita uchochez utaona kesho utaskia waislam wakitoa tamko juu ya hili.
nenda soma 2nyak20:1-19. utaelewa ninachomaanisha
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo mapadri wote saizi wapo Chadema?

Mbona watuhumiwa wote wa kesi za kuchoma makanisa wameishafikishwa mahakamani.

Maaskofu wanataka serikali iwanyonge hadharani ndiyo wafurahi.

sheh ponda ni mtuhumiwa wa kwanza wa kueneza chuki, halafu mnafuatia nyinyi
 
Udini tayari upo wazi hakuna tena kujificha kama viongozi wa dini wameamua kuongea haya basi tena tujiandae na lolote litakalotokea.
Kwani wale akina ponda hawakuwa viongozi wa dini?walianza long time ila hukutaka ona n akusema haya.Naona umekandamizwa kama ulivyosema kwa unyonge kuwa Lema anatumia wanajeshi kuondoa viongozi waliowekwa kisheria.

Mtapiga kelele sana ila "waki NENA watakatifu Watu kusikia na kufurahi". Namuonea Huruma JK na wengine watasemaje hadharani haya ya maaskofu huku wakijua, kuwa kuna wenye version nyingine ya siku nyingi.CCM wameshikwa pabaya tena. Jk alikuwa akikausha kwa vile wana Version nyingine ya sirini inayopita misikitini huku makafiri wakizugwa na ukimya.

Sasa awaeleze wananchi kuhsu MOI au arudishe mali kwa dini husika na kuifuta.Sijui itakueje kwa wasio nazo? Ima sure hili CCM wameshahsikiwa chini vibaya sana, na hii tabia yao ya kuwadnaganya waislam ktk hili halafu kuonge lugha za kuwabembeleza na kukwepa lisemea kwa uwazi ni Tabia ya viongozi wa kizanzibar wanapokuwa zenj wana version yao, wakiwa bara wana version ingine ila net effect ni kuzidi wapumbaza wale watu na baadaye kusababisha hatari ya malimbikizo.
 
Jukwaa la jumiya ya kikristu leo imetoa tamko kuhusiana na mwenendo wa amani nchini, hasa likijikita kuelezea machafuko yaliyoongozwa na kuratibiwa na baadhi ya makundi ya kiislamu nchini.

Moja ya mambo yaliyotolewa ni kukanusha kuwa NCHI hii haiongozwi kwa mfumo kristu, na zaidi imefafanua kuwa:

Rais ni muislamu, Makamu wa rais ni Muislama, Mkuu wa jeshi la Polisi, ni Muislamu, Jaji mkuu ni Muisla, Mkuu wa usalama wa Taifa ni Muislamu,

Na kwa upande wa Zanzibar 100% ya viongozi wa serikali ni waislamu, na sikuwa kule Zanzibar hakuna wakristu wenye sifa za kuwa viongozi!

Akisoma maadhimio hayo kiongozi wa kiroho wa ukanda wa Kilimanjaro Dr Martin Shayo amezidi kusisitiza kuwa Jumuiya ya Kikristu inafikiria kuiomba serikali izirejeshe huduma za kijamii zilizokuwa chini ya makanisa hayo zinazoendeshwa na serikali ili na waislamu nao waweze kuendesha huduma hizo!

Ameiomba serikali kutoyafumbia macho mambo yanayohatarisha umoja wetu,

Tamko Zito sana na lenye afya kwa Taifa.
 
Viongozi wakuu asilimia 90 jmt kuwa waislaam haimaanishi mfumo kristo haupo.hayo ni matokeo wa vyama vya siasa nchini.askofu nivyema ukataza watendaji wakuu na wakurugenzi ndani ya jamhuri ya muungano wa tanzania nani ni wengi ni waislamu ama niwakiristo.

Unapo ongea mambo hayo utasema waislamu wamesoma madrasa wala hawana elimu.its hell.katika baraza la kuundwa katiba mwenyekiti wa tume ya katiba jee ni muislamu?na kama robo tatu ya tume ni waislamu kwa upande wa watanganyika wakiristo ni wengi katika tume hyo kuliko waislamu.

Kwa upande wa zanzibar asilimia 99.9 ni waislamu na uwepo kwao katika tume yakatipa ndo iliyopelelea waislamu wakawa ni wengi mno ndani yatume hyo.kama munataka mambo yakitaifa waislamu wasiwe wengi kwanza vunja muungano.lapili,sera za vyama zieleze wazi mgawanyo wa waislamu na wakiristo kiuongozi ndani ya chama husika.maswali yakujiuliza.

Ni katika kipindi cha nyerere mawaziri na wakurugenzi ndani ya jmt wakiristo na waislamu nani walikuwa wengi?swali hilo hilo jiuleze kwa maraisi wengine waliopita akiwemo ali hassan mwinyi,benjamin mkama na kikwete.hapo aliyekuwa na akili timamu ataelewa na kama hukuelewa huo ndo mfumo kristo wenyewe.

Kama point nikwamba waislamu hawakusoma hiyo asilimia 90 ya viongozi wajuu wa serikali kama ni waislamu swali ni kwamba hao viongozi wamehitimu 2010?naomba facts kama zipo.
 
CHADEMA,Mkuu Ritz utashangaa ukanda na ukabila haujadiliwi hapa kwa kuwa ni mfumo waliorithishwa .

Mkuu Mingoi,
Inasikitisha sana kiongozi wa dini anahoji uwiano wa dini kwenye ofisi za serikali.

Nadhani itasaidia wizara zote ziwe na uwiano wa dini ili twende sawa.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo mapadri wote saizi wapo Chadema?

Mbona watuhumiwa wote wa kesi za kuchoma makanisa wameishafikishwa mahakamani.

Maaskofu wanataka serikali iwanyonge hadharani ndiyo wafurahi.

Mkuu Ritz kheri ya Christmas
 
Last edited by a moderator:
Sioni chochote hapa zaidi ya ubabaishaji! Serikali ipo kimya kwa muda mrefu, kwanini Kanisa lisichukue hatua kwa upande wake kuelezea umuhimu au ubaya wa MoU, au kwanini Kanisa lisisitishe MoU?..kulikuwa na thread nzima hapa kuhusu hili.
Kwa sababu gai wakati serikali ndio iliomba msaada tuta, sasa kama inakwenda ongea kivingine basi wamepewa nafasi ya kuuvunja mkataba. Mkataba ni pende mbili, na kuuvunja ni wote waridhie au mmoja avunje masharti na mwingine kuwa na haki ya kuvunja bila ridhaa ya mingine.

Hatua ya kanisa ya kwanza ndiyo hiyo, kanisa lingekuwa na mamlaka ya kuchukua mali zake wangechukua ila seriklai ndio inanguvu ndio maana walizichukua bila kanisa kufanya kitu.

JK keshwadanganya sana nyie akina sideeq,mmepost junks sana humu ndani, povu na misuli ya shingo iliwatoka hata pale mlipofafanuliwa kwa uelewa wa kawaida kabisa.

Sasa mjiandae lipa hela la Aghakhan au muwe dhehebu lake, mjiandae kukata mkwanja wakutosha au mkasome shule za kabisa kinodnoni muslim.
 
Back
Top Bottom