Maandamano ya TANESCO yawe mwanzo wa kuacha 'KULALAMIKA' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya TANESCO yawe mwanzo wa kuacha 'KULALAMIKA'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lukindo, Oct 26, 2011.

 1. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,070
  Trophy Points: 280
  Habari ya kazi wanajamvi,

  Naomba kuwaleteeni mawazo yangu ni jinsi gani tunaweza kumjibu waziri aliyesimama juzi na kutuambia hakuna mgao mpaka February lakini sasa ninaandika hii thread kwa generator. Pia kurespond juu ya ufisadi unaoiangamiza nchi hii ambayo watawala wanashindwa hata kuitaja jina!

  Niliona juma lililopita wafanyakazi wa Tanesco wakikubaliana katika mkutano wao halali kuwa wataandamana nchi nzima kushinikiza DOWANS isilipwe.
  Hili lilikuwa ni wazo zuri na unaweza kuwa mwanzo wa Tanzania mpya ukichukulia kuwa sasa hivi kila Mtanzania ana hasira na maamuzi yanayoendelea hapa nchini na wote tunasubiria kuwa ni wapi tunaweza kuanzia 'kuwavuruga' hawa watu ambao wamevuruga nchi.
  Lengo likiwa ni wapi pa kuanzia kuwawajibisha hawa watawala wasiowajibika.

  My take:
  Kwa vile kila maandamano yaliyoanzishwa na cdm, cuf, tawla, nk yameonekana kama aina ya uchochezi wa kisiasa, napendekeza hizi taasisi zitumie maandamano haya ya TANESCO (kwa kuwaunga mkono) kuhamasisha wananchi kuwasupport ili yawe na matokeo mazuri. Ninachojua, endapo Watanzania (Waliochoshwa na ufisadi tu) watajitokeza kwa wingi kuwaunga mkono TANESCO nchi nzima inaweza kuwa na mwangwi mzuri kwa hawa watawala waliojisahau.

  Pia waandaaji wa maandamano haya (TANESCO) wachukulie hili wazo kama lenye nia nzuri na wafanye maandalizi mazuri tu kwa kuto mawasiliano (instant communication) mazuri kwa watakaotaka kuwaunga mkono. Wanaweza kufungua internet blog (facebook, jf, twiter nk) na kutoa namba za simu kwa ajili ya instructions ya je yatakuwa lini, sehemu tutakazo kusanyika, njia, ajenda nk

  Endapo hili likifanikiwa litasaidia Watanzania kuacha kulalamika lalamika bila kufanya chochote kutatua matatizo yao. Mwenye mawazo tofauti, tafadhali yalete.

  Nawakilisha
   
Loading...