Uchaguzi 2020 Maandamano ya tarehe 2 Nov: Je, Ni Demokrasia au waliokosa wanapigania Maslahi Binafsi?

Sasa hivi wamebakia kusubiri matamko mbalimbali, kama chanzo cha faraja kwao..!
Sasa mtu kama Tundu Lissu yupo nchini kwake lakini anashinda kutwa nzima anaomba misaada ya kimataifa ije kuiadhibu serikali. Mbaya zaidi watu wengi wamemchunia kama hawamuoni au kumsikiliza, this is Tragedly kwa kweli. Yaani anadhani akitutajia Mahakama ya ICC ndiyo tutaogopaaa.
 
Watanzania wameamua kwenda na John Pombe Magufuli
Watuache tupumue
Watu milioni 12 ndiyo watanzania milioni 45!!!!!!😂😂😂😂. Tena hiyo milioni 12 mmebebwa na tume yenu mliyoiajiri, polisi, jeshi, katiba ya upendeleo, sheria kandamizi na watu wasiojulikana!!!!
 
Sasa mtu kama Tundu Lissu yupo nchini kwake lakini anashinda kutwa nzima anaomba misaada ya kimataifa ije kuiadhibu serikali. Mbaya zaidi watu wengi wamemchunia kama hawamuoni au kumsikiliza, this is Tragedly kwa kweli. Yaani anadhani akitutajia Mahakama ya ICC ndiyo tutaogopaaa.
Kuiadhibu CCM siyo serikali tofautisha serikali na chama chenu, chama chenu kitaenda serikali itabaki na nchi itabaki, chama chenu siyo kila kitu nchi hii
 
Tarehe 31 Oktoba tumeshuhudia kuitishwa kikao cha waliokosa nafasi mbalimbali za ubunge na urais ili kutangaza kufanya maandamano siku ya tarehe 2/11/2020. Tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, vyama vya upinzani havijawahi kukubaliana na matokeo katika kila sehemu walizoshindwa. Kwa miaka ya nyuma viongozi wa juu wa vyama vya CHADEMA, CUF na ACT-Wazalendo walizoea kushinda na kurudhika na matokeo huku wakisaini malipo ya mishahara na posho za ubunge kila mwezi bila kujali majimbo ambayo wengine walipoteza katika vyama vyao.

Sote tunafahamu kuanguka kwa wenyeviti wa vyama kama Zitto Kabwe na Freeman Mbowe kumekuwa na mshtuko kwa watanzania kutokana na umaarufu na umashuhuri walionao kwa taifa lakini sio suala linalowashangaza wapiga kura katika majimbo yao kutokana na hali ya ushawishi wao ilivyopungua huko majimboni.

Suala tunalotakiwa kujiuliza juu ya uamuzi wa kuandamana, Je! Tunaandamana kwa lengo la kutafuta demokrasia au tunatumia kivuli cha demokrasia kutetea maslahi binafsi ya viongozi wa vyama vilivyoanguka? Ni kwa nini picha za mauaji yaaliyotokea nchi nyingine zitumike kuidanganya umma wa watanzania na jumuia za kimataifa kuwa mauaji haya yanatokea Tanzania? Majibu ya maswali haya yanatupekea kuamini kuwa nia si demokrasia bali ni maslahi binafsi.

Tukumbashane tu nchi ya Marekani na Kenya ndizo zimekuwa vinara wa ufutiliaji na ukosoaji wa uchaguzi huu. Taasisi kama FICHUA TANZANIA na TANZANIA ELECTION WATCH zimeonyesha kuwa na usajili kutoka serikali ya Kenya na ndizo zimekuwa zikiongoza mashambulizi dhidi ya ushindi wa CCM.

Sababu kubwa ambayo watanzania wanatakiwa kuielewa ni maslahi binafsi ya nchi kama Kenya na USA. Itambulike kwamba kuna vita kubwa kiuchumi na watu hawa wanaopanga kuandamana wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu ili kuuza nchi yetu kwa ajili ya uchu wa madaraka na maslahi binafsi kwani wamekuwa wakipokea fedha nyingi ili kufanikisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii. Kwa muda wa miaka mitano, Tanzania chini ya uongozi wa Magufuli, imeshuhudia mtazamo wa nchi kujitegemea kiviwanda na mikakati ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda imekuwa sumu kwa taifa la Kenya kwa sababu Tanzania imekuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa kutoka Kenya. Uwekezaji wa viwanda Tanzania ni mwiba kwa viwanda vya nchi hiyo.

Kwa upande wa Marekani (USA), sera ya demokrasia hutumika kama njia ya kuingilia kwenye nchi nyingi lakini kwa undani huwa ni maslahi ya kiuchumi na uwezo wa kutawala nchi za Africa. Suala kubwa ni kuvunjwa kwa mkataba mbovu wa SYMBION chini ya utawala wa Dr. John Magufuli. Hali hii imepelekea USA, kupiitia Balozi wake nchini Tanzania Dr. Donald J. Wright, kutumia mwamvuli wa demokrasia kuchafua serikali ya Tanzania baada ya kufuta mkataba huo. Katika mkataba huu tuliibiwa zaidi ya bilioni 6 kila mwezi na kuuziwa umeme kwa gharama kubwa sana. Watu kama MANGE KIMAMBI kupitia account za mitandao ya kijamii wa INSTAGRAM na GOODLUCK HAULE, KIGOGO2014, FATMA_KARUME, HILDERNEWTON21, JJMNYIKA kupitia account ya TWITTER ndio wamekuwa wakitumiwa sana kuhakikisha wanaharibu amani na kuchafua jina la Tanzania ndani na nje ya nchi.

Ikumbukwe kuwa vurugu za nchini Libya zilianza kwa maandamo ya kile kilichotajwa demokrasia lakini baadae mataifa makubwa yakiongozwa na marekani yalivamia kijeshi kupitia nafasi ya vurugu zilizoanzishwa na walibya wenyewe. Muda mfupi baadaye, uzalishaji wa mafuta ulishuka kwa kasi kutoka katika nchi iliyokuwa na hazina kubwa ya mafuta Africa na kuifanya nchi yenye uchumi unaosuasua ukiambatana na vita kabla ya Marekani kurudi na kukiri kufanya makosa katika uvamizi huku wakiiacha nchi wa Libya ikiendelea kuangamia kutokana na madhara ya vita hivyo.

Hali itakuwa hivyo Tanzania endapo tutawafuata wanaotaka kuandamana kwa maslahi binafsi.

Ukisikiliza kampeni zilivyokuwa zikiendeshwa kwa upande wa vyama vya upinzani, mtakubaliana na mimi kuwa mgombea wa CHADEMA alipanga kuandaa maandamano kwa kuwa alijua hawezi kushinda. Mara kadhaa amekuwa akihubiri kuwa iwe kwa amani au kwa vita anataka kushinda uchaguzi huu.

Hii iliashiria malengo ya kuharibu amani tangu siku ya kwanza. Ikumbukwe tu katika mpango huu, hata kama Jeshi halitaingilia kati, Vikundi maalumu vya CHADEMA na ACT-Wazalendo vimeandaliwa ili kuanzisha vurugu na kuwapiga waandamanaji wenzao ili kuonyesha jamii ya kimataifa kuwa Tanzania kuna vurugu. Tuepuke hili kwa nguvu zote ili kuondoa maslahi binafsi ya Freeman Mbowe, Maalim Seif, Tundu Lissu na Zitto kabwe.

Ifahamike tu kuwa Robert Amsterdam, mwanasheria na wakili wa Tundu Lissu, ambaye kwa sasa yupo Uturuki baada ya kuondoka aliwekwa kwa ajili ya kuhakikisha anafanikisha zoezi la kuleta vurugu na kuiacha Tanzania katika mazingira ya sintofahamu kabla ya mataifa makubwa kuingia na kuiba mali za nchi hii kupitia vita.

Niwapongeze watanzania kwa kutokubaliana na mkakati huu wa mataifa makubwa. Niwakumbushe tu huu ni wakati wa kuwaonyesha mabeberu namna watanzania tulivyo na umoja na tunavyoweza kuamua masuala yetu wenyewe bila kuwategemea wao ambao wanatuletea masharti ya ushoga na kutuibia malighafi kwa kigezo cha kupigania demokrasia.
Rubbish, maslahi binafsi si wamedhulumiwa? Nani hayupo Kwa maslahi binafsi, tumeweka utaratibu wa kura lazima ufuatwe
 
Rubbish, maslahi binafsi si wamedhulumiwa? Nani hayupo Kwa maslahi binafsi, tumeweka utaratibu wa kura lazima ufuatwe
Ni wazi JPM ni mtu ambaye hayuko kwa maslahi binafsi maana tunaona ni namna gani anavyoumiza kichwa kila siku ili kuhakikisha nchi inakuwa salama na inafanikiwa.
 
Watu milioni 12 ndiyo watanzania milioni 45!!!!!!😂😂😂😂. Tena hiyo milioni 12 mmebebwa na tume yenu mliyoiajiri, polisi, jeshi, katiba ya upendeleo, sheria kandamizi na watu wasiojulikana!!!!
Watu 45M wangekua wameonewa maandamano yao yasingezuilika na yoyote
Watanzania wameamua kwenda na John Pombe Magufuli
 
N
Kuiadhibu CCM siyo serikali tofautisha serikali na chama chenu, chama chenu kitaenda serikali itabaki na nchi itabaki, chama chenu siyo kila kitu nchi hii
Ni sawa, nakubaliana na wewe...na nadiriki kusema wazi kuwa ..."Nchi ni zaidi ya Chama cha siasa" Ni nchi kwanza na vyama baadaye. Kutanguliza nchi mbele kabla au kuliko maslahi ya chama ni jambo la kwanza na la muhimu zaidi. Lakini tukumbuke Chama kilichoshinda uchaguzi ndicho kinaweza kuifanya nchi iwe na maendeleo. Na hapo kwenye chama gani na chama gani ndipo panapoanzia kwenye IDEOLOGY ya chama, ILANI ya chama fulani inasemaje! Ndiyo maana watu wakakaa na kusikiliza kwa makini ILANI ya CCM na CHADEMA na ACT , wakaona wazi ILANI ya CCM inaeleweka zaidi kuliko za vyama vingine. Huwezi kuwa na ILANI iansema ushoga ni halali, au kuweka madini rehani, halafu utegemee tutakuchagua, kwa misingi gani? Mtu yupo supported na Ma Activists wa mtandaoni ambao kwenye foleni ya kupiga kura huwaoni ila wanashoindwa kutwa kucha wanabwabwaja tu na kutukana viongozi. Kuna kila haja ya vyama pionzani kujitathimini sana sana sana sana.
 
Utumwa hauwezi kuisha si unaona Amsterdam anavyotuingilia sie tunamuona shujaa
Huyo Robert Amsterdam kama anajiamini akanyage bongo land aone tutakavyomyoosha kwanza, na hao akina Jeff.

Watanzania tumeshaamua n atunachokitaka kwa sasa ni kuona utulivu na kazi za kujenga taifa zinaendelea.
 
Sasa mtu kama Tundu Lissu yupo nchini kwake lakini anashinda kutwa nzima anaomba misaada ya kimataifa ije kuiadhibu serikali. Mbaya zaidi watu wengi wamemchunia kama hawamuoni au kumsikiliza, this is Tragedly kwa kweli. Yaani anadhani akitutajia Mahakama ya ICC ndiyo tutaogopaaa.
Hiyo mahakama siku hizi haina mashiko tena kama zamani,watu washaiona kama mahakama ya mwanzo tu.

Inamaana kwakuwa wao wameshindwa,ndio kigezo cha uchaguzi huu kuwa na some irregularities?
 
Hakuna anayeweza zuia maandamano ya amani maana huwa kama mafuriko, wala hayo ya kuwalipa vijana wafanye uharibifu kwa kisingizio cha haki na demokrasio hatuwezi kuyaita maandamano
Labda kwanza tufahamu maana halisia ya maandamano, ndio tuendelee kujadili.
Halafu taarifa za polisi kuwa maandamano yangekuwa ya kihuni, sio kweli 'Hollywood', 'Bollywood', na 'Nollywood'?
 
Back
Top Bottom