Maandamano yasiyo na ukomo hayana tija-Cheyo

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Imeandikwa na Mwandishi Maalumu, New York; Tarehe: 29th November 2011 Habari Leo

MAANDAMANO yasiyokuwa na ukomo na yasiyozingatia utawala wa sheria, vurugu na fujo zinazofanywa na vijana kwa kisingizio cha kutaka fursa sawa na uwajibikaji, hayawezi kujenga
mazingira ya uzalishaji wa ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa UDP ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi
Mashariki, John Cheyo wakati alipochangia majadiliano kuhusu fursa na changamoto za ushiriki wa vijana katika demokrasia.
Cheyo ni kati ya wabunge wawili wa Tanzania wanaohudhuria mkutano wa siku mbili unaoshirikisha wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ulioandaliwa na UN kwa kushirikiana na Chama cha Mabunge (IPU).

Mshiriki mwingine ni Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu (CCM).
Cheyo alisema ingawa vijana wanadai uwajibikaji zaidi kutoka Serikali zao pamoja na fursa za ajira, lakini ajira na fursa hizo haziwezi kupatikana katika mazingira ambayo yametawaliwa na vurugu na maandamano asiyokuwa na kikomo.
Akizungumzia ushiriki wa vijana katika siasa, Cheyo alisema bila ya kubadili mifumo ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya makusudi itakayoongeza idadi ya vijana mabungeni, vijana wengi hususani barani Afrika watabaki kuwa wasindikizaji badala ya kuwa
washiriki.

Alisema vurugu nyingi na maandamano yasiyokwisha na yanayoendelea sehemu mbalimbali duniani na yakiwahusisha zaidi vijana, yanatokana na sababu nyingi, lakini kubwa ni kunyimwa fursa za kushiriki siasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom