Maandamano yasiyo koma kupinga KATIBA endapo isipokidhi mahitaji.

Ningewashauri wakina Kibamba wachukue ile staili ya CDM kama pale NMC Arusha,
waweke point kila mkoa.
Wala hamna kutoka jasho, watu mnaenda pale kwenye mkutano mnakaa mnapiga stori mnasikiliza hotuba za mapinduzi, mixer manyimbo ya ukweli ya kiharakati.
Tehe tehe tehe machalii wa Arusha wanaita nyimbo za ukombozi. Kazi ipo.
 
Aisee ntachukua likizo kazini ili nishiriki hayo maandamano. CCM wanajifanya wanajua kila kitu kuchakachua mpaka katiba safari hii wamenoa TUTAANDAMANA Mpaka ikulu pale tuchukue nchi. Suala la katiba ni nyeti sana tena sana wasicheze na akili zetu.

Mkuu niliposoma hii post yako ukanikumbusha makala moja kwenye Raia Mwema aliandika jamaa ninayemkubali sana anajiita Msomaji Raia makala yake ilienda kwa jina la "TUTAANDAMANA NA KUFUTURU PAMOJA".
Toka nmeonja staili ya "ku-OCCUPY" nadhani ni bora zaidi kuliko maandamano, natamani wakina Kibamba wangeliona hili au wangeomba consultation kwa wataalamu wa harakati hizi hapa bongo.
 
Nadhani kesho JF itakuwa busy sana kutokana na jinsi watu watavyokuwa wanapashana habari. Mwenye softcopy ya huo mswaada tafadhali jamani auweke jukwaani.
 
Back
Top Bottom