Maaskofu & Masheikh - Mama wa Wizi & Ufisadi Amejipambanua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu & Masheikh - Mama wa Wizi & Ufisadi Amejipambanua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bill, Aug 19, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,243
  Trophy Points: 280
  Hatimaye Mama wa ufisadi nchini amejipambanua na kujiweka wazi kwa kila mwananchi. Katika vikao vya CC na NEC vya CCM vilivyomalizika Jumatatu 17/08/09 hakika imedhihirika mapambano dhidi ya Rushwa na Ufisadi yanayoendelea hapa nchini si kazi rahisi kwani kuna kundi kubwa lilolojipatia hati miliki ya mali ya nchi likiongozwa na kulindwa na mama yao CCM.

  Siyo rahisi kuupiga vita ufisadi bila kwanza kuipiga vita CCM, kwani mama wa hawa mafisadi ni CCM, na hawa watoto ndio wanaomlisha mama yao CCM. Haiwezekani kuwapiga vita akina RA,EL na Mzee wa Vijisenti bila kumgusa mama yao CCM. Kwa upande mwingine hata ikiwa hawa mafisadi wa sasa wataondoka Mama yao yaani CCM atazaa wengine kwa maana hiyo tatizo liko palepale.

  Kuukata mzizi huu wa ufisadi ni lazima kuanza na mama yao yaani CCM. CCM ni lazima iondoke sasa, imeshapoteza mwelekeo na mwelekeo wake ni dhahiri - Ufisadi.

  Wito kwa Maaskofu na Masheikh
  • Ikiwa ninyi mnahubiri amani, upendo, uvumilivu na ustawi wa kiroho na kimwili - Haya yote hayawezekani chini ya usimamizi wa Mama wa Mafisadi yaani CCM. Hubirini habari ya ukombozi kutoka katika kundi la hawa wadharimu ili haya yote yawezekane. Hubirini na kuhamisisha waumini wenu bila ya kificho, hubirini wazi wazi waumini wenu wakikikatae Chama cha Mafisadi
  • Hamasisheni waumini wenu kutokushabikia vyama bali utaifa. Chama kinaweza kufa lakini taifa letu litaendelea kuwepo hadi utimilifu wa dahari. Kwa hiyo fumbueni macho waumini wenu waache ushabiki wa kijinga kama inavyoenezwa na CCM kuwa maslahi ya chama kwanza. Hubirini maslahi ya nchi kwanza, Hakuna maana yoyote ya kutanguliza maslahi ya chama kwani hii ina maana ya kutanguliza mbele maslahi ya kundi fulani.
  • Waambieni waumini wenu kuikataa CCM kwani imeshajipambanua kuwa ni kundi la mafisadi na lisislozingatia katiba ya nchi kwa malengo ya kutimiza malengo yao. Kitendo cha kumkemea spika kinadhihirisha hili na kinajaribu kurudisha nyuma vita hii ya mapambano dhidi ya ufisadi. Hamasisheni waumini waikatae CCM kwani haina agenda ya msingi ya kuwaletea maendeleo.
  Hakika Hakuna njia nyingine mbadala ya kupambana na Ufisadi bila kwanza kuiondoa CCM na kuhakikisha inakufa kabisa. Mkakati mmoja wapo ni huo wa watumishi wa Mungu kuikataa na kuwahimiza waumini kuikataa CCM.

  Amri ya Mungu inazuia wizi "Usiibe", CCM leo inatetea wizi. Hakika CCM nao wanashiriki wizi

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA NA VIONGOZI WAO WA KIROHO
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kazi ipo kwa kweli, CCM imedhihirisha kuwa ni chama cha mafisadi
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Hao Maaskofu na Masheikh wakihubiri hivyo, tutasema wanachanganya dini na siasa. Wakikaa kimya tutasema wanabariki ufisadi! Whatever they will do or refrain from dpoing, we'll have something against them. The only right thing to do is for them to see what they can do and do it.
   
  Last edited: Aug 19, 2009
 4. K

  Konaball JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,767
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Kuijadili CCM mimi naona ni kupoteza wakati maamuzi mnayo wenyewe mwaka 2010 WADANGANYIKA wenzangu
   
 5. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Aisee ndugu zanguni sio lazima mungu atushike mkono kutusaidia kupiga kura. Ni kwamba hata malaria hujulikana kwa symptoms lakini huwezi extract malaria kutoka mwili wa mtu.

  Ndugu zanguni symptom za kwamba hatuna chama cha wanyonge kinachoitwa ccm zimethihirika baada ya long laboratory analysis ambayo imekuwa confirmed kwenye nec iliyomalizika jana.

  Kazi kwetu tuache ushabiki tulinde taifa letu. Hakuna dalili nyingine za usaliti zaidi ya zile za kutetea wezi,na mafisadi na kuwapiga vita maadui na wanaharakati wa ufisadi.
  Mwaka 2010 tuingie kwa kuiondoa ccm na kuwaweka watu safi. Naomba kuunga mkono hoja
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,243
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wanatufanya WaTZ wote ni mabwege na hakuna mtu mwenye akili. Wanalifanya bunge kuwa la chama kimoja kiasi kwamba wanataka kulielekeza nini cha kufanya.

  Huu upuuzi usipite bilakukemewa na wanaharakati na wapenda amani. Hapa ndio mahali pa kuanzia kwa watu wote wenye mapenzi mema na hii nchi.
   
Loading...