Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Polisi wamefyatua gesi za kutoa machozi na maji kwenye makundi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana nje ya bunge la Indonesia juu ya mapendekezo ya sheria mpya ya uhalifu itakayozuwia tendo la ngono kabla ya ndoa.
Maandamano dhidi ya mswada huo pia yalifanyika katika miji mingine nchini humo.
Mswada huo pia unaharamisha kisheria aina nyingi za utoaji mimba na kumtusi rais itakuwa ni kinyume cha sheria.
Mswada huo umekuwa ukicheleweshwa, lakini waandamanaji wanahofu kuwa inaweza hatimae kupitishwa na bunge.
Pendekezo la sheria mpya ya uhalifu inajumuisha yafuatayo;
Licha ya kucheleweshwa kwa kura hiyo, Waindonesia wengi wanahofia kwamba muswada huo unaweza kupitishwa na bunge na hivyo kuwazuwia ''haki zao''.
Aidha wanahasira juu ya kupitishwa kwa sheria mpya inayodhoofisha mamlaka ya tume ya kupambana na ufisadi , ambayo ni muhimu katika juhudi za kumaliza rushwa.

- Ngono kabla ya ndoa litakuwa ni kosa la jinai na mhusika anaweza kufungwa mwaka mmoja jela
- Kuishi pamoja nje ya ndoa inaweza kukusababishia kifungo cha miaka sita jela
- Kumtukana rais, Makamu wa rais , kiongozi wa kidini, taasisi za serikali na nembo kama vile bendera na wimbo wa taifa itakuwa ni ukiukaji wa sheria
- Iwapo mtu atatoa mimba atafungwa kifungo cha miaka minne jela iwapo hakutakuwa na sababu za kimatibabu au ubakaji