Maandishi meusi yaliyoandikwa kwa wino mweusi

Jumannnne

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
667
2,001
Nawasalaam ndugu zangu wapendwa natumai wote ni wazima wa afya.

Moja kwa moja nianze na maandishi yangu meusi yaliyo katika karatasi nyeupe na haishangazi sana mana ni utaratibu na uandishi wenye kusomeka kama sio kueleweka kwa urahisi zaidi na ndio maana unapata nafasi maridhawa ya kusoma utakavyo, just imagine ningetumia karatasi nyeupe kuandika kwa wino wa rangi nyeupe sidhani kama ungeona kitu wala kuelewa.

Rangi ni kielelezo cha ufahamu, maono, uhalisia na hata fumbo ajabu ni kuwa Tanzania ya leo haijuwi ni rangi gani itumike katika kupambia nguzo zake nzito za pamba.

Ni muongo wa sita sasa nchi yangu ya bado inapambana na umasikini, ujinga na maradhi na tumejitowa kwa nguvu zote kupambana na maadui hawa ila cha ajabu ni kwamba utekelazaji wa mapambano umeandikwa kwa maandishi nyeusi yaliyo ktk karatasi nyeusi sasa najiuliza huyu muandishi alikuwa anawaza nini?

Kichekesho ni kwamba maadui zetu wanapendwa sana na waandishi wetu yani wanafurahi sana wanapoona ujinga, umasikini na maradhi vinavyokutesa wanajuwa hauwezi kusoma utekelazaji wa mapambano kwa kuwa wameyameandika kwa wino mweusi katika karatasi nyeusi na anapotokea mwerevu wa kutaka kuandika utekelazaji wa mapambano katika mtindo wa kisasa yani mchanganyiko wa nyeusi na nyeupe hawezi kueleweka anaonekana sio mwenzetu.

Mapambano yaliyoandikwa hayaeleweki ila yanapendwa na kulindwa na werevu wanaopenda ujinga wenye faida kwao, alafu hata hawashituki na wewe unawaona wenzako kisa tu unaipenda hiyo rangi ya kijani na njano kwakuwa inafanana na timu yako pendwa ya Yanga Afrika alafu unajisifu haujawai kupoteza yani kila mwaka wa uchaguzi wewe ni tiki tu, na unawacheka wenzako wa Simba SC kwa kufungwa goli la Mkono na Tambwe aliyewai kuichezea timu hiyo miaka michache iliyopita.

Nasikitika kukuharifu hata wewe pia uliibiwa kura yako licha ya kuiweka sehemu iliyojipatia umiliki mkubwa wa mchezo ni kwasababu hauna tofauti na waliofungwa unabaki tu kujinunulia jezi kama wao, pole sana tatizo lako wewe ni mjinga tena mgonjwa na hauna kipato cha mana.

Embu tafuteni karatasi nyeupe na wino mweusi tufanye jambo la msingi au hamjachoka kusoma msivyovielewa? Simba na Yanga embu jaribuni kuchangia karatasi nyeupe na nyeusi labda mtasomeka vyema.

Nashauri Rais wa Yanga avuwe hiyo miwani haitamsaidia kusomea kwenye hayo maandishi meusi yaliyo katika karatasi nyeusi ni zaidi ya upofu.
 
Back
Top Bottom