Maandamano zaidi yapangwa kufanyika Sudan, Waziri Mkuu atoa wito wa makubaliano ya kisiasa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amesema utulivu na umoja wa Sudan uko hatarini.

Hamdok ametoa wito wa kuwepo kwa makubaliano ya kisiasa, ili kulinda nchi siku zijazo, wakati taifa hilo likiwa limegubikwa na maandamano makubwa ya kupinga mapinduzi ya kijeshi.

Akizungumza kabla ya maandamano yaliopangwa kufanyika leo Jumapili, kuadhimisha miaka mitatu ya maandamano ambayo yalianzisha vuguvugu maarufu la uasi ambalo lilipelekea kupinduliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.

Hamdok amesema Sudan inakabiliwa na kikwazo kikubwa katika mchakato wa mageuzi ambayo inatishia usalama, umoja na utulivu wa nchi, na kulirudisha nyuma taifa hilo

Mapinduzi ya Oktoba 25 yalihitimisha ushirikiano uliokuwepo kati ya jeshi na vyama vya siasa vya kiraia baada ya kuondolewa al-Bashir.

Vyama hivyo, na kamati za upinzani za mitaa ambazo zimeandaa maandamano makubwa, wamekataa mazungumzo na ushirikiano na jeshi.

Chanzo: DW Swahili
 
Baada ya kuwasaliti watu wake, Hamdok haaminiki tena na muda si mrefu atapigwa chini.
 
Baada ya kuwasaliti watu wake, Hamdok haaminiki tena na muda si mrefu atapigwa chini.
Hajawasaliti tena Hamdok ni mgumu pamoja na kuwekwa under house arrest hakukubali lolote walilomwambia mpaka walipoamua kumuachia na wananchi wakiwa bado wanaandamana. Hao raia hawaelewi, Hamdok anaelewa bado jeshi linatakiwa kwenye stability ya nchi ingawa haliitajiki kwenye serikali. Nchi kwa miaka zaidi ya 30 ilikuwa inaenda kidikteta na kijeshi huwezi weka raia tu ikawa rahisi. Taratibu isije kuwa kama Ethiopia
 
Back
Top Bottom