Kikundi cha watanzania wanaojiita wanaharakati wazalendo leo kimeitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza azimio la kufanya maandamano siku ya Jumapili kwa lengo la kulaani mgomo wa madaktari unaoendelea nchini!
Awali maandamano hayo yalipangwa kufanyika kesho Jumamosi,lkn yakaahirishwa ili kupisha mazungumzo kati ya Rais Kikwete na viongozi wa chama cha madaktari.Sina hakika na tafsiri ya neno 'wanaharakati wazalendo',iwapo maana yake ni kuwa kuna wanaharakati mamluki au la,lkn hili si lengo langu.
Kilichonisukuma kuandika hii thread ni kwanza jinsi walivyowashambulia madaktari waliogoma.Niliudhika na kauli yao kuwa madaktari wasijifanye ni watu muhimu sana kuliko wengine na kadhalika.Sasa nikajiuliza,kama madaktari si muhimu,kuna umuhimu gani wa kuweweseka kuwataka warudi kazini?Kwa nn tusiwaache tu waendelee na mgomo?
Pili,ni namna kibali cha maandamano yao kilivyotolewa chapchap na polisi,tofauti na maandamano mengine ya watu wengine ambapo hudaiwa kuna taarifa za kiintelijensia kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani!
Hapa utagundua kuwa kumbe ili upate kibali cha kuandamana,inabidi lengo la maandamano yako liwe ni kuunga mkono upande wa chama tawala au serikali na si kwa kigezo cha maandamano ya amani.
Ni dhahiri kuwa kikundi kingine kikioma kibali cha kuandamana kwa lengo la,mfano,kuunga mkono mgomo wa madaktari hakutakuwa na kibali kitakachotolewa na hata kama kitatolewa na maandamano hayo yakafanyika sambamba na haya ya 'wanaharakati wazalendo' polisi watatembeza bakora upande mmoja.
Kwa hiyo hii intelijensia ya hawa jamaa huwa ni janja ya kisiasa tu.