Maaskofu: Mungu amejibu maombi, wampongeza rais Magufuli

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,844
BARAZA Kuu la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) limetoa tamko la kumpongeza Rais, Dk John Magufuli kutokana na kupigania rasilimali za nchi ambazo ziliumbwa na Mungu.

“Kama Maaskofu tukasema tusikae kimya lazima tuseme kitu kwa ajili ya shujaa na jemedari huyo anayesemea Watanzania. Mungu ametupatia mtu wa muhimu sana,” lilisema sehemu ya tamko hilo.

Katika tamko lao lililosomwa juzi na Askofu Peter Konki mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige, limesema hakika Tanzania imepata kiongozi kutokana na maombi mazito yaliyofanywa na viongozi wa dini na waumini na sasa rasilimali za nchi zinakwenda kukombolewa ili ziwanufaishe Watanzania wote.

Akisoma, Askofu Konki alisema baraza lilipokaa liliona si busara kukaa kimya kutokana na kuwa na tukio kubwa hapa nchini na kuamua kutoa tamko la kumpongeza Rais Magufuli juu ya uponyaji wa maliasili za nchi ambazo zimeumbwa na Mungu.

“Rais Magufuli kwa muda mfupi aliokaa madarakani amefanya mambo mengi, Rais ni mvumilivu na anajua cha kufanya ameleta mageuzi makubwa nchini amewaona wenye vyeti feki na watumishi hewa na kuwaondoa kwenye utumishi wa umma,” alisema.

Pia alisema katika suala la madini, Rais amefanya kazi kubwa na kugundua rasilimali ya nchi ilivyokuwa ikitoroshwa huku ikiwaacha Watanzania wakiwa masikini. Alisema Rais Magufuli ni kiongozi shujaa ambaye anatakiwa kupongezwa kutokana na kazi kubwa anayofanya.

“Serikali ijue Wapentekoste wana dhamira na serikali na wako nyuma ya Serikali, tunajua Rais anajeruhiwa na maneno mengi Sisi CPCT siku zote tunaunga mkono Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tunaona juhudi katika utendaji kazi,” alisema.

Askofu Konki alisema katika kikao cha kawaida walichokaa Mjini Dodoma walijadili juhudi za Serikali na wamejionea jinsi serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imejitanabaisha katika kupambanua na matendo ya kifisadi na hayo ni majibu ya kanisa kutoka kwa Mungu.

“Uongozi uliotukuka, hali ya utukufu na amani ni zawadi kutoka kwa Mungu na tunamrudishia sifa na shukrani kwa kutuonesha ni kwa namna gani madini yetu yalikuwa yakiporwa,” alisema.

Alisema kama maaskofu wanamuahidi Rais Magufuli kuendelea kumuombea na kumuunga mkono kama jemedari wa taifa na aendelee na kazi ya kunyoosha nchi kwani ameweza kudhibiti matumizi ya serikali na kuongeza juhudi katika ukusanyaji kodi.

Alisema kama kanisa wataendelea kumuombea Rais Magufuli, Mungu ampe afya njema, hekima na busara wakati anatekeleza majukumu yake. “Tunawaombea na viongozi wa nchi Mungu awape hekima, busara na uaminifu bila kuathiriwa na matamanio ya muda mfupi yatokanayo na maslahi ya kisiasa,” alisema.

Naye Mwigulu Nchemba alisema uchaguzi wa mwaka 2015 ni uchaguzi ulioombewa sana na walikuwa wakiomba Mungu awape Rais mwenye roho ya pekee na kazi alizofanya zimekuwa na utukufu.

“Kwenye uchaguzi uliopita kama si maombi nchi hii ingebadilika lakini wacha Mungu kwa maombi yao uchaguzi ukapita salama. Mungu alisikia mambo na akajibu sawa sawa na mapenzi yake tuendelee kumuombea Rais Magufuli afanye kazi yake ili sifa na utukufu vimrudie Mungu,” alisema.

Alisema kama kiongozi anaiona nia njema aliyonayo Rais kwa Watanzania. “Tumuombee Rais wengine wanasema mbona Rais anakuwa mkali ni lini uovu ukaondoka kwa upole, mnatambua mapepo yapo halafu unasema shetani toka basi, huwezi kubembeleza pepo hata siku moja,” alisema.

Alisema hata Yesu kwa mambo ya kibinadamu alipoona pepo akasema kwa ukali shetani toka. Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige alisema alisema tamko la kumpongeza Rais ni zuri kwani anastahili kupongezwa kutokana na kazi kubwa anayofanya.

“Ufisadi uliogundulika ni kiasi kidogo sana lazima tuambiwe vile vitofali vya dhahabu vilizalishwa vingapi na vina thamani gani hapa tunazungumzia mchanga tufike na kule kwenye vitofali,” alisema.

Chanzo: Habari leo
 
Katika maisha binadamu kaumbiwa changamoto nyingi kumfikishia malengo yake,

Kwa sasa naona Magufuli anapitia changamoto nyingi, hili ni pamoja na wananchi wake wenyew kutwa kumpigia kelele, lakini ukweli utajulikana baadae,

Wengi wa wananchi wanaopiga kelele ni wale wasioweza kufanya lolote zaidi ya kulaumu, mi nawaita "Losers" kuna makosa yalifanyika katika utawala zilizopita lakini, tujiulize jitihada gani zinafanyika sasa kuyarekebisha, wengi wetu tunalamikia vitu vilivyopo kweny hisia lakin tunashindwa kuangalia ukweli wa mambo,

Swala la ACACIA lilitakiwa kuangaliwa upya kutokana na mikataba chakavu iliyokuwepo, lakini watu hao hao, Leo ii wanalalamika kuona serikali inakurupuka, na kingine wanaweka vikwazo, muheshimiwa asishinde, lakin ivo ni vikwazo tu vya watu wasioweza kufanya chochote,
...sikuzote lawama haiui,ila fedhea, kwa iyo Magufuli kazi kazi, ii nchi ilikua imekwisha,.. Watu wanaitafuna wanavotaka, sasa wamekosa pa kushika, kazi kuweka vikwazo ili uonekane mbaya,...wanapelekwa na mihemko ya matukio mapya, kwa iyo usivunjike moyo kaza buti,sisi tunaona kazi yako, kuitengeneza nchi upya inaitaji nguvu na juhudi ya ziada, utuondoe maskini kwenye hili wingu jeusi lililotanda juu yetu,..tunakuamini Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, Tutazidi kukuombea. MUNGU AKUBALIKI
 
Kwani yeye ni malaika kusema hakosei?

Katika tawala zilizopita yeye pia ni miongoni mwa watu waliosababishia matatizo taifa hili. Possibly yeye anaweza kuwa 2nd after Mkwere

Kila uongozi una unique features zake, uwez kulaumu matatizo, ya uongozi wa zamani kweny uu mpya, ila jitihada zake zinakidhi kulekebisha Yale yaliyoachwa,
..???ndo swali
 
Mkuu umesahau kuacha jina na namba ya simu ili uteuzi ukupitie.

Ili kushinda jambo lolote lazima ujiandae na uwe na mipango mizuri inayoonekana.

Mpaka sasa tunaona ukurupukaji wa maamuzi bila kujali sheria za nchi. Ukurupukaji huu unaanzia juu kabisa mpaka kwa wakuu wa wilaya. Hili jambo watu wanalalamikia lakini mmeeka pamba masikioni.

Mwisho wake watu wanahofia kwa sababu kesi za fidia zitakuwa nyingi na hakuna jambo la maana litakalofanyika.

Unapozungumzia suala la ACACIA uelewe mahakama ndiyo ina wajibu wa kuamua huyu mtu ni mwizi au la! Kuita makamera na ushahidi wa hovyo na kuaminisha watu ACACIA ni mwizi haimaanisha kimahakama ACACIA ni mwizi.

Ni ushamba tu wa kufikiri kwamba kwa sababu wewe ni Rais basi ukisema mtu mwizi anakuwa mwizi. Hizi njia za kishamba ndo tunazipinga.

Unaweza ukawa na mapenzi mazuri na nchi na usiwe na mbinu za kuisaidia nchi.
 
Peleka upumbavu wako kwenye ofisi za ccm kule ndio watakupigia mpaka makofi.
359ac93cf93f08e4a9f8514438bf4ae0.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mwalimu Nyerere pamoja na kuwa wakati anaongoza nchi haikuwa na uelewa mkubwa kiasi cha sasa, upashanaji habari haukuwa kama wa sasa na wigo wa demokrasia haukuwa kama huu duniani pote achia Tanzania yetu lakini hakuwa na uendeshaji wa serikali wa aina hii primitive kabisa.
Alijali mawazo ya watu kwa namna fulani, katiba iliheshimiwa na alijua mipaka ya madaraka yake. Sasa miaka zaidi ya 50 tunajikuta kama ndio tunajifunza uongozi? Hii ni shida sana. Na nina uhakika this is one term president, hilo hata ccm wanalijua labda utumike ubabe ambao nahakika hata ndani ya ccm hawaukubali.
 
Hata Mwalimu Nyerere pamoja na kuwa wakati anaongoza nchi haikuwa na uelewa mkubwa kiasi cha sasa, upashanaji habari haukuwa kama wa sasa na wigo wa demokrasia haukuwa kama huu duniani pote achia Tanzania yetu lakini hakuwa na uendeshaji wa serikali wa aina hii primitive kabisa.
Alijali mawazo ya watu kwa namna fulani, katiba iliheshimiwa na alijua mipaka ya madaraka yake. Sasa miaka zaidi ya 50 tunajikuta kama ndio tunajifunza uongozi? Hii ni shida sana. Na nina uhakika this is one term president, hilo hata ccm wanalijua labda utumike ubabe ambao nahakika hata ndani ya ccm hawaukubali.

JPM anajitengenezea yeye mwenyewe mazingira magumu,

Kila mahali kuna chuki,

1. Ndani ya CCM wanachuki naye

2. Wapinzani wanachuki naye

3. Wasio na vyama wanamchukia

4. Wafanyakazi wanamchukia

4. Wanachuo wanamchukia

5. Wafanya biashara wanamchukia

Wanaojifanya kumpenda ni wale wanafiki wachumia tumbo wasiotaka kumwambia ukweli.

Kwa hali hii nani atamsaidia?

Ajirekebishe akishindwa aibu yake inakuja.
 
Katika maisha binadamu kaumbiwa changamoto nyingi kumfikishia malengo yake,

Kwa sasa naona Magufuli anapitia changamoto nyingi, hili ni pamoja na wananchi wake wenyew kutwa kumpigia kelele, lakini ukweli utajulikana baadae,

Wengi wa wananchi wanaopiga kelele ni wale wasioweza kufanya lolote zaidi ya kulaumu, mi nawaita "Losers" kuna makosa yalifanyika katika utawala zilizopita lakini, tujiulize jitihada gani zinafanyika sasa kuyarekebisha, wengi wetu tunalamikia vitu vilivyopo kweny hisia lakin tunashindwa kuangalia ukweli wa mambo,

Swala la ACACIA lilitakiwa kuangaliwa upya kutokana na mikataba chakavu iliyokuwepo, lakini watu hao hao, Leo ii wanalalamika kuona serikali inakurupuka, na kingine wanaweka vikwazo, muheshimiwa asishinde, lakin ivo ni vikwazo tu vya watu wasioweza kufanya chochote,
...sikuzote lawama haiui,ila fedhea, kwa iyo Magufuli kazi kazi, ii nchi ilikua imekwisha,.. Watu wanaitafuna wanavotaka, sasa wamekosa pa kushika, kazi kuweka vikwazo ili uonekane mbaya,...Watanzania wengi ni kama wafu, wanapelekwa na mihemko ya matukio mapya, kwa iyo usivunjike moyo kaza buti,sisi tunaona kazi yako, kuitengeneza nchi upya inaitaji nguvu na juhudi ya ziada, utuondoe maskini kwenye hili wingu jeusi lililotanda juu yetu,..tunakuamini Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, Tutazidi kukuombea. MUNGU AKUBALIKI
Wewe mwenyewe ndio first Looser.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom