Maaskofu na CCT toeni boriti kwenye macho yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu na CCT toeni boriti kwenye macho yenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Xuma, Jun 8, 2011.

 1. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Na Yona F Maro (from wanabidii)
  Jun 7, 6:01 pm

  Kumekuwa na mijadala kwenye mitandao hii juu ya Mhe Raisi kutuhumu

  baadhi ya viongozi wa dini kujihusisha na biashara za madawa ya
  kulevya na baadaye viongozi hao kwa kutumia taasisi yao ya CCT kutoa
  tamko kumtaka Raisi atoe orodha ya majina hayo ndani ya Masaa 48 .

  Mimi binafsi sikushangazwa na Tamko hili la maaskofu wala lile la

  Ikulu ambalo lilitoa majibu kwa hilo la Jumuiya yao yaani CCT .

  Lakini la msingi ni kwa maaskofu wenyewe kupitia viongozi wao wengine

  wa makanisa wa madhehebu kadhaa ambao huko nyuma wamewahi kuwa katika
  tuhuma kadhaa ambazo sio nzuri mbele ya jamii ambazo hawajawahi
  kuzitolea maelezo wala majibu kama walivyofanya kwa hili la Madawa ya
  Kulevya .

  Maaskofu na viongozi wengine wa dini wamekuwa wakihusishwa na vitendo

  vya aibu kama kutembea na wake za watu , kunyanyasa wanafunzi kijinsia
  haswa kwenye shule za seminari , kashfa za mapenzi kwenye vyuo vikuu
  vinavyomilikiwa na taasisi hizi na maovu mengine mengi haya yote CCT
  haijawahi kutoa tamko kukana wala kuomba orodha ya majina ya
  watuhumiwa .

  Ukiacha hiyo ya unyanyasaji viongozi Hawa kupitia ndugu zao au watu

  wao wa karibu wamekuwa wakitumia vyeo vyao kupitisha mali kwenye
  bandali yetu na viwanja vya ndege kwa kutumia majina ya makanisa na
  taasisi zingine za dini kwa sababu ya mapunguzo ya kodi .

  Wakati wao wanampa Raisi masaa 48 kujibu tuhuma hizo nami nawaambia

  watoe boriti kwenye macho yao waangalie mbali zaidi na kujua sisi
  watanzania hatupendi kuona mjadala wao na raisi kwanza hautufurahisi
  kiroho wala kiimani tunataka kuona viongozi hawa wa dini wanawajibika
  wao wenyewe na taasisi zao katika kulea watanzania na kuwawezesha
  kuendelea na maisha yao kwa amani kutokana na mafunzo na vitendo vyao
  mbele ya jamii .
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Unachosema ni kweli kabisa mkuu, kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa viongozi wote wa kidini.Si wakristo wala waislamu wote wamekuwa hovyo tu.Ndo maana hata rais amewadharau kiasi cha kuwatolea tuhuma nzito.

  Anajua kuwa wengi wako kibiashara zaidi kuliko kutoa neno la Mungu.Rais anajua kuwa kama wameweza kuwapa hela viongozi wa dini ili waweze kutoa matamko ya kushambulia dini nyingine na vyama vya upinzani watashindwa nini kufanya biashara haramu ili watajirike?
   
 3. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeipenda hiyo statement.

   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Viongozi wa dini mjifunze kutokana na tukio hili, msipende kuwakaribisha watawala kwenye shughuli zenu za kiroho matokeo yake mmevunjiwa protocal mbele ya kondoo wa bwana.Imefikia pahala viongozi wana-impair independence yao katika kuikemea serikali kulingana na maovu inayowafanyia wananchi.

  Angalia mmeshindwa hata kukemea tukio la kihistoria la Nyamongo Tarime, maiti ya kondoo wa bwana zimedhalilishwa kiasi kile, mauaji ya kikatili kiasi kile bado mmeendelea kukaa kimya. Inauma sana waheshimiwa wetu, mimi ni mkristu lakini nilikuwa nimekosa pa kusemea maana nisingeeleweka lakini Rais JK kanifungulia njia. Badala yake JK amekuwa na independence ya kuwasema hadharani kwani anajua fika ninyi ndiyo mnajipendekeza kwake.

  Viongozi wa makanisa lazima mjirekebishe kwa kufanya mambo yenu kitaasisi zaidi bila kujipendekeza serikalini, kwani serikali inapofanya mambo yake kama uzinduzi wa barabara, majengo, semina elekezi na mengine huwa mnaalikwa? Jibu ni hapana.

  Jengeni independence ili muwe na nguvu wakati wa kuandika hata nyaraka zenu kuionya serikali, lakini kwa utamaduni unaojengeka kwa sasa mnakaribia sana siasa na matokeo yake mnadiriki hata kuwaambia watanzania kuwa huyu ni CHAGUO LA MUNGU na hivyo ku-influence maamuzi ya wapiga kura wakati ule.

  Kichaa mmemukabidhi rungu weenyewe sasa anawarudi.

  GO JK GO
   
 5. t

  tufikiri Senior Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi ndio thread ambazo tunazitaka humu. zisizo na ushabiki wa upande wowote. Thread km hizi hazichangiwi kwa kuwa sio za kishabiki. Most of people here are no longer Great thinkers.
   
 6. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Haaah haaahaah MAASKOFU NA CHAGUO LA MUNGU. Kaaaz kweli kweli!!!
   
 7. B

  Biro JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 331
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Mi inanitia kichefuchefu kusikia viongozi wa dini wanashiriki biashara hiyo haramu lakini, kama kuna kiongozi wa dini amejihusisha na madawa ya kulevya si akamatwe na atiwe ndani? Unamwacha ni sababu kiongozi wa dini au?

  Sidhani, wanaogopwa kama wanavyoogopwa mafisadi kwa sababu viongozi wa serikali wenyewe huenda wamo, akichangia majibu ya ikulu kwa maaskofu nzowa alisema wanaofanya biashara hiyo wamo viongozi wa serikali ila uchunguzi bado unaendelea, sasa maboriti yapo kila mahala. tunazugana tu.
   
 8. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Wewe hatutaki umbea wala kujitafutia sifa. Maneno yako unayoyasema inamaana unauhakika na unachokisema kama sio umbea. Tunaomba utupe kazi za mahakama na dola mara mhalifu anapotenda kosa au wao wanakwenda kuwapikia pilau wakakuletea wewe uje utulete umbea hapa.

  Hatutaki unafiki wa kumumunya. Tunajua yaliyotokea wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria sasa wewe unatuletea mambo ya umbea sijui seminari je walikufanyia wewe, tuambie kama walikulamba.

  Mnajua hapa hamjengi ila mnaendelea kujenga chuki kati ya maaskofu na serikali. Hapo kwenye red nitakuomba umpelekee RIZ1 atakupa ufafanuzi na majibu.

  ACHENI KUMCHONGANISHA RAIS NA JAMII. BADO KIDOGO TUTAANZA MAMBO YA BUNGA BUNGA.
   
 9. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono 100% mtoa thread hii. Viongozi wa dini za aina yeyote ile wangetumia muda huu kuisaidia serikali katika kusafisha maovu katika taifa hili - kuna muda utafika hata sehemu ya heshima wanayoipata itatoweka.

  Badala ya kukalia kuisema serikali na kumpa mkuu wa nchi ultimatum ya masaa 48 waelewe nao upande wao unadorora/umeanza kudorora. GOD IS FOR US ALL.
   
 10. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  hii post nimeipenda, kama viongozi wa dini mumo humu ombeni orodha ya hayo yaliyotajwa hapo juu na mtoa mada.

  Ni aibu kubwa kwa Mokiwa kutoa lile tamko, kama angelipotezea asinge wasaliti maaskofu wanaojihusisha na dili hizo.

  Imenisikitisha hiyo ya kusema wanatembea na wake za watu? Hii mbaya sana, unajua kiuharisia ni kwamba Mungu aliyetuumba sisi binadamu hakuna aliposema kuwa kiongozi wa dini asioe, sasa binadamu anapojitungia sheria tofauti na maumbile lazima ataumbuka tu.
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  viongozi wa dini kwa kutokufanya kazi zao maadili yamepolomoka kwa kiwango kikubwa mno, sasa hivi wanawake wanatembea uchi barabarani hadi kwenye nyumba za ibada wala hawaoni hata haya. Baadhi ya viongozi wa dini wanaojihusisha na tabia chafu hupenda kuona ****** ya wanawake ndio maana hawakemeni hata kidogo. Mimi siamini eti kiongozi wa kiroho(padre) Mtalimbo uko poa unafunction eti asiwe na matamani kwa kuona ****** ya muumini wake aliyepita mbele yake? haiwezekani yeye alizike kupiga kuny...to mpaka kufa kwake.Tunaomba viongozi wa kiroho ambao si wachafu walisimamie hili kwa nguvu zote kwani watawajibishwa mbele ya Mungu kwa kutokemea
   
 12. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nachukizwa sana na general sentence zinazotolewa na kuonyesha kuwepo kwa jambo kubwa na baya lakini bila kuwepo kwa maelezo ya ziada ya ku-specify nini hasa kinaongelewa na kwa mifano valied au kutoa udhibitisho!! kama jambo ni baya kwa nini husitaje hata huyo aliyelifanya?? Hii imekuwa ni tabia mbaya, mfano utasikiwa ...wapo watu wanahubilri/wanatugawa kwa kuleta udini (haielezwi ni akina nani na kwa jinsi gani) sasa inakuja kusema wapo watumishi wanafanya biashara za dawa za kulevya ....again no detail!! Hii inafanya watu wanaishi kwa speculations na hofu za bure!!
  Mfano mwingine ni hapo juu maandishi mekundu...mwadishi anataka kuonyesha kuwepo kwa mambo makubwa maovu na kwa kiwango cha kutisha sana bila specific details. Binafsi naona watu wa jinsi hii ni hatari, wazushi, wenye hila na wenye sumu kali kuliko ya kobra!!
   
 13. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  chonde chonde mkuu!

  Hii article nimekutana nayo kule wanabidii google group nikaona inafaa kuja kujadiliwa hapa JF kwa hiyo toa maoni yako usinishambulie mimi mtanzania wa kawaida!!!!!!!!!
   
 14. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Safi sana wana JF
  Bado kidogo muwe huru zaidi.

  Naomba niongezee kwamba, wanaotakiwa kuchukua hatua zaidi,
  kama alivyoanza mwenzao Jakaya, ni waumini wote wa dini hizi,
  kujiuliza, watu hawa, na uovu woooote huu, na uongo wooote huu
  "Jakaya Chaguo la Mungu etc", Hawa wanaleseni ya kuwa watumishi
  wa Mungu hawa?.

  Kwa mfano, na tofauti zoooote hizi baina ya vyombo wanavyoviongoza,
  inawezekana kwamba woooote hawa wanamtumikia Mungu Mmoja?

  Fikiria
   
Loading...