Maandamano ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,963
3,805
Wanafunzi wa shule kadhaa za jiji la dar waliokuwa katika maandamano (yasiyo ya amani) ya kupinga ongezeko la nauli kutoka tsh 50 hadi Tsh 100 leo walifanya uharibifu wa magari kadhaa ya daladala.

Maeneo ya Ilala-boma kulionekana magari kadhaa yakivunjwa vioo na wanafunzi hao. Kati ya magari yaliyovunjwa na kuharibiwa ni lililopewa jina h.G Trans na lingine City Boy.

Askari walitawanya wanafunzi hao wakiwa tayari wamefanya uharibifu.
 
Nchi yetu inaelekea kubaya. Ukiona vijana wadogo wameanza kudiriki kuwa defiant kwa kiasi hiki basi ni ishara ukutani kuwa things are bad! Viongozi wetu walione hili na watafute ufumbuzi wa matatizo ya wananchi.
Mitaani nako yanayozungumzwa ni wazi kuwa matabaka yanazidi kujengeka na kufgawa watanzania - wenye nacho na wasio nacho, maadam hakuna viashiria vya wazi kuonyesha nani ni fisadi na nani anajipatia riziki yake kihalali basi kila aonekanaye na unafuu wa maisha anawekwa kwenye kundi la MAFISADI! sijui tunaelekea wapi ndugu zanguni! TUAFANYE NINI?
 
Maadam wadogo zetu wamejua kuwa tunatesana bila sababu za msingi,ni dalili nzuri kuwa si mda mrefu nchi yetu itapata wapiganaji wapya.
 
Hivi zile SCHOOL BUSES ziko wapi jamani?

Kama zingekuwepo haya yote yasingetokea hii ni aibu kila mwaka wa ubunge wabunge wanunua "mashangingi" ya mabilioni ya pesa. Sirikali inashindwa kununua mabasi kwa ajili ya wanafunzi school buses ambao miaka ijayo ndio watakuwa viongozi wetu inanisikitisha sana. Tunaelekea wapi hii nchi. Ikiwa hatuwezi kuwadhamini hawa watoto wadogo na kuwapa haki zao za msingi JE TUTAFIKA?? Mzee Makwaiya & Jenerali Ulimwengu wekeni hii mada ktk vipindi vyenu tuchangie.
 
Baadhi ya mabango yalisomeka SERKALI GANI HII, INAKABA MPAKA PENATI. MAISHA BORA KWA KILA FISADI

Na jingine

KIKWETE HUONI KUWA SERIKALI IMEKUSHINDA?

NAURI KUPANDA TOKA 50 MPAKA 100 KWA LIPI LILILOBORESHWA

SUBIRI KIHAMA CHAKO 2010

na mengine mengi.
 
baadhi ya mabango yalisomeka

SERKALI GANI HII, INAKABA MPAKA PENATI.
MAISHA BORA KWA KILA FISADI

Na jingine

KIKWETE HUONI KUWA SERIKALI IMEKUSHINDA?
NAURI KUPANDA TOKA 50 MPAKA 100 KWA LIPI LILILOBORESHWA
SUBIRI KIHAMA CHAKO 2010

na mengine mengi.
Will they be eligible to vote at that time? Iwish they do!
 
Jamani mi naona serikali ingetafuta ufumbuzi kuhusu usafiri wa wanafunzi, watoto wanashida sana.. mi nakaa kijichi, usafiri wa kwetu huko mpaka mbagala kwa asubuhi ni shughuli, utakuta wanafunzi saa kumi na moja na nusu anatembea kwa mguu toka mbagala rangi tatu mpaka mtongani na hapo hajui atapata usafiri saa ngapi wa kwenda shule, wakati mwingine unakuta mpaka saa tatu wapo stand kwanini wabunge wasione haya jamani kwanini matajiri wasijitoe kwa ajili ya hili badala ya kupoteza pesa zao kwenye mambo yasiyo ya msingi kwa Taifa letu.......... Mungu ibariki Tanzania
 
Maandamano haya yamefanyika jana Jijini DSM kwa wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi.

Ni nadra sana kusikia wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi wanaandamana kupinga kitu, je?huu ni mwanzo wa enzi mpya Tanzania?

Soma ujumbe wa Mabango yao ni mkali sana , kuna nini kinakuja?

Taarifa ya gazeti la mwananchi,.

Date::8/1/2008
Wanafunzi waandamana kupinga nauli mpya Dar
*Wataka mafisadi wafilisiwe fedha zikanunue magari

Kizitto Noya na Festo Polea

MAMIA ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam jana waliandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kupinga ongezeko la nauli yao kutoka Sh50 hadi Sh100.

Wanafunzi hao walihoji sababu za serikali kuwaongezea nauli wakati imeshindwa kuwafilisi watuhumiwa wa ufisadi na kutumia fedha walizoiba kununua magari kwa ajili yao.

Katika maandamano hayo yaliyoanza majira ya saa 5:00asubuhi wanafunzi hao wakiwa na mabango walipinga kulipa nauli hiyo na kushinikiza serikali iwakubalie waendelee kulipa Sh50.

Baadhi ya mabango yalisomeka: "Wafilisiwe Chenge, Mkapa, Karamagi na Yona tuletewe mabasi ya shule, J.K utawala umekushinda, Tulipe Sh100 kwa lipi uliloboresha?".

Mabango mengine yalisomeka: "Tumegundua Kandoro na askari wake pia mafisadi, Heri Makamba kuliko Kandoro, Bora Mkapa kuliko Jakaya na imekuaje hatuna kazi na tulipe Sh100 huku polisi wanapanda bure"
Mbali na mabango hayo wanafunzi hao walikuwa wakiimba nyingi za hamasa kulaani vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, wakidai kuwa ndivyo vinavyochangia ugumu wa maisha na kupanda kwa nauli.

Baadhi ya nyimbo hizo walizokuwa wanaimba zilikuwa zinasema: "Wawafilisi mafisadi watununulie magari, usiseme Tanzania, sema kaburi la Waafrika, mara kumi Makamba kuliko Kandoro...?"

Kwa zaidi ya nusu saa, polisi wa kawaida walikuwa wakisukumana na wanafunzi hao kuwazuia wasiingie lango kuu la ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambako walitaka kwenda kumwonyesha mabango yao na kumtaka atoe msimamo mbadala kuhusu nauli ya wanafunzi.

Vurugu hizo ziliwafanya askari hao kuomba msaada wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU), ndipo zaidi ya askari 30 wakiwa na rungu, bunduki mabomu ya machozi na gari la maji ya kuwasha waliwasili katika eneo hilo saa 5:57 asubuhi.

Hata hivyo askari hao ambao walionekana kujiandaa kupambana nao, waliofika katika eneo hilo kwa magari mengine matatu, hawakuweza kutumia silaha hizo wala kuwafukuza wanafunzi hao kwa nguvu baada ya kuona kuwa hawakuwa wamevunja amani.

Wanafunzi hao waliondoka kwenye lango kuu la ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuziba Barabara ya Kawawa huku wakiendelea kuimba na kunyanyua mabango yao jambo ambalo liliwapa kazi ya ziada askari hao.

Wakati wanafunzi hao wakiendelea kuimba na kuonyesha mabango yao nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa ambako kazi zilisimama , viongozi wao walikuwa ndani wakikutana na maafisa wa ofisi ya RC, kindo ambacho kilitafsiriwa na wanafunzi wenzao kuwa ni batili wakidai kuwa wana njama za kutaka kuwahujumu.

Zaidi ya mara tatu viongozi hao walitoka kwenye mkutano huo na kujaribu kuwatuliza wanafunzi wenzao, lakini ushauri wao ulionekana kugonga mwamba kwa sababu ya kukosa imani nao na kisha wakaamua wawachague wawakilishi wengine wa kuungana na viongozi hao katika mkutano huo.

"Wanafunzi mpo?," aliuliza Desemba Malaki mmoja wa viongozi hao na mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Ementi ya Kibamba.

"Tupo," walijibu kwa pamoja.

"Mkuu wa mkoa hayupo ofisini hivyo tunawaomba mrudi shuleni na sisi tunaendelea na mkutano na maafisa wake na makubaliano yoyote tutawangazia leo (jana) jioni kupitia vyombo vya habari," alisema

Nao wakamjibu kwa sauti ya juu: "Hatutoki hapa mpaka kieleweke".

Baada ya tangazo hilo lililotolewa kwa kipaza sauti cha FFU, viongozi hao na wawakilishi wa wanafunzi waliondoka kwa gari la polisi kuendelea na mkutano huo katika shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa.

Kuondoka kwa viongozi hao kuliibua upya fujo baada ya baadhi ya wanafunzi kudandia gari hilo huku wengine wakilizuia kuondoka, wakitaka tamko la kupunguzwa nauli litolewe hapo hapo.

Mpaka tunaondoka katika shule ya Benjamin Mkapa saa 7:00 mchana, mkutano huo ulikuwa haujaanza.

Awali akizungumza na gazeti na hili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Shule za Sekondari nchini (TASSA), Augustin Matefu, alisema maandamano ya wanafunzi hao sio sahihi kwani tayari mamlaka zinazohusika na nauli zimekubali kufanya mazungumzo nao na kutafuta uwezekano wa kupunguza nauli hizo.

"Sisi juzi (majuzi) jana (juzi) na leo (jana) tulikutana na Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kujadili suala hilo na tumekuja hapa kuwatuliza wenzetu. Mimi nasema sio sahihi kuandamana, kwani suala hilo liko kwenye mazungumzo," alisema.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alijaribu kuwasihi wanafunzi hao na kuwataka kuchagua viongozi iliwakazungumze na Sumatra kuhudu suala hilo, lakini haikusaidia.

Kwa upande wa Kamanda Kova, aliwataka wanafunzi waliounda umoja wa wanafunzi huo kufuata taratibu za maandamano ili waandamane.

“Wanafunzi wakifuata masharti waliyopewa sisi hatuna tatizo kwani kazi yetu ni kuwalinda, lakini sasa hatutoi kibali cha kuandamana, tunataka watimize masharti kwamba maandamano yao yatakuwa ya amani,” alisema Kova.
 
Haya maneno kama ni ya kwao wanafunzi msishangae utawala huu ukaangushwa na wanafunzi ,kama tawala nyingine duniani zilivyowahi kuangushwa na wanafunzi.
 
Safi Sana..., Hii inaonyesha Tanzania kumekucha...!

1. Taarifa kwamba nini big potatoes wanafanya zimefika mbali/zimewafikia wengi

2. Warithi wa nchi hii wameshagundua wakicheza na nyani wanaelekea kuvuna mabua
 
Ndo kizazi kijacho hicho mambo ya ndiyo mzee hayapo kwao. Ndo kizazi kitacholeta mabadiliko nchii hii. Hicho ndo kizazi kipya.
 
Ona wasivyo na hafu hata mbele ya silaha utadhani wamezaliwa Afganistan ama Irak.
 
Attachments

  • 2.JPG
    2.JPG
    66.5 KB · Views: 99
Ndo kizazi kijacho hicho mambo ya ndiyo mzee hayapo kwao. Ndo kizazi kitacholeta mabadiliko nchii hii. Hicho ndo kizazi kipya.
Umenena vyema mkulu, nadhani sasa ni wakati wa kufanya mpango liwepo somo la utawala bora mashuleni ili hiki kizazi kiamke na kufanya mambo inavyotakiwa.

Inatisha sana maana kitendo cha kubeba wazi mabango waliyobeba jijini Dar-Es-Salaam ni kitu cha kuwafedhehesha sana viongozi walioko madarakani. Hakuna aliyewahi kusema wazi tofauti na wale vijana waliomzomea Mkapa wakakamatwa kamatwa na fisi wengine wakapiga kelele bungeni ati mnamdhalilisha kongozi wetu.

Hapa lakini kuna mawili tofauti, kwanza wao wanaona Mkapa ni mzuri kuliko JK kwasababu bidha/nauli hazikupanda bei hovyo hovyo kama wakati huu. Lakini Mkapa alikuwa alikuwa mwizi anayejua namna ya kukamua na kumlisha ng'ombe aliyekuwa anakamuliwa. Sasa huyu bishoo JK hajui kufuga, yeye na makumbaf wenzake wanakamua tuu, hata wakiona ng'ombe amekonda wanakamua tuu, wakiona ng'ombe ameanguka nao wanaendelea tuu kukamua.

Hata Lowassa alipoona mambo yameharibika na kufikia kutimuliwa alikuwa kama fisi aliyefukuzwa kwenye mzoga, akavizia tena akapita na kunyofoa hapo kipande chap kisha kukimbia tena...??? Huu ni mkataba wa UV-CCM, ni sawa tu fisi aliyekwapua ingawa sina hakika alisaini kabla au baada ya kutimuliwa U-PM, ila nina hakika alishaona tatizo kubwa na naamini alishaanza kuandamwa sana kuhusu Richmond, bado akarukia UV-CCM..., huyu ni mtu kweli...???
 
Nani aliweza kuwakusanya wanafunzi hawa? hivi wakiamua kutoka barabarani wote kuna nguvu ya kuwazuia?

Tuepushe balaa hili kwani kama tumeweza kununua magari ya wafungwa inatushina nini kununua ya wanafunzi?
 
Attachments

  • 4.JPG
    4.JPG
    20.4 KB · Views: 101
Jamani mi naona serikali ingetafuta ufumbuzi kuhusu usafiri wa wanafunzi, watoto wanashida sana.. mi nakaa kijichi, usafiri wa kwetu huko mpaka mbagala kwa asubuhi ni shughuli, utakuta wanafunzi saa kumi na moja na nusu anatembea kwa mguu toka mbagala rangi tatu mpaka mtongani na hapo hajui atapata usafiri saa ngapi wa kwenda shule, wakati mwingine unakuta mpaka saa tatu wapo stand kwanini wabunge wasione haya jamani kwanini matajiri wasijitoe kwa ajili ya hili badala ya kupoteza pesa zao kwenye mambo yasiyo ya msingi kwa Taifa letu.......... Mungu ibariki Tanzania

waliojitolea magari yao yamevunjwa vioo, wafanyeje...?
 
Safi Sana..., Hii inaonyesha Tanzania kumekucha...!

1. Taarifa kwamba nini big potatoes wanafanya zimefika mbali/zimewafikia wengi

2. Warithi wa nchi hii wameshagundua wakicheza na nyani wanaelekea kuvuna mabua

Akilimtindi,

Big up kwa vijana hawa. Hakika pole pole we will get our country back
 
Attachments

  • 4.JPG
    4.JPG
    20.3 KB · Views: 101
  • DSC_0055.JPG
    DSC_0055.JPG
    24.1 KB · Views: 95
  • DSC_0092.JPG
    DSC_0092.JPG
    21 KB · Views: 108
1217658676_1web.gif

hivi hadi hawa watoto wamefikia kumkumbuka Nyerere na siyo Mwinyi waliyekua chini yake au Mkapa na kumruka kabisa Kikwete.. basi huko twendako siko.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom