Katika haya yanayotokea Kila siku katika nchi yetu Maaskofu na Mashehe mnatakiwa kutoa kauli Kali kwa serikali hi ya Kikwete ambayo imeshindwa kulinda Amani ya raia wake. Mnapokaa kimya bila kuzikemea tabia hizi wakati zinavunjwa kwa makusudi hamuwatendei haki waumini wenu. Mnahubiri Amani makanisani misikitini mnashindwa nini kuikemea serikali? Acheni uoga nyie ni watumishi wa mungu inabidi mseme ukweli Daima hata Kama serikali itachukia ni wajibu wenu. Inatakiwa kuirekebisha serikali Kama inaenda mrama sio kuisifia tu. Waumini watawalaumu Kama mataacha hii hali na raia kuangamia. Yametokea Mtwara na Kila kona ya Tanzania lakini hamjatoa kauli yoyote kwa waumini wala serikali. Mtahubiri vipi Amani makanisani misikitini wakati Serikali inaua raia wake na ushahidi upo au nyie hamwoni wala kusikia. TOENI KAULI KATIKA KUIOKOA NCHI YETU MSIKAE KIMYA NI WAJIBU WENU.