Maandamano yaendelea ndani ya Israel kuhusu ufisadi na wizi wa Netanyahu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,840
17,438
Maandamano yaendelea ndani ya Israel; Netanyahu ayafumbia macho na kuendeleza siasa za chuki dhidi ya Iran.

Wakazi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel wamefanya maandamano kwa wiki ya 32 mfululizo dhidi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni.

Maandamano hayo yalianza mwezi Mei mwaka uliopita wa 2020. Netanyahu anakabiliwa na mafaili manne muhimu ya uongozi mbaya na ufisadi wa kifedha. Akiwa na mke wake Sara, wawili hao wanatuhumiwa kwa pamoja katika faili linalojulikana kama '1000', ambapo wameshtakiwa kwa kupokea hongo na zawadi zenye thamani kubwa zikiwemo sigara za bei ghali. Katika faili linalojilikana kama '2000' Netanyahu anatuhumiwa kukubaliana na Arnon Mozes mmiliki wa gazeti la Yedioth Ahronoth kwa ajili ya kumpendelea katika upashaji habari naye Netanyahu alibane gazeti shindani la Israel Today kwa manufaa ya Yedioth Ahnonoth.

Faili linalojulikana kama '3000' linamuhusisha katika kashafa ya kupokea rushwa katika ununuzi wa nyambizi kutoka Ujerumani. Faili la '4000' nalo linamuhusisha waziri mkuu huyo na kashfa nyingine katika wizara ya mawasiliano ya Israel pamoja na shirika la mawasiliano la Bezeq. Netanyahu amekuwa akitumia ushawishi mkubwa alionao serikalini kuzuia juhudi zozote za kufuatilia ufisadi wake serikalini na amefanikiwa kwa kiwango fulani katika uwanja huo.

Netanyahu na mkewe Sara wanatuhumiwa kuhusika na kashfa kubwa za ufisadi na wizi wa fedha

Pamoja na hali hiyo, Waisreali wamekuwa wakifanya maandamano ya kila wiki kulalamikia ufisadi na kashfa za kifedha zinazomkabili waziri mkuu huyo pamoja na njama yake ya kuzuia kufuatiliwa kisheria, kwa kisingizio cha kuenea virusi vya corona katika ardhi hizo za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Ubuniwaji wa serikali ya mseto kati ya Netanyahu na Benny Gantz, mkuu wa Chama cha Buluu na Nyeupe na ambaye pia ni Waziri wa Vita wa utawala ghasibu wa Israel, ni jambo jingine ambalo linachochea maandamano ya kila wiki ya raia wa ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu. Hivi sasa katika hali ambayo bunge limevunjwa kwa mara ya nne na uchaguzi wa nne wa bunge hilo kupangwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu, wakazi wa ardhi hizo wamekuwa wakifanya maandamano hayo kwa ajili ya kumlazimisha Netanyahu ajiuzulu na kutoshiriki katika serikali ijayo.

Kuenea kwa kasi virusi vya corona na kushindwa serikali ya Netanyahu kukabiliana na virusi hivyo na vilevile kufungwa mara kwa mara viwanda na vituo muhimu vya uchumi, ni suala ambalo limewasababishia matatizo mengi wakazi hao na kuwafanya wamshinikize Netanyahi ajiuzulu. Hizo ndizo sababu ambazo zimewapelekea washiriki katika maandamano ya kila wiki ili kumlazimisha waziri mkuu huyo mfisadi aondoke madarakani.

Pamoja na hayo, Netanyahu ameyafumbia macho maandamano na malalamiko hayo ya Wazayuni na badala yake kujishughulisha na siasa za chuki na uhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Yeye na wenzake ambao hawajaridhidhswa na ushindi wa Rais Joe Biden wa Marekani, wanaishinikiza serikali mpya ya nchi hiyo ifuate siasa za rais aliyeondoka madarakani, Donald Trump hasa kuhusiana na suala la mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Kwa msingi huo Netanyahu amemuonya Rais Biden asirejee katika mapatano hayo ya Iran yaliyofikiwa mwaka 2015.

[https://media]Maandamano makubwa yanayofanyika kila wiki mjini Tel Aviv dhidi ya Netanyahu

Mbali na hayo, baadhi ya maafisa wa serikali ya Netanyahu wanaendelea kupiga ngoma ya vita na badala ya kuzingatia matatizo ya ndani ya Israel, wameamua kuendeleza uchochezi na vitisho dhidi ya Iran. Katika uwanja huo Aviv Kochavi, mkuu wa jeshi la Israel amesema kuwa jeshi hilo linaimarisha mipango yake ya kioperesheni ili ikihitajika iweze kutumika dhidi ya miradi ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameendelea kusema kuwa ikiwa jamii ya kimataifa itaamua kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya 2015 itakuwa imefanya kosa kubwa hata kama mapatano hayo yatakuwa yamefanyiwa marekebisho.

Hata kama kwa sasa kutoa mashinikizo dhidi ya serikali mpya ya Joe Biden nchini Marekani na kuzidisha vitisho dhidi ya Iran ni siasa zinazopewa kipaumbele na serikali ya Netanyahu, lakini ni wazi kwamba kupotoshwa fikra za waliowengi huko Israel kwa ajili ya kupunguza mashinikizo dhidi ya waziri mkuu huyo ni jambo ambalo halitamsaidia lolote katika kupunguza mashinikizo na maandamano yanayofanyika kila wiki dhidi yake.

Tags

ISRAEL
4bvb1943d1ab6a1p7mc_800C450.jpeg

MAANDAMANO
 
Nani anamiliki vyombo vya habari vya kimataifa?
Yupo upande gani kati ya wananchi na kiongozi?
Vyombo unavyosema bina maslahi gani hapo israel?
Anayemlipa mpiga zumari media anachangua mwimbo mkuu
Taarifa ngapi Aljazeera anaripoti kuhusu Israel hii hakuiona??
Sometimes mnajiabisha kwa ushabiki maandazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Israel bado inamuhitaji Sana netanyah kwa Sasa,ukiangalia bado Wana bifu kubwa na Iran,pamoja na mapungufu hayo madogo madogo ,bado Wana mhitaji huyu kuwabana wa Iran,netanyah uzalendo kwa taifa lake ndio unaompa heshima kubwa na kukubalika pale israel.hata Iran inajua Hilo na inamgwaya Sana netanyah,kuuawa kwa yule general wao wa Iran wanaamini netanyah pia ameshiriki na iko hivyo.israel haiwez kufanya ujinga kumtoa netanyah kwa kipindi hiki.
 
Acha ujinga ww unadhani hizo nchi zinaongozwa na mawazo za mtu mmoja kama nchi za bara la giza?
Israel ni nchi inayo ongozwa na mfumo imara na haitegei mtu mmoja ili kuwa Imara.
 
Sasa hao mosad wanatukuzwa sana wanafanya kaz gan kama ni full maufisad mpaka huko!?
Tuache kuilaumu tiss kwa mtindo huu
 
Maandamano yaendelea ndani ya Israel; Netanyahu ayafumbia macho na kuendeleza siasa za chuki dhidi ya Iran.

Wakazi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel wamefanya maandamano kwa wiki ya 32 mfululizo dhidi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni.

Maandamano hayo yalianza mwezi Mei mwaka uliopita wa 2020. Netanyahu anakabiliwa na mafaili manne muhimu ya uongozi mbaya na ufisadi wa kifedha. Akiwa na mke wake Sara, wawili hao wanatuhumiwa kwa pamoja katika faili linalojulikana kama '1000', ambapo wameshtakiwa kwa kupokea hongo na zawadi zenye thamani kubwa zikiwemo sigara za bei ghali. Katika faili linalojilikana kama '2000' Netanyahu anatuhumiwa kukubaliana na Arnon Mozes mmiliki wa gazeti la Yedioth Ahronoth kwa ajili ya kumpendelea katika upashaji habari naye Netanyahu alibane gazeti shindani la Israel Today kwa manufaa ya Yedioth Ahnonoth.

Faili linalojulikana kama '3000' linamuhusisha katika kashafa ya kupokea rushwa katika ununuzi wa nyambizi kutoka Ujerumani. Faili la '4000' nalo linamuhusisha waziri mkuu huyo na kashfa nyingine katika wizara ya mawasiliano ya Israel pamoja na shirika la mawasiliano la Bezeq. Netanyahu amekuwa akitumia ushawishi mkubwa alionao serikalini kuzuia juhudi zozote za kufuatilia ufisadi wake serikalini na amefanikiwa kwa kiwango fulani katika uwanja huo.

Netanyahu na mkewe Sara wanatuhumiwa kuhusika na kashfa kubwa za ufisadi na wizi wa fedha

Pamoja na hali hiyo, Waisreali wamekuwa wakifanya maandamano ya kila wiki kulalamikia ufisadi na kashfa za kifedha zinazomkabili waziri mkuu huyo pamoja na njama yake ya kuzuia kufuatiliwa kisheria, kwa kisingizio cha kuenea virusi vya corona katika ardhi hizo za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Ubuniwaji wa serikali ya mseto kati ya Netanyahu na Benny Gantz, mkuu wa Chama cha Buluu na Nyeupe na ambaye pia ni Waziri wa Vita wa utawala ghasibu wa Israel, ni jambo jingine ambalo linachochea maandamano ya kila wiki ya raia wa ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu. Hivi sasa katika hali ambayo bunge limevunjwa kwa mara ya nne na uchaguzi wa nne wa bunge hilo kupangwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu, wakazi wa ardhi hizo wamekuwa wakifanya maandamano hayo kwa ajili ya kumlazimisha Netanyahu ajiuzulu na kutoshiriki katika serikali ijayo.

Kuenea kwa kasi virusi vya corona na kushindwa serikali ya Netanyahu kukabiliana na virusi hivyo na vilevile kufungwa mara kwa mara viwanda na vituo muhimu vya uchumi, ni suala ambalo limewasababishia matatizo mengi wakazi hao na kuwafanya wamshinikize Netanyahi ajiuzulu. Hizo ndizo sababu ambazo zimewapelekea washiriki katika maandamano ya kila wiki ili kumlazimisha waziri mkuu huyo mfisadi aondoke madarakani.

Pamoja na hayo, Netanyahu ameyafumbia macho maandamano na malalamiko hayo ya Wazayuni na badala yake kujishughulisha na siasa za chuki na uhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Yeye na wenzake ambao hawajaridhidhswa na ushindi wa Rais Joe Biden wa Marekani, wanaishinikiza serikali mpya ya nchi hiyo ifuate siasa za rais aliyeondoka madarakani, Donald Trump hasa kuhusiana na suala la mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Kwa msingi huo Netanyahu amemuonya Rais Biden asirejee katika mapatano hayo ya Iran yaliyofikiwa mwaka 2015.

[https://media]Maandamano makubwa yanayofanyika kila wiki mjini Tel Aviv dhidi ya Netanyahu

Mbali na hayo, baadhi ya maafisa wa serikali ya Netanyahu wanaendelea kupiga ngoma ya vita na badala ya kuzingatia matatizo ya ndani ya Israel, wameamua kuendeleza uchochezi na vitisho dhidi ya Iran. Katika uwanja huo Aviv Kochavi, mkuu wa jeshi la Israel amesema kuwa jeshi hilo linaimarisha mipango yake ya kioperesheni ili ikihitajika iweze kutumika dhidi ya miradi ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameendelea kusema kuwa ikiwa jamii ya kimataifa itaamua kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya 2015 itakuwa imefanya kosa kubwa hata kama mapatano hayo yatakuwa yamefanyiwa marekebisho.

Hata kama kwa sasa kutoa mashinikizo dhidi ya serikali mpya ya Joe Biden nchini Marekani na kuzidisha vitisho dhidi ya Iran ni siasa zinazopewa kipaumbele na serikali ya Netanyahu, lakini ni wazi kwamba kupotoshwa fikra za waliowengi huko Israel kwa ajili ya kupunguza mashinikizo dhidi ya waziri mkuu huyo ni jambo ambalo halitamsaidia lolote katika kupunguza mashinikizo na maandamano yanayofanyika kila wiki dhidi yake.

Tags

ISRAELView attachment 1693098

MAANDAMANO
Hii taarifa imetokea parsday na Igna imeandikwa kichuki sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom