Maaskofu kuliombea Bunge

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Kuna habari kuwa maaskofu wa kinachoitwa makanisa yasiyofungamana na upande wowote wamemwandikia spika wa bunge barua wakiomba kupewa nafasi ya kwenda Dodoma kuliombea Bunge ili lisikumbwe na mauzauza ya unga unga tena.

Pili kanisa limeamua kumrudishia Rostam sadaka yake leo .....

Mwanzo wa drama ama mwisho wa picha?

more news to come later.
 
Inabidi sasa akome kwenda kwenye vyombo vya ibada kuzungumza mambo ya siasa. Yes fisadi akwama sasa kutumia kanisa, sijui next move ni ipi? Kuna hatari ya kuwatokea machinga.
 
kwani sadaka huwa tunatoa kwa nani? mimi huwa natoa kwa Mungu, hivyo haiwezi kurudishwa mechanically.

Sadaka Unaitowa kwa Mungu na inatumiwa na watumishi wa Mungu kwa kazi ya Mungu.
Make sense?
 
Fedha za RA imeagizwa kuwa zirudishwe kwake mara moja.

Pili hawa maasikofu wamemwandikia spika barua ya kuomba kibali cha kwenda Dodoma kuliombea bunge ili lisikumbwe na mauzauza siku za usoni.
 
Du siku hizi ukitaka kuombea kitu mpaka upewe ruhusa!

Kwa kuwa sijaona kilichomo kwenye barua labda wanataka waruhusiwe kuingia ndani ya lile zulia lenye bendera ya taifa na kukalia viti vyote vyenye mahusiano na ungaunga.....
 
kama wanataka kuingia huko ndani basi wanataka kibali yasije yakawakuta ya Chenge!
 
Huyu ni Mungu gani ambaye wanamuomba ambaye anafungwa na umbali, muda, au mahali? Wamesahau kisa cha Binti wa Jemedari ambaye aliponywa toka mbali? Nadhani itabidi bunge liwaombee hao wachungaji ili wasiende Dodoma na warudishe fedha zote walizopokea toka mikononi mwa mafisadi!
 
sasa watanzania wameingiliwa,wasipoangalia watakosa hata pa kuomba maji.hao ni maaskofu uchwara wanaotafuta umaarufu kwa mgogo wa ufisadi.
 
Kitu hiki nilikiandika mwaka 2008 na bado leo kimetokea tena kuna timu ya Maasskofu wakiongozwa na mtume Fernandiz wa ATN wanaelekea Dodoma kwa ajili ya kuliombea bunge .

Wwat is this ? nini kinaendelea ? mwaka ule walisema kuwa ni kutokana na unga unga uliokutwa kwenye viti vya baadhi ya wabunge leo miaka 3 baadae bado hoja ni hiyo ama ni ipi? Nakumbushia
 
Ningekuwa na kauli ya mwisho kwenye hili ningesema hawa maaskofu wasikaribie kabisa eneo la bunge. Unless wanaenda kwa shughuli zingine kama mtu wa kawaida lakini si kwa kuliombea bunge. Tuachane kabisa na hii tabia ya kuchanganya siasa na wauza mafuta, maaskofu masheikh n.k. Bunge libaki huru, na kama issue ni kuomba si lazima waende bungeni, wanaweza kufanya mahali popote. Mimi nahisi hawa wanaenda ku-lobby. waondoke kabisa.
 
Wameanza safari leo asubuhi kutoka hapa DSM kuelekea huko Dom na walimwandikia Spika barua rasmi ...sasa ngoja tuone
 
Labda dua zao ni mfano wa singe kwenye bunduki za kizamani ambapo ili kumpiga nayo adui ni lazima umkumbatie kwanza. Huwezi kumpiga adui ukiwa mbali. Hawa "Mitume" wetu wa leo!

Pia ningewashauri waende na yule Kondoo aliyeandikwa YASIN akawaongezee nguvu
 
Kuna habari kuwa maaskofu wa kinachoitwa makanisa yasiyofungamana na upande wowote wamemwandikia spika wa bunge barua wakiomba kupewa nafasi ya kwenda Dodoma kuliombea Bunge ili lisikumbwe na mauzauza ya unga unga tena.

Pili kanisa limeamua kumrudishia Rostam sadaka yake leo .....

Mwanzo wa drama ama mwisho wa picha?

more news to come later.
Jamani habari nyeti kama hii inataka reference na soucrce maana ukisema makanisa yanarudisha sadaka ni ipi hiyo? au ni zote alizotoa tokea awe mbunge? ameyasema mwenyewe au ni askofu gani ametamka hayo?
 
Nasikia makao makuu KKKT wamewataka kinondoni wairudishe hiyo sadaka
<br />
<br />
Kama ni kweli basi, hao watumishi wa kanisa, wamepotoka. Maana TAJIRI Rostam alimtolea Yehova au Allah, na wala sio wahudumu wa nyumba za ibada. MSIHUKUMU, msije mkahukumiwa ninyi. Soma: Mathayo 7:1
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom