Maaskofu na watumishi wa Mungu mjitafakari sana kuhusu siasa za nchi yetu!!

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,458
17,282
Wanabodi za asubuhi!
Tangu zamani sana nyakati zile za biblia Mungu aliwafunulia waja wake kuhusu hatma yao ya matukio ya mbeleni kwenye maisha kupitia watumishi wa mungu kama manabii na mitume!!Nakumbuka kisa cha nabii Eliya cha kutabiri kutokunyesha mvua miaka mitatu na nusu kutokana na taifa kumkosea mungu na kukengeuka kwa kumfuata Baali na ibada zake!!maono yalitolewa ili kulionya taifa na kulikemea kutokana na kukengeuka kwao!!

Tangu awamu ya tano iingie madarakani kumekuwa na matamko,nyaraka,Hamaki na Midahalo kinzani kutoka kwa maaskofu mbali mbali kwa madhehebu tofauti tofauti!Wakati wengine wakikemea wengine wameunga mkono na kuwa upande wa serekali!!Sasa sisi waumini tunashindwa kuelewa je Mungu mnae mtumikia ni kigeugeu? Nani anamtumikia mungu wa kweli?Mungu yupi anaebariki mateso ya wananchi kutoka kwa watawala?

Kwa nini watumishi wa Mungu Hamkupata Unabii wa awamu hii taifa likaomba tukapata utawala usiotugawa wananchi? Ni Mungu gani mnaemtumikia ambae ni Bubu asiefunua yajayo? Mbona mmesubiri hadi mambo yameharibika ndio mnatoa matamko na nyaraka?Mlikuwa mnafanya nini kabla ya awamu hii kuingia madarakani?

Ndugu zangu Maaskofu na Watumishi kama Mungu mnae mwabudu hakufunua kabla haya hayajatokea sisi watz tuna mashaka na utumishi wenu!!Ni Mungu kweli mnaemtumikia au Tumbo?

Kwanini Hamkufunuliwa kuwa huyu aliepo ni naamani na atatatutesa watanzania na wenye dhamana wakamwepuka kugombea uongozi?

Nawaombeni watanzania wenye imani na dini zetu tuwaulize hawa makuhani walikuwa wapi na kwa nini hawakuonyeshwa gharika hii inayotutesa watanzania!!!!Kama wana kiroho cha kweli wangesema mapema tena kwa ujasiri kuwa Huyu atamwaga damu za watoto wetu,Atatubebesha mizigo na nira kila siku na tungeamua vinginevyo hata wenye dhamana wange epuka mauaji na vitisho hivi awamu hii!!!
 
Wenye haki ni jasiri kama simba hawataogopa kuwauliza makuhani wao kwa nini haya???Bwana hakusema???Mungu haneni tena???
 
- Wajibu pekee wa viongozi wa dini ni kuhubiri, na kushape maisha ya watu katika imani zao..watu ambao ndio viongozi wa serikali. Madhaifu ya mienendo ya viongozi yanareflect moja kwa moja udhaifu wa mafundisho yanayotolewa.

- Hawatakiwi kujitafakari kuhusu siasa, bali wanatakiwa watafakari kusudi na wito wao kama viongozi wa kiimani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Licha ya kwamba sikubaliani na ulichoandika lakini naomba kuuliza :Ujumbe huu mchungaji Msigwa unamuhusu? Kama ndivyo ,naomba nakala ya Kwanza kàbisa afikishiwe yeye na kama sivyo, tuambie kwa Nini?
 
Wao wanajukumu la kumuuliza mungu juu ya taifa letu na hatma yake!tangu zamani wanaonekana wakifanya hivyo!sio kuhubiri tu!na mafunuo pia!!!
 
Manabii walitabiri. Tb Joshua alikanyaga nchi akiwa mpeku akina Bushiri walitamka wakatukanwa sio hao tu akina kakobe walipiga kelele na kuwa upande wa upinzani mwishowe wakashindwa kabisa kwakuwa wananchi tumerogwa na wanasiasa hatujiwezi kabisa kifikra ni mazezeta. Labda ungeleta mada ya viongozi wa kidini kuwafungua watu fikra zao. Umeyaona ya moshi watu ishirini chali kisa kukanyaga mafuta umeona reaction ya serikali kwa aliyefanya tukio hili ati vibaka walitisha watu kweli?. Manabii wa uongo na viongozi wa serikali wanatumia uchawi mmoja kuwapumbaza watu kupitia maji mafuta na mchanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi na Kanisa la Mungu linapita katika kipindi kigumu na majaribu.

Wakatoliki, mnafahamu juu ya ujumbe wa Fatima. Katika siri tatu alizopewa Lucia mwaka 1907 (yawezekana nikawa nimekosea mwaka lakini najua ni kabla ya 1910), mojawapo ilikuwa ni kuanguka kwa ukomunisti (limetimia), ya pili ni kuwa kuanzia mwaka 1980, Shetani atatenda kazi zaidi kwa kupitia viongozi wa dini. Watu wengi watapotea kwa kufuata maelekezo/mafundisho ya viongozi wa Kanisa. Waumini, kwa kufuata mafundisho ya viongozi hao wa dini walio mawakala wa shetani, wataanguka kwa kudhania wanafuata mafundisho ya Mungu, kumbe ni mafundisho ya shetani.

Kwa hiyo ndugu zangu katika Kanisa la Mungu, kuna mawakala wa shetani, katika uongozi wa Kanisa. Tena ujumbe ule unaongeza kunena, shetani atajitahidi sana, hata kutaka kukalia mpaka kiti cha juu kabisa katika Kanisa.

Kwa hiyo tusiwategemee sana viongozi wa Kanisa, maana hata wao, miongoni mwao kuna mawakala wa shetani. Tuombe hekima ya Mungu ya kuwatambua wakala wa shetani ndani ya uongozi wa Kanisa.

Viongozi wa Kanisa mawakala wa shetani, aghalabu watajishikamanisha na watawala ili wafaidi anasa za watawala. Lakini watumishi wa Mungu wa kweli, daima watasimama na wanaodhulumiwa. Kristo ni mdhulumiwa aliyetutangulia, Yeye atashikamana na wanaodhulumiwa ili awape tumaini kuwa dhuluma yao ni ya kupita, lakini ushindi wao ni wa daima. Lakini ushindi wao hauji kama mana bali kwa kujitoa, kwa mateso na hata kifo maana yeye aliye kuhani na nabii alijitoa, aliteswa, alikufa, akafufuka na ushindi wa kudumu.
 
Wanabodi za asubuhi!
Tangu zamani sana nyakati zile za biblia Mungu aliwafunulia waja wake kuhusu hatma yao ya matukio ya mbeleni kwenye maisha kupitia watumishi wa mungu kama manabii na mitume!!Nakumbuka kisa cha nabii Eliya cha kutabiri kutokunyesha mvua miaka mitatu na nusu kutokana na taifa kumkosea mungu na kukengeuka kwa kumfuata Baali na ibada zake!!maono yalitolewa ili kulionya taifa na kulikemea kutokana na kukengeuka kwao!!

Tangu awamu ya tano iingie madarakani kumekuwa na matamko,nyaraka,Hamaki na Midahalo kinzani kutoka kwa maaskofu mbali mbali kwa madhehebu tofauti tofauti!Wakati wengine wakikemea wengine wameunga mkono na kuwa upande wa serekali!!Sasa sisi waumini tunashindwa kuelewa je Mungu mnae mtumikia ni kigeugeu? Nani anamtumikia mungu wa kweli?Mungu yupi anaebariki mateso ya wananchi kutoka kwa watawala?

Kwa nini watumishi wa Mungu Hamkupata Unabii wa awamu hii taifa likaomba tukapata utawala usiotugawa wananchi? Ni Mungu gani mnaemtumikia ambae ni Bubu asiefunua yajayo? Mbona mmesubiri hadi mambo yameharibika ndio mnatoa matamko na nyaraka?Mlikuwa mnafanya nini kabla ya awamu hii kuingia madarakani?

Ndugu zangu Maaskofu na Watumishi kama Mungu mnae mwabudu hakufunua kabla haya hayajatokea sisi watz tuna mashaka na utumishi wenu!!Ni Mungu kweli mnaemtumikia au Tumbo?

Kwanini Hamkufunuliwa kuwa huyu aliepo ni naamani na atatatutesa watanzania na wenye dhamana wakamwepuka kugombea uongozi?

Nawaombeni watanzania wenye imani na dini zetu tuwaulize hawa makuhani walikuwa wapi na kwa nini hawakuonyeshwa gharika hii inayotutesa watanzania!!!!Kama wana kiroho cha kweli wangesema mapema tena kwa ujasiri kuwa Huyu atamwaga damu za watoto wetu,Atatubebesha mizigo na nira kila siku na tungeamua vinginevyo hata wenye dhamana wange epuka mauaji na vitisho hivi awamu hii!!!
'There are not united' kila mtu anaongea kivyake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona wajiitao wachunga kondoo wako upande wa tawala dhalimu upande Wa wanaowanyima watu haki ya kuishi uhitaji kujua wanamtumikia Mungu yupi
 
Nchi na Kanisa la Mungu linapita katika kipindi kigumu na majaribu.

Wakatoliki, mnafahamu juu ya ujumbe wa Fatima. Katika siri tatu alizopewa Lucia mwaka 1907 (yawezekana nikawa nimekosea mwaka lakini najua ni kabla ya 1910), mojawapo ilikuwa ni kuanguka kwa ukomunisti (limetimia), ya pili ni kuwa kuanzia mwaka 1980, Shetani atatenda kazi zaidi kwa kupitia viongozi wa dini. Watu wengi watapotea kwa kufuata maelekezo/mafundisho ya viongozi wa Kanisa. Waumini, kwa kufuata mafundisho ya viongozi hao wa dini walio mawakala wa shetani, wataanguka kwa kudhania wanafuata mafundisho ya Mungu, kumbe ni mafundisho ya shetani.

Kwa hiyo ndugu zangu katika Kanisa la Mungu, kuna mawakala wa shetani, katika uongozi wa Kanisa. Tena ujumbe ule unaongeza kunena, shetani atajitahidi sana, hata kutaka kukalia mpaka kiti cha juu kabisa katika Kanisa.

Kwa hiyo tusiwategemee sana viongozi wa Kanisa, maana hata wao, miongoni mwao kuna mawakala wa shetani. Tuombe hekima ya Mungu ya kuwatambua wakala wa shetani ndani ya uongozi wa Kanisa.

Viongozi wa Kanisa mawakala wa shetani, aghalabu watajishikamanisha na watawala ili wafaidi anasa za watawala. Lakini watumishi wa Mungu wa kweli, daima watasimama na wanaodhulumiwa. Kristo ni mdhulumiwa aliyetutangulia, Yeye atashikamana na wanaodhulumiwa ili awape tumaini kuwa dhuluma yao ni ya kupita, lakini ushindi wao ni wa daima. Lakini ushindi wao hauji kama mana bali kwa kujitoa, kwa mateso na hata kifo maana yeye aliye kuhani na nabii alijitoa, aliteswa, alikufa, akafufuka na ushindi wa kudumu.

Paragraph yako ya mwisho ni ukweli usiopingika. Ubarikiwe Mtumishi wa Bwana Yesu wa Nazareth.
 
Back
Top Bottom