MAASKOFU, chonde chonde kizazi kinaangamia: ASKOFU MWINGINE ADAKWA NA UNGA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAASKOFU, chonde chonde kizazi kinaangamia: ASKOFU MWINGINE ADAKWA NA UNGA

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Tume ya Katiba, Jun 21, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Wadau, tuungane katika hili, hawa watu watamaliza kizazi chetu.


  MORIS Charles anayejitambulisha kuwa ni askofu wa kanisa moja la kiroho jijini Dar es Salaam amedakwa na unga hivi karibu katika Kijiji cha Mchingambili, mkoani Lindi.
  Vyanzo vya habari vimeeleza kwamba Charles ambaye wakati fulani hujitambulisha kwa jina la Yusuph Mohamed Lutengwe alidakwa nyakati za usiku Januari 11, mwaka huu akiwa katika gari lake aina ya Toyota Land Cruiser (namba zinaifadhiwa ).
  Taarifa hizo zimedai kwamba kudakwa kwa mtu huyo kulifuatia habari zilizowafikia polisi mapema ambapo waliarifiwa na aina ya gari analotumia Charles kupokea ‘unga’ au dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 210 zenye thamani ya shilingi bilioni 9.4.

  MTEGO WA POLISI
  Imeelezwa kwamba siku ya tukio polisi waliweka mtego baada ya kupata taarifa ya kiongozi huyo kuwa atakuja katika kijiji hicho na gari lake la kifahari, wakapewa namba na raia wema.
  Habari zinasema ilipofika saa tano usiku waliliona gari kwa mbali na lilipowakaribia, walilisimamisha lakini inadaiwa kuna mtu alichomoka ndani ya gari hilo na kutokomea gizani.
  Vyanzo hivyo vinadai kuwa jeshi la polisi halikumjua mtu huyo lakini baadaye wakaambiwa kuwa aliyekimbia ndiye huyo anayejiita Askofu Charles ambapo mtu mmoja aliyekuwa akiliendesha gari hilo alitiwa mbaroni.
  Habari hizo zilieleza kwamba muda huo huo watu aliokuwa akiwapokea wakiwa na madawa walikamatwa na polisi wa kikosi kazi.

  Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na Ismail Adamu (28), Hamad Said (27), Morine Amatus (22) na Pendo Mohammed Chausi (67) ambaye ni mwenye nyumba yalipokamatwa madawa hayo. Tayari watu hao wamepandishwa kizimbani.
  Habari zinasema polisi walimfuatilia askofu huyo na kugundua kuwa anaishi Mikocheni, jijini Dar es Salaam na wakafanikiwa kukamata mali nyingine ambazo ni magari mawili ya kifahari aina ya Porsche Cayenne na Jeep Wrangler.
  Hata hivyo, imeelezwa kuwa askofu huyo amefanikiwa kuwakimbia polisi na ametorokea nje ya nchi Januari 15, mwaka huu.

  Vyanzo hivyo vya habari vimedai kwamba kiongozi huyo wa dini huwa ana hati mbili za kusafiria, moja anatumia jina la Kiislam na huitumia anapotembelea nchi za Kiislam na nyingine yenye jina la Kikristo.
  Uchunguzi wetu umebaini kuwa hata magari anayotumia, usajili wake una utata kwani tulipofuatilia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) anayedaiwa kumiliki gari hilo Toyota Land Cruiser lililokamatwa na polisi ni Rashida Abushir Jumanne na aliuziwa na huyo kiongozi Januari 16, mwaka huu.
  Afisa mmoja wa TRA alisema mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Makame .O. Juma na kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba Juni 9, 20011 aliliuza kwa kiongozi huyo anayejulikana pia kwa jina la Lutengwe.

  UTATA WA GARI
  Kinachoshangaza ni kwamba Lutengwe alikimbia nchini Januari 15, mwaka huu, iweje auze gari kwa Abushiri Januari 16, mwaka huu wakati gari hilo tangu likamatwe Januari 11, mwaka huu bado lipo polisi hadi sasa?
  Hata hivyo, mwandishi wa habari hii akiwa TRA alipata namba ya simu ya Abushiri, alipopigiwa alipokea mtu ambaye alijitambulisha kuwa yupo Morogoro na alisema kwamba anamfahamu Abushiri ambaye anaishi Sinza jijini Dar es Salaam .

  Kijana aliyepokea simu aliwasiliana na Abushiri alimpa namba ya mwandishi na akapiga simu. Katika mahojiano alikana kwamba yeye hana gari aina ya Toyota Land Cruiser na hajawahi kulimiliki, akadai inawezekana jina lake na namba yake ya simu inatumika vibaya na wahalifu.
  Abushiri alipohojiwa zaidi na mwandishi sababu ya simu yake kumkabidhi mtu ambaye yuko Morogoro wakati yeye yupo Dar es Salaam alijitetea kuwa huyo ni mdogo wake, hivyo ameamua kumpa hiyo simu ili aitumie.
  Uchunguzi umebaini kwamba hata baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na madawa ya kulevya, simu zao zimegundulika kuwa waliosajiliwa ni marehemu waliokufa kati ya miaka miwili na mitatu na wengine walikuwa wakiishi Morogoro.

  Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alipoulizwa kuhusu kiongozi huyo alisema kwamba hayupo tayari kulizungumzia suala hilo kwa vile bado linachunguzwa.
  Hata hivyo, alikiri kwamba kuna mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya aliyekimbilia nje ya chini na kwamba magari yake yanashikiliwa na jeshi la polisi

  sosi: ASKOFU MWINGINE ADAKWA NA UNGA - Global Publishers
   
 2. B

  Bob G JF Bronze Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Naamini huyo hawezi kuwa askofu na hasa ukifuatilia wahusika wengine ambao wamekamatwa na ana majina ya aina zote. ametumia jina hilo kufanya uhalifu, Nivizuri polisi wajitahidi wamkamate muhalifu huyu
   
 3. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Askofu: Yusufu Mohamed???? Iwapo gazeti haliuzwi wanapachika title ya ASKOFU ili linunuliwe!!!!!
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  mbona ni habari ya siku nyingi......!
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Good job police!
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Lakini mbona tumechelewa kupata hbr hii?

  Kidogo hapo police wametufaa kama ni kweli wamelikamata gari na baadhi ya wahalifu bila ya kupokea takrima.
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hawa ni maaskofu pori kiuhalisia hana sifa ya kuwa askofu,mfano ili uwe askofu kwa wakatoliki ni lazima uwe na shahada mbili
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kichwa cha habari na content tofauti kabisa
   
 9. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Yaani saana!!watu wameishiwa na points!!
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Usiingizwe mkenge kitoto namna hii, wewe ni mgeni hapa JF? mleta mada hajaleta Habari kwa misingi ya kuopashana habari bali udini uliomkaa na ufuasi wa vikundi vya kigaidi kama Uamsho ndio vinamsumbuwa. hii habari tuliijadiri hapa miezi 3 iliyopita.

  Nadhani nia ya mleta mada anataka atokee chizi mwenzake naye abandike ile Habari Sheikh atiwa mbaroni kwa ulawiti. hawa ni wapuuzi.

  [h=1]ASKOFU MWINGINE ADAKWA NA UNGA[/h]
  • Posted by GLOBAL on March 6, 2012 at 8:00am
   
 11. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  mleta hii habari yawezekana alikuwa jela,tumsamehe hii habari ni toka mwezi wa kwanza,yawezekana ajui ata tuliondokewa na kanumba,anaweza kupost kama breaking news
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Afadhali wewe umesema...maana wengine wetu bwana tunapenda kusikia yale tunayotaka kuyasikia. Hawa sio maaskofu rasmi...ni wale wa kujipachika
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Huyu ni Gaidi tu mfuasi wa kikundi cha Uamsho.

  [​IMG] Tume ya katiba

  Today 01:08
  #1 [​IMG]
  [​IMG] JF Senior Expert Member Array


  Join Date : 6th April 2012

  Location : Chumbuni-Zanzibar

  Posts : 1,548

  Rep Power : 543

  Likes Received
  350

  Likes Given
  148
   
 14. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Hii ni thread ya kidini zaidi kwa sababu ni ya siku nyiingi sana. Na huyo aliyejidai askofu alithibitika kuwa ni USTAADHI Mohamed Yusufu. Hata hilo kanisa la kiroho alilotaja halipo! Kwa hiyo hii hi front nyingine ya waislamu wenye mtazamo finyu dhidi ya ustsaarabu wa kikristu.
   
 15. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Huyu Shigongo nadhani ana ugomvi binafsi na maaskofu,anaandika headline kubwa lakini kumbe wahusika wenyewe sio Maaskofu,yeye angefafanu kuwa ni askofu wa kanisa gani na kanisa lake lipo wapi.Kwani yule kada wa CCM Arusha,yule mmasai illiterate Mr Mollel aliyeokota Tanzanite na Kutajirika ghafla,akauziwa hotel isiyo na Parking ya PARSON si naye anaitwa askofu,lakini hana kanisa wala cheo chochote cha kidini?lakini awezi kukamatwa na kosa kubwa ukaandika MAADILI YAMOMONYOKA,ASKOFU AKAMATWA KWA KOSA LA..HuKO ARUSHA,sana sana utaandika yule mfanyabiashara maarufu na kada wa CCM anayejiita Askofu......etc etc.Shigongo acha kuchafua dini za watu!
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,846
  Trophy Points: 280
  mbona umekimbilia kwa maaskofu moja kwa moja..kwani hakuna mashekhe wauza unga??
  waulize wabunge walioona ule mkanda pale bungeni wakupe japo kaukweli kiduchu...unaeza ukagoma kuswalishwa na baadhi ya mashekhe wa misikiti fulani fulani hapa daslam
  SUALA LA KUJIPATIA FEDHA KINYUME CHA TARATIBU ni tabia ya binadamu woote hakuna dini hapa "A SUSPECT SHOULD REMAIN A SUSPECT"
   
 17. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  eshimuni maaskofu, huyu ni pure askofu sema kapituka. kwa nini hamtaki kukiri taifa linapotea
   
 18. Constantine Akitanda

  Constantine Akitanda Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  [​IMG]
  HEAD OFFICE​
  P.O BOX2233, MBEYA, TANZANIA
  EAST AFRICA​
  Registration No. SO NO 12079​
  Tel: No. 0717655775​
  Kumb.Na. HP/MBY/VOL.9/5/3 Tarehe 30/ June, 2012
  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
  Rais wa Jamhuri ya Muungano – Tanzania,
  IKULU,
  D'SALAAM.
  YAH: HALI YA KISIASA MKOA WA MBEYA.
  Tafadhali rejea kichwa cha habari tajwa hapo juu.
  Mheshimiwa, wakati huu ambapo tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa nimeonelea kama rafiki tuelezane juu ya hali halisi ya mkoa wa Mbeya, lazima nimshukuru Mungu kwa muongozo wa busara aliyokupa mpaka ukamteua Mh. John Livingston Mwakipesile kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya, uteuzi ambao umeleta tija na ufanisi mkubwa katika Mkoa wa Mbeya. Nitakuwa sina utu ikiwa sitakushukuru kwa uamuzi wako mzuri na wewe kusikia kilio chetu wananchi wa mkoa huu tajwa Mh. John Mwakipesile aendelee kuwepo hapa na kusaidia kama mkuu wa Mkoa na mtetezi Mkuu wa Chama mama na Tawala CCM katika Mkoa huu.
  Mheshimiwa Mwakipesile amepita vita katika vita kubwa kwa kushambuliwa sana na wabunge wachache ambao walikuwa na agenda zao za siri na mbaya, wabunge hawa waliandika barua nyingi sana za majungu, shutumu na za kashifa ambazo zingine zilikufikia. Bado pia baadhi wameitisha mikutano ya hadhara na kumtukana mkuu wa mkoa na familia yake kitu cha ajabu wabunge hawa bado wamefikia hatua ya kuwaambia viongozi baadhi ya waandamizi wa CCM kuwa kuwa Mh. Mwakipesile hapendwi mkoa wa Mbeya. Kwa kuzingatia Ibara No. 32 ya Katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977 nina uhakika uteuzi wako kwa Mh. Mwakipesile ulizingatia sheria. Huyu Mkuu wa mkoa ni jicho lako hapa kwa nini atukanwe? Kwa nini baadhi ya wabunge wapuuzi wachache wampige vita Mkuu wa mkoa ambaye Mkoa wake mwaka 2009 umefanikisha kuwezesha watoto 41,000 kujiunga na kidato cha kwanza ni Mkoa gani Tanzania uliofikia hatua hii halina ubishi kabisa. Huu Mkoa wakati wa utawala wa Mh. Mramba na Ndugu Mateo Kares usalama ulikuwa Mbovu, ulikuwa umetawaliwa na ujambazi wa silaha, wachuna ngozi, upigaji nondo, magendo ya sukari ya MALAWI, NA VIPODOZI VYA Afrika ya Kusini ambavyo ni hatari kwa afya.
  Mheshimiwa Mwakipesile alitoa mikakati mikali sana kwa aliyekuwa Kamanda POLISI Mkoa SACP Kova na mkuu Usalama wa Taifa Mh. Saidi Salimin (Mkoa wa Mbeya) na hiyo hali alitoweka.
  Mbeya leo Mkoa shwari na mfano Mkuu wa mkoa bado alisimamia operesheni kabambe kufuta uhamiaji haramu wa kisomali na kazi hili kiufasaha aliifanya mkuu wa uhamiaji Mkoa Mh. Matana.
  Mheshimiwa, Mkuu wako wa Mkoa wa Mbeya siyo Kiongozi anayeshinda ofisini kusubiri taarifa ni Mkaguzi mzuri wa maedneleo na miradi ya umma, miundo minu na kazi za serikali Mkoa wa Mbeya.
  Mheshimiwa, Wabunge hao wanaovuruga Mkoa wa Mbeya orodha ipo mezani kwako kuna umuhimu mkubwa kuwa mwaka 2010 chonde wapumzike, majungu yao wamewapa wananchi wa Mkoa wa Mbeya muda mgumu. Imefikia hatua wanahcochea wananchi wa Mkoa wamchukue mkuu wa Mkoa.
  Mheshimiwa unaendelea katika uchaguzi wa serikali za mtaa napenda kukuhakikishia kuwa usalama Mkoa wa Mbeya chini ya Usimamizi wa Mh. Mwakipesile akisaidiwa na wakuu wa Wilaya zake na mkuu wa usalama wa Taifa Mh. Said Salim. Tumempokea Kamanda wa Polisi mpya ACP Advocate Nyombi ambaye ni mchapa kazi na chini ya Mh. Mwakipesile kazi zitakwenda vizuri.
  Mheshimiwa, wewe ni kiongozi usiyekurupuka kuchukua hatua lakini hao Wabunge kuna umuhimu wa kuwa shughulikia.
  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
  Wako katika ujenzi wa Nchi yetu ya Tanzania
  Mulilege Mkombo
  ASKOFU MKUU MWANZILISHI
  Nakala kwa. Mh. Ally Mohamed Shein
  Makamu wa Rais
  IKULU – DSM

  " " Mh. Mizengo Peter Pinda (MB)
  Waziri Mkuu wa JAMHURI
  Dsm
  " " Mh. Pius Msekwa (MB)
  Makamu Mwenyekiti – Bara
  CCM – MAKAO MAKUU

  " " Mh. Yusufu MAKAMBA (mb)
  Katibu Mkuu
  CCM – Tanzania

  " " Mh. Kapt. George Mkuchika (MB)
  Naibu Katibu Mkuu CCM

  " " Mh. Kapt. John Chiligati (MB)
  Siasa, Uenezi na Hitikadi - CCM
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Tume ya katiba, I wish you could know what I have in mind...Askofu sio cheo cha kugombaniwa barabarani...ni uteuzi anaopewa mtu tena kwa kuwekwa wakfu. Askofu anapaswa kuongoza waamini kumuelekea Mungu. Ushaona wapi askofu muuza unga? Unafikiri kila mtu anayesema bwana bwana ataenda kwa Mwenyezi Mungu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ndahani, hii habari sijaitunga, na ndio maana nimeweka link ya habari corporation for your reference, ipo very clear ASKOFU adakwa na unga! sasa usichoelewa ni nini? huyu atabakia kuwa askofu, tukubaliane kuwa amepotea njia, na ni ishara ya kizazi chetu kupotea pia maana mchungaji wa kondoo anawachinja kondoo wake!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...