Maaskofu na madawa ya kulevya, Pinda ahojiwa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu na madawa ya kulevya, Pinda ahojiwa bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Aug 11, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Suzan Lymo ktk kipindi maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu bungeni alimhoji waziri mkuu Pinda kwamba, Ni lini viongozi wa dini wanaohusika na madawa ya kulevya ambao Rais alisema ana taaarifa zao watapelekwa Mahakamani?

  Suzan alisema ni matumaini yangu kuwa na wewe unawajua wauza madawa ambao ni viogozi wa dini na kama hujui Rais wako ameshasema anataarifa zao.

  Suzan Lymo pia alieleza kuwa madawa ya kulevya yamerudisha sana nyuma heshima ya nchi yetu Duniani.

  MAJIBU YA PINDA

  Pinda alipata wakati mgumu sana na hakujibu swali la Msingi. Alitumia muda mwingi sana kutetea kuwa Tanzania inaheshimika duniani na si kweli kwamba heshima yetu imeshuka. Alijitetea kuwa akiwa nje ya nchi anakutana na watu ambao wanasifia sana Tanzania hasa kutokana na Amani yetu.

  Kuhusu ni lini viogozi wa dini watapelekwa mahakamani alisema
  Kwani kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya imeacha kazi yake? Vita hii ni endelevu na haina mwisho idara husika zinaendelea na vita hii dhidi ya mdawa ya kulevya.

  Rais hakumaanisha kuwa ni viongozi wote, bali alimaanisha baadhi ya viogozi wa dini - si wote. Akagusia kwa mbali kuwa hasa viongozi wa madhehebu madogo madogo.

  My take, Waziri mkuu hakujibu kabisa swali la msingi la muda wa kuwashtaki.
  Pili hakukuna wala kukiri kuwa JK ana majina ya viongozi wa dini wanaouza madawa ya kulevya. Zaidi sana alimtetea kuwa Rais alikuwa na ni njema.

  Nawasilisha.

   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,677
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Kama kuna kitengo cha madawa ya kulevya,kwa kweli sioni haja ya waziri mkuu kujua tarehe ya kuwapeleka mahakamani.
  kitengo......prosecutor.....mahakama.
   
 3. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kobelo,
  Rais wa nchi, Amiri jeshi mkuu wa Majeshi, kioo cha nchi amesema ana majina ya wauza madawa ya kulevya. Kwanini asiwapeke mahakamani kupitia vyombo husika?

  Kama vitengo vinavyohusika na madawa ya kulevya vipo na havijaweza kupata ushahidi huo ambao Rais anao, kwanini asiwasaidie.
  Rais kama kioo cha nchi anapokaa na majina ya wahalifu wa makosa ya jinai inaleta picha gani kwetu Taifa?

  Je, unataka kuwaaminisha watanzania kuwa Rais wetu anajiongelea tu bila kujua kuwa iko siku atalzimishwa kuwataja hadharani kama ilivyotokea leo bungeni?

  Je, huoni kuwa jambo hili linadhalilisha sana ofisi ya Rais?
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  mnamtegemea rais????HOSEA alisemaje???rais anamzuia,hata nzowa atakuja ropoka
   
 5. N

  Nipe tano Senior Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magwanda wenzenu wameshasema MASWALI yalipangwa... Hili nalo lilipangwa kumbe Suzan Lyimo kibaraka????? Magwanda vilaza KWELI ......
   
 6. MANI

  MANI Platinum Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo watu hawawezi kupambanua udhaifu wa kujinadi una majina ya wahalifu na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa !
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu una uhakika na hapo kwenye red, kabla sijachangia!!
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Mkuu,
  CCM ndo wanapangana majibu labda, mimi sina hakika. Ila jambo moja nina uhakika nalo. CCM hawawezi kuwapangia Chadema maswali ya kuwauliza.
  Pili, kama ulitazama Kipindi cha maswali kwa waziri mkuu. Pinda alipata tabu sana na kusita sana kujua namna ya kuanza kulijibu. He was shocked and totally confused. Akatumia muda mwingi kueleza asichoulizwa ili apate muda wa kutafuta majibu kichwani.
  On other hand, alipoulizwa swali la madiwani wa chadema na mbunge wa CCM. Alijieleza vizuri sana mambo makubwa bila kubabaika, utadhani anasoma majibu.
   
 9. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hiv naomba kuuliza tunaposema viongoz wa din tunamaanisha wakristo tu yaani maaskofu na wachungaji tu? Kama mwazilishi wa thread alivyosema au nipamoja na mashehe? Mbona karib waarab na wahind waliopo bongo ni waislam na ndo wanafanya biashara haramu pamoja na madawa ya kulevya. Naomba kueleweshwa.
   
 10. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...kama sio juhudi zakoMkweere na mgawo ungetoka wapiiiiii?

  ...kama sio juhudi zako Mkweere na mafuta yangekwisha liniiii?

  ...kama sio michongo yako Mkweere na kina shimbo wangekua wapiiiiii?

  ...kama sio usanii wako Mkweere Ufisadi na gutter politicians wangekuwa wapiiiii?

  ...kama sio ulegelege wako Mkweere foleni kwenye petrol station zingetoka wapiiiii?

  ...kama sio usanii wako Mkweere na umaskini ungezidi vipiiiii?

  ...kama sio ujanja wako Mkweere shilingi ingeporomoka vipiiiiiiii?

  ...kama sio bora liende Mkweere serikali ingeyumbishwa vipiiiiiii?

  ...kama sio ushikaji wako Mkweere uchumi wetu ungeporomoka vipiiiii?

  ...kama sio kutokujali kwako Mkweere vidumu na magaloni mtaani vingetoka wapiiiiii?
   
 11. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Hujui hizi ni juhudi za makusudi za ****** kuwapaka wakristo matope na kujustify ule mnongono kuwa hawezi kuwaachia nchi makafri. Kama anawafahamu kwa nini tusiwaone mahakamani. Hakuna haja ya kucheka na wahalifu hata kama ni maaskofu or mashehe.Wewe humfahamu jamaa kwa kupika fitina.
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kuwa mwarabu au mhindi haimaanishi kuwa ni mashehe. shehe ni mwana taaluma bila kujali rangi yake. kuna waarabu wakirsto pia. Au wewe ndo wali wakiwaona wazungu tu unajua kuwa huyu ni askosfu au padre? simply hapa ameongelea viongozi wa dini kama vioo mitaani na si waumini wao.
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kikwete si mkapa. mkapa hana simile. aliwashika mashehe hata wakiwa misikitini wakiswali na kubabikizia kesi eti ni wa chochezi. akina ponda walisakwa kila kona ya nchi kuwa ni wa chochezi. leo hii akina ponda wapo na hatuuoni huo uchochezi wao.

  Kikwete si mtu wa kuwadhalilisha watu. hebu imagine akiwashika leo viongozi wa kanisa, kanisa zima linapata kashfa na fedheha. si kwa Tz tu bali duniani kote. Au huoni ile ishu ya mashoga ilivyolidhalilisha kanisa? huoni wale waliobaka watoto walivyolidhalilisha kanisa mpaka na papa akaomba radhi hadharani?

  I think JK alifanya vizuri. just kuwataadharisha. pia akizingatia heshima yao kwenye jamii.
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu tatizo ninaloliona hapa ni JK kupenda kusema kila kitu, na hicho ndo kinachomcost mshikaji. Si kweli kwamba Mkapa alikuwa hajui na hajui majina ya wauza unga. Na mwinyi naye pia.

  Ila kwa nyerere sina uhakika kwa kwani kwa msimamowa mchonga sina comment. Ila wenzio waliomtangulia hawakutaka kusema kila kitu, vingi vilibaki vifuani vyao lakini si kwamba walikuwa hawajui. Tatizo la JK ninaloliona ni kidomodomo.

  Na haya ndo madhara yake. wanaofaya hii biashara haramu nahisi wengi wako kwenye system wamemzunguka, si kwa yeye tu na watangulizi wake.
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Mimi ninavyofahamu ni kwamba shutuma hizi za kuwafahamu viongozi wa dini wauza unga zilitolewa kwenye sherehe ya maaskofu wa kikatoliki. Maana yake ni nini? Na ni kwa nini isitolewe kwa viongozi wa dini za protestant ama waislamu?

  Nafikiri rais wetu hakurupuki, ukizingatia ana vyombo makini vya kiintelejensia vinavyompa habari sahihi. Hivyo viongozi hao watakuwa ni maaskofu wa katoliki, ndio maana aliwapasha wao. Hawawezi kuwa maaskofu au wachungaji wa kiprotestant/kipentekoste ama waislamu, maana kauli haijatolewa kwao.

  Sasa hivi mitaani tunajua kuwa viongozi wa kanisa katoliki wote ni wauza unga kwa mujibu wa kauli ya rais wetu kipenzi. Labda tunaweza badilishwa mawazo yetu kwamba sii maaskofu wote wa katoliki kama rais atapenda kuwataja miongoni mwao wahusika na kuwashitaki.
  Hapo tu ndipo anaweza kuturudishia imani yetu kwa maaskofu wa katoliki ambao hawatakuwa kwenye hiyo listi ya mh rais.
  .
   
 16. Fighter

  Fighter JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ehehehe!!!!!!!!alafu du maskofu na madawa du wasifanye nasi waumini tukawa mateja!
   
 17. k

  kikono Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini tuache maskhara. Hivi mlisikia wapi rais anasema anawafahanu wanaofanya biadhars ya madawa na polisi usalama wa Taifaa wapo??? Hivi hii ni kazi yake?? Mbaya zaidi hawashughulikiwi.

  Na kama ni wa vikanisa vidsogo why alienda kuyazungumzia kwenye kuwekwa wakfu kwa Askofu wa Lindi tena wa lanisa kubwa lenye sifa duniani la RC? Huku ni kudhalilisha ukristo. Malipo hapa hapa.
   
 18. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Thanks for this useful comment! Thank you.
   
 19. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Japo sikuangalia kipindi cha maswali ya papo kwa papo, hakika Susan Lyimo atakuwa ameuliza swali la msingi sana, na ni swali lililokwenda shule, ndiyo maana MP alibabaika katika kulijibu. Naungana kabisa na hoja ya Michael P. Aweda. Waziri mkuu amekwepa swali, ngoja tuone kama ataulizwa tena siku nyingine atajibu nini.
   
 20. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mbona
  wanavaa misalaba mikuuubwa
  shingoni kumbe ni minyororo
  ya yule mwovu! Na jirani zao
  kiimani, wanvaa majoho
  mareeefu na hijab kwa ajili ya
  kuficha/kufunikia dhambi/
  bhangi.
  "Mwamini Bwana Yesu nawe
  utaokoka." (Mdo. 16:31)
   
Loading...