Maandamano ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi

hivi hadi hawa watoto wamefikia kumkumbuka Nyerere na siyo Mwinyi waliyekua chini yake au Mkapa na kumruka kabisa Kikwete.. basi huko twendako siko.

Jibu langu kwa kifupi ni kwamba: Pamoja na failures kadhaa katika system ndani ya uongozi wake, Mwl. Nyerere ni ishara pekee ya kiongozi wa juu aliyeonekana kuipenda nchi yake na utaifa wake kupita viongozi wengine kama si wote katika ngazi hiyo hiyo waliofatia.
 
1217658676_1web.gif


hivi hadi hawa watoto wamefikia kumkumbuka Nyerere na siyo Mwinyi waliyekua chini yake au Mkapa na kumruka kabisa Kikwete.. basi huko twendako siko.

Mzee, ndiyo maana tunasema nchi ipo njia panda. Tatizo la viongozi wetu, wanaangalia mambo yaliyopo na namna ya kujipatia kura uchaguzi ujao siyo masuala ya kujenga taifa. Mtazamo na jitihada za Mwl. Nyerere ilikuwa ni kujenga vijana/watoto wawe na mtazamo wa usawa na kujitegemea.

Marais waliomfuata hawana mpango juu ya hali ya baadaye ya watoto/vijana. Hata hii hali ya maandamano ya vijana hawa tena wakiwa na mabango yanayosema Chenge, Rostam, Mramba, Mkapa wafilisiwe ili wapate nauli, unaweza ukaona namna hali ilivyo ngumu unapofikiria miaka ijayo.
 
Dah vijana wananikumbusha enzi zangu, pale Aza boy!

ningekuwa bongo ningekurupua uniform zangu za kale, ili kuonesha mshikamano nao.
nauli jiti, hataaa, haikubaliki!!, besides kama nauli jiti hela ya kununua mhogo wa kukaanga itatoka wapi?(naongea kwa experience yangu pale dsm), halafu hapo baadhi ya madenti mfano mzuri wana aza boy, hawajapiga ruti kwenda tuition, mwenge, magomeni , ubungo ,n.k,halafu wapande tena daladala kurudi home!!, hiyo hela yote wataafford vipi wakati kazi hawana?.
 
jibu Langu Kwa Kifupi Ni Kwamba: Pamoja Na Failures Kadhaa Katika System Ndani Ya Uongozi Wake, Mwl. Nyerere Ni Ishara Pekee Ya Kiongozi Wa Juu Aliyeonekana Kuipenda Nchi Yake Na Utaifa Wake Kupita Viongozi Wengine Kama Si Wote Katika Ngazi Hiyo Hiyo Waliofatia.
nyerere Bado Anabaki Juu....!
 
Watoto ndio walileta haki za kiraia yuesei walipoandamana pamoja na dakta king na ndio walioleta mabadiliko sauzi walipoandamana sharpeville poa ndio wataleta mapinduzi Tz!
 
Wanafunzi kuandamana tena Jumatano


BAADHI ya wanafunzi walioandamana wamesisitiza kuwa wataendelea kuandamana hadi pale Serikali itakaposikiliza kilio chao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa Chama cha Wanafunzi wa Sekondari Tanzania (TASSA Bw. Agustino Matefu alisema kuwa wameiandikia barua Serikali kuhusu kupunguziwa nauli na kuipa siku mbili kutoa majibu ambapo wasipojibiwa wataandamana nchi mzima bsiku ya jumatano.

Wakizungumza na Majira Jumapili jana Dar es Salaam, wanafunzi vwengine walisema kuandamana kwao juzi kupinga nauli mpya ya sh. 100 si mwisho bali ni mwanzo wa kuendelea kudai haki yao ya msingi.

Walisema inasikitisha kuona wanafunzi wakipandishiwa nauli wakati Serikali inajua wazi wao hawafanyi kazi yoyote.

"Sisi tutaendelea kundamana hata kama watakuwa wakitumwagia maji ya kuwasha na kutupiga mabomu ya machozi, ipo siku haki yetu itapatikana,"alisema mwanafunzi aliyejitambilisha kwa jina moja la Idd.

Alisema kusitishwa kwa maandamano hayo juzi haina maana wameshindwa kuyaendeleza, bali wanasubiri majibu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Kandoro ambaye walifika ofisini kwake lakini hawakufanikiwa kumkuta.

Alisema wapo baadhi ya wanafunzi wamemua kuacha maandamano baada ya kupigwa na baadhi ya askari waliokuwa wakiwazuia lakini hiyo haiwazui wao kuendelea kuandamana na kudai haki yao.

Hata hivyo wakati wanafunzi hao wakipanga mikakati ya kundamana tena Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) jana walikutana kwa kikao cha dharura ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia kusikiliza kinachojadiliwa.

Wakati huo huo baadhi ya wazazi wameunga mkono maandamano hayo yaliyofanywa na wanafunzi na kuitaka Serikali kuangalia upya suala la kupandisha nauli ya wanafunzi.

Bibi Rehema Juma mkazi wa Tandika jijini alisema hakukuwa na sababu kwa SUMATRA kupandisha nauli ya wanafunzi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kuwatwisha mzigo wazazi.

Aliongeza kuwa yeye alitegemea nauli itabaki kuwa sh. 50 kwakuwa kuna kundi kubwa la askari ambao walikuwa hawalipi nauli na sasa wameamriwa kulipa na kufidia pengo la nauli ya wanafunzi.

Mkazi mwingine wa Airport Bi. Grace Gurisha, alitofautiana na wenzake na kusema maandamano hayo hayakupata kibali ndio maana kuna baadhi ya wanafunzi katika shule nyingine hawakufika kabisa.

"Mimi kama mzazi nina haki ya kulalamikia suala la nauli kupanda kwa wanafunzi... lakini watoto wetu utaratibu walioutumia sio sahihi na inaonyesha jinsi gani wasivyo na adabu" alisema Bi. Gurisha.

Naye Mkazi wa Sinza Kijiweni, Bw. Thomas Dominick, alielezea jinsi wanafunzi hao wanavyopata misukosuko ya usafiri kwa kulipia kiasi cha shilingi 50 na kusema kuwa huenda kiasi kilichoongezwa kinaweza kuwapunguzia manyanyaso ya kugombania usafiri.

Kwa upande wa Bw. Matiko Musubi ambaye ni mfanyabiashara wa Ubungo-Terminal alieleza kwamba wanafunzi hao walikuwa wakifikisha kilio chao kwa viongozi wa Serikali na kusema kuwa walikuwa na hoja za msingi. Habari hii imeandikwa na Said Mwishehe, Prosper Mosha, Flora Amon na Frida Ally.
 
Kama hali imefika hapo ujumbe ulivyopekwa na wanafunzi, basi hii ni ishara wazi kuwa huu utawala umefika ukingoni sasa.
 
baadhi ya mabango yalisomeka

SERKALI GANI HII, INAKABA MPAKA PENATI.
MAISHA BORA KWA KILA FISADI

Na jingine


KIKWETE HUONI KUWA SERIKALI IMEKUSHINDA?
NAURI KUPANDA TOKA 50 MPAKA 100 KWA LIPI LILILOBORESHWA
SUBIRI KIHAMA CHAKO 2010

na mengine mengi.


Nikweli, kiama cha sisiem ya mafisaad na serikali yake ni 2010. Hata wao wamelifahamu hilo na ndio maana sisiem mkoa wa dar wameamua kutoa tamko la kuwaunga mkono hawa vijana, kwani wanaona ni tishio kubwa 2010. Kumbuka kwamba wengi wa hawa vijana ni wapigakura wazuri 2010. HAPO NDO KIAMA CHA CCM NA MAFISADI KINAONEKANA WAZIWAZI!
 
Dah vijana wananikumbusha enzi zangu, pale Aza boy!

ningekuwa bongo ningekurupua uniform zangu za kale, ili kuonesha mshikamano nao.
nauli jiti, hataaa, haikubaliki!!, besides kama nauli jiti hela ya kununua mhogo wa kukaanga itatoka wapi?(naongea kwa experience yangu pale dsm), halafu hapo baadhi ya madenti mfano mzuri wana aza boy, hawajapiga ruti kwenda tuition, mwenge, magomeni , ubungo ,n.k,halafu wapande tena daladala kurudi home!!, hiyo hela yote wataafford vipi wakati kazi hawana?.



Mkuu gamba la nyoka,

Umenishangaza sana ulipolinganisha haya maandamano tukufu na yenye tija ya hawa vijana na yale ya enzi zako! Maandamano ya vijana yamebeba na kutuma ujumbe mzito kwa watawala wakuu na mafisadi wa nchi, wakati yale ya enzi zako yalifanyika tu pale mlipopikiwa chakula kibovu!

Maandamano ya vijana yanajenga utamaduni wa umoja wa watz kutetea haki zao za msingi zilizobakwa na viongozi na mafisadi wa nchi, wakati yale ya wakati wenu yalilenga kutatua matatizo ya muda mfupi shuleni kwenu!

Kwa kifupi ni kwamba maandamano ya vijana hayawezi kufananishwa na maandamano yoyote yaliyowahi kutokea hapo tz. Hawa ni vijana shupavu walioamua kuungana na kupambana na serikali yao waziwazi. Wameungana bila kujali tofauti za itikadi za wazazi wao na chimbuko lao.

Hawa ndio viongozi shupavu wa kesho na ndio watakaowaongoza watanzania kuifikia ile nchi ya maziwa na asali; nchi ya maisha bora kwa kila mtanzania!

Na kama serikali itapuuzia madai ya hawa vijana, basi 2010 ITAGEUKA KUWA KIAMA CHA SISIEMU NA MAFISADI!

Hongera vijana kwa ujumbe wenu uliotukuka. Mungu awabariki.
 
Quote:
Originally Posted by kiranja

Nao wakamjibu kwa sauti ya juu: "Hatutoki hapa mpaka kieleweke".

Haya ndiyo maneno ya VIJANA walioanza MABADILIKO huko Ufaransa mwama sijui arobaini na ngapi. Walipozuiliwa, walifanya mkutano ndani ya meli kwenda GREECE? na hadi waliporudi Ufaransa, walikuwa wameshaiva. Wakaanza VUNJA VUNJA kali sana. Hii iliendelea hadi miaka ya 70 kwa wale vijana waliokuwa wanavalia SOX za rangirangi na VICHUPI. Uholanzi ni WAVUTA bangi na vijana waliopelekea FUJO kubwa sana na kulazimisha mabadiliko ambayo yameifikisha hapo UHOLANZI ilipo. Kwa mawazo yangu mimi si VIONGOZI wa SERIKALI tu inabidi waangalie ila VIONGOZI WA DINI PIA. Kama kweli viongozi wa DINI mnataka kibarua kiwepo basi ENDELEZI MAPIGANO nyie wenyewe. Mkisubiri vijana wapigane peke yao, hawa vijana huwa WAPINZANI sana wa MILA NA TAMADUNI zote zilizowafikisha hapo walipo. Wakiimaliza CCM, nyie mjue mtafuata. Watavunja MAKANISA na MISIKITI na MAHEKALU yote. Hii ilitokea nchi nyingi kama Czeck-Slovakia. Uholanzi huko ni kama vile hamna dini. Ukiona dini ni WATU WA KUJA.
Katika yote haya nashindwa kujua VIONGOZI WA UPINZANI HUWA WANAKUWA WAPI? Kazi ya vyama vya UPINZANI ni hii. Walitakuwa kuwa BEGA KWA BEGA na wanafunzi.
Kwa nchi za AFRICA ilishawahi kutokea huo GHANA. Huyu General Rawlings aliingia kwa msaada wa FUJO na MAANDAMANO ya WANAFUNZI. Nawapa hongera vijana wetu. Lazima TUKIRI kuwa sisi KAKA/DADA zao, BABA/MAMA zao, BIBI/BABU zao kwa kweli tumewafikisha PABAYA. Tumekuwa KONDOO wee, hadi MUIRAN anatutia KIDOLE. Na anakutia KIDOLE na KESHO unakwenda kunua GAZETI LA RAI, ama VODA. Sijui hapo unakuwa unafikiri au hufikiri. Mie Milele sintanunua CHOCHOTE kilicho na mahusiano na RA. Nafikiri utakuwa MUUNGANO wangu pekee kwa vijana. Sijui wewe.
 
Jamani imenisikitisha sana tumefikia huku? Serikali haina hata huruma kwa watoto wake?.. wataipata wapi huruma wakati watoto wa wakubwa wanapelekwa shuleni na mashangingi ( kama wanasoma nchini).

Eti walipe shilingi 100 and then wakalie siti... Hivi aliyetoa kauli hii anayo akili kweli??? makonda watakubali kweli ......... yaani nalia peke yangu
 
Jamani imenisikitisha sana tumefikia huku? Serikali haina hata huruma kwa watoto wake?.. wataipata wapi huruma wakati watoto wa wakubwa wanapelekwa shuleni na mashangingi ( kama wanasoma nchini).

Eti walipe shilingi 100 and then wakalie siti... Hivi aliyetoa kauli hii anayo akili kweli??? makonda watakubali kweli ......... yaani nalia peke yangu


Mkuu MwanajamiiOne,

Kama ulimsikiliza vizuri huyo mkulu wa mkoo wa dar, utagundua kwamaba hakuwa na point. Huwezi ukawatangazia wanafunzi kuwa wanahaki ya kukalia viti vya daladala halafu hapohapo ukawaonya wasivikalie kama kuna mkubwa wao kiumri aliyesimama ndani ya daladala!

Ukweli ni kwamba, daladala za dar huwa zinajaza watu na muda wote huwa kuna watu wazima ambao husimama mwanzo hadi mwisho wa safari siku zote za wiki. Sasa huyo mkulu wa mkoao wa dar anapowambia wanafunzi wanahaki ya kukalia viti, halafu hapohapo anawambia waachie viti wakiona wakubwa zao wamesimama anamaana gani?! Wanafunzi wakitekeleza hayo maneno ya mkulu watapata wapi viti vilivyowazi ikiwa hata hao watu wazima huwa wanalazimika kusimama muda wote kwa kukosa viti?! Hivi ni kweli kwamba madai ya wanafunzi yalikuwa ni 'kukalia viti' ndani ya daladala?! Au ni punguzo la nauli ya sasa sh. 100 iwe 50?! Kwanini hawa viongozi hawataki kuwa wakweli?! Au waliwatishia hawa wawakilishi wa wanafunzi kiasi cha kushindwa kudai madai yao yaliyowafanya wagome?! Au waliwahonga ili waseme madai yao yalikuwa ni kukaa kwenye viti ndani ya daladala na si kupunguziwa au kufutiwa kabisa nauli ya daladala?! Sielewi nia ya huyu mkulu!

Nionavo mimi: Kwa vile hawa vijana hawana kipato chochote iwe kwa siku au kwa mwezi, napendekeza wasilipe nauli yoyote na badala yake serikali ibebe mzigo wa hawa wanafunzi kwa njia moja au nyingine kwani ina pesa nyingi za kuchezea. Kama serikali haina pesa za kuchezea mbona mafisadi wa epa wamechota pesa nyingi na haiwafanyi lolote?! Kwanini isiwakamate na kuwashitaki hao mafisadi ili warudishe pesa zetu zitumike kununua magari/mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri kwa wanafunzi?! Tutaendelea kuchezewa akili mpaka lini?! Muda umefika wa kuhoji haya waziwazi na wahusika watupatie majibu yenye tija.
 
Tatizo ni kwamba siku hizi viongozi wetu hawajui ama hawatilii maanani uzito wa shida wanazopata wananchi ama wanateseka kiasi gani kutokana na kupanda kwa gharama za maisha. Akina sie wapanda daladala tunaelewa wazi kwamba makondakta wasiofuata utaratibu watawakandamiza abiria wasioelewa kwa kuwatoza nauli iliyo juu kama walivyokuwa wakifanya kwa muda mrefu hata kabla nauli mpya hazijatangazwa. Kutangazwa kwa nauli mpya ilikuwa ni kuhalalisha tu kile ambacho tayari kilikuwa kikiendelea.

Kuhusu nauli ya Sh. 100 kwa wanafunzi, jana kwenye daladala, abiria walimuuliza kondakta mmoja maoni yake. Je, alikuwa anaona ni sahihi wanafunzi kutozwa Sh. 100 badala ya 50. Kondakta yule akakiri kwamba kuwalipisha wanafunzi sh. 100 si sahihi. Sh. 50 ilikuwa inatosha. Akasema, nauli ya Sh. 300 wanayotozwa watu kwa safari fupi fupi inatosha kabisa kufidia, maana pamoja na kupanda kwa nauli, bado wale wasioweza ama wasiotaka kutembea wanaendelea kupanda daladala kwa safari fupi, mradi mtu awe na 300 yake.

Mkuu wa Mkoa akizungumza alisema kwamba nauli mpya zimepitishwa kisheria na wanafunzi watalipa nauli ya Sh. 100 iliyopangwa. Nikaamini kwamba viongozi wetu siku hizi hawako katika kusikiliza, kuchunguza, kuelewa na kuwasaidia wananchi katika matatizo yanayowakabili. Nilidhani Kandoro angelikuwa upande zaidi wa wanafunzi. Tatizo lililopo ni la msingi, kwamba wanafunzi kulipa sh. 100 ni mzigo mwingine kwa wazazi ambao tayari wanaumia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha k.m. bei ya chakula na bidhaa zingine muhimu.

Haki ya kukaa kitini inamsaidia vipi mwanafunzi? Leo nilipoingia kwenye daladala nimeshuhudia wanafunzi kabla bus halijajaa walikuwa wameketi kwenye viti, walipoingia watu wazima vijana wale bila kuambiwa na mtu walinyanyuka na kuwapisha wakubwa waketi. Haki yao kisheria ya kuketi iko wapi?

Nadhani hapa tuna tatizo kubwa ambalo linatokana na ukweli kwamba si Kandoro, Selesi, Kova, wala watoto wao wamewahi kupanda daladala na kuelewa mazingira ya hayo mambo waliyoyajadili hadi kufikia makubaliano kwamba kumlipisha mwanafunzi nauli ya Sh. 100 ni halali, na kutoa haki ya kuketi. Inashangaza kuona kiongozi anayepaswa kuwatumikia wananchi anaridhika kirahisi na maamuzi yanayozidi kuwakandamiza wananchi, kwa manufaa ya wafanyabiashara! Kondakta wa daladala anaelewa kabisa kwamba nauli ya Sh. 100 kwa wanafunzi si ya lazima. Kandoro na wenzake hawajui hilo.

Nawapongeza vijana waliobeba picha ya Mwalimu Nyerere! Nakumbuka enzi hizo wakati Mwalimu anajaribu kujenga Ujamaa na Kujitegemea nchini (Ryoba kwenye makala zake ndani ya gazeti la Raia Mwema anazungumzia sana umuhimu na uzuri wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea). Enzi hizo, ulikuwepo uhaba wa vitu kadha wa kadha, Mwalimu na viongozi wengine wa aina ya Sokoine, walisikiliza, walifuatilia na kujaribu kutafuta ufumbuzi kwa manufaa ya wananchi. Yasemekana Mwalimu aliwahi kupanga foleni katika duka moja pale karibu na Fire Brigade ili kuona na kujiridhisha na jinsi zoezi la uuzaji wa bidhaa adimu lilivyokuwa likiendeshwa, bila kuwepo upendeleo. Waliokiuka utaratibu uliowekwa walikiona cha mtema kuni. Huo ni mfano tu wa jinsi ambavyo Mwalimu alikuwa akijali sana shida za wananchi aliokuwa akiwaongoza na kuwatetea dhidi ya wafanyabiashara. Bila shaka vijana hao walioamua kubeba picha ya Mwalimu wamekuwa wakisimuliwa na baba na mama zao kama si babu na bibi zao jinsi Mwalimu alivyokuwa akiwahurumia wananchi wake!

Mtoto akilia bila sababu ya msingi tunachukulia kwamba ni utoto unamsumbua. Watu wazima wakilia inabidi wasikilizwe, ijulikane kilio chao ni cha nini, na itafutwe njia ya kuwasaidia. Wananchi wanapolalamika inabidi Serikali iwasikilize, na ijue kwamba kuna tatizo na kwamba wananchi wanahitaji msaada wa Serikali, vinginevyo wataendelea kupunguza imani kwa Serikali yao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom