Maandamano ya Kupinga Ufisadi

wengi tutajitokeza mtaani siku hiyo kama ni kweli. tumechoshwa na ufisadi tz. watu wako tayari kwa lolote. selikali inabidi iwe makini sana. siku hata jiwe tu likanza kurushwa hapa bongo, nakwambia watu watarusha hadi funguo zao, alimradi tu hasira zao zilizojaa mioyoni mwao ziwatoke. tumechoka jamani.
 
Uzuri wa TZ wananchi wanajua kuandamana kuunga mkono. Haya mambo ya kuandamna kulaani au kupinga wao hawajui. Sasa usije shangaa wanajisahau na kuandamana kuunga mkono MAFISADI!!!!!!!!!!!!
 
Uzuri wa TZ wananchi wanajua kuandamana kuunga mkono. Haya mambo ya kuandamna kulaani au kupinga wao hawajui. Sasa usije shangaa wanajisahau na kuandamana kuunga mkono MAFISADI!!!!!!!!!!!!

ha! ha! angalizo zuri kaka!
 
kweli manji mwaka huu tunaye. kama watu wanajua kuandamana kusapoti vitu, kuna siku utawaona watz kuwa wanajua kuandamana kufukuza wezi. siku hiyo ipo tena inakuja.
 
Hivi wewe uliona lini kufanywa maandamano.

haya kaka! kama ni lugha imekosewa ivuke halafu ukate issue, lengo hapa ni kuangalia jinsi gani wananchi maoni na mitizamo yao juu ya ufisadi iwe sauti maja na kuifisha kwa serikali. Ni hilo tu kaka!
 
what will be an ideally time for maandamano! what conditions should we look for before organizing? what form of alliances do we need?
 
Brilliant idea, tupo tayari. Kama wananchi hawa waliohongwa na kuwapa ushindi wa kishindo wakiandamana, nadhani itakuwa ni meseji nzuri sana kwa hawa mamwinyi wanaodhani kuwa wao watatawala milele, na kwamba katika milioni 40 ya watz hakuna watu wenye uwezo wa kulipeleka hili taifa kwenye mstari sahihi kuliko wao. Let's tell them, we need a better Tanzania, and we can do tht without them.
 
Nafikiri ipo haja ya kuonana na viongozi wa CUF kwani wanayo historia ya kuvunja katiba kwa kufanya maandamano ,Nchi nzima na walifanikiwa kufika pale walipokusudia kuhitimisha maandamano yao na kuwawacha polisi wa Sultani CCM kwenye mataa.
 
Wazo sio bomba. Labda maandamano yawe kama madagascar au Thailand. Vinginevyo bora kuwaiga mungiki. Wajua tatizo letu wa TZ twaogopa kumwaga damu. Kumbukeni Majimaji, Mkwawa na majasiri wetu wa jadi. Nchi ni yetu hii tuipiganie.
 
Wazo sio bomba. Labda maandamano yawe kama madagascar au Thailand. Vinginevyo bora kuwaiga mungiki. Wajua tatizo letu wa TZ twaogopa kumwaga damu. Kumbukeni Majimaji, Mkwawa na majasiri wetu wa jadi. Nchi ni yetu hii tuipiganie.

Majimaji ni uwongo mkubwa sana ulioenea,kuna mjanja aliwadanganya wafuasi wake ila wengine walishitukia hiyo janja na kuingia mitini ,kaitafute historia ya vita vya majimaji uone jamaa walivyokuwa wakiulishwa kwa uongo huo. Tunatoka mbali sana.
 
maandamano ya kulindwa na Polisi hayana RAHA...haytatokuwa na tofauti na maandamano ya UWT au Umoja wa Vijana wa CCM.....raha ya Maandamano mpambane na POLISI....na hapo ndipo Ulimwengu utalipuka na kelele zenu...from there we can write a new history...otherwise tuache idea ya Maandamano.

for what i know from JK..Mkiandamana hamtopigwa..mtaachwa ila mtazuiwa tu msifike IKULU au kuleta fujo za kuvunja biashara. JK his heart is soft in nature...Hawezi ona damu ya Mtanzania inamwagwa kwa Maandamano ambayo kesho yake tu watu watasahau....
the way yanavyoratibiwa hapa tayari yashafeli....!!!
 
Mko tayali afu mnaludi hapa kuulizia kama yamefanyika na kumetokea nini mnadai live newz ,nakumbuka yale maandamano ya CUF pale bongo tulibambwa na polisi katika uchochoro na kuendeshwa mchura mapaka ndani ya karandinga na rungu mtu ,tulipoachiwa jamaa kwenye mskani wacha watucheke yaani na acting kabisa ,walitusanifu vibaya sana.
 
kuna rafiki yangu mmoja kutoka ng'ambo ya bahari, huwa anawahamasisha sana washkaji zake kuandamana kule ng'ambo ila inapotokea dalili ya majiwasha huwa haonekanagi ktk kilinge hata kushiriki, yeye huchagua aina ya maandamano ya yeye kuandamana nao.
Sina nia mbaya ila kwanza lazima kuelimishana kuondoa ukungu wa sheria na haki kutoka kwa wabeba bunduki wetu kisha hata wakiamua kututandika shaba iwe wanajua wanafanya nini maana sasa wanajua kuwa wana kazi moja tu kuwalinda watawala hata kama hao watawala wameoza vipi.
umenipata hapo?

Mkuu Tuache kuonge saana bila vitendo si watu woote wanao ingia na Kusoma yanayo andikwa kweye JF asilimia kubwa hawajui hata kutumia

Sasa magazeti tuliashazoea kama nia hadithi tu sasa wakati umefika kwani haya maandamano ni ya amani tu

Jamani WAKUU wenye nguvu waandae tutakuwa pomoja

Mungu yu Pamoja nasi
 
Mimi nataka maandamano ya fujo kumg'oa JK na CCM madarakani basi. Hawa ndio maadui wetu wa kwanza. Ndio wanaofunga ndoa na mafisadi na kutusababishia umasikini. Kote kwenye mafanikio/maendeleo duniani, raia wake hawataki masihara na wamewahi kutandikana:Ufaransa, Ujeremani, China, USA, Japan, South Africa, Kenya n,k. Damu lazima imwagike kwa ustawi wa kizazi kijacho.
 
Ni woga wetu sisi watu wakati, hesabu tunazipiga nyingi, elimu yetu hajatufanywa tuwe jasiri ila imetufanywa tuwe woga wa kusema wazi tunachofiri.

Hapa mkuu naomba kutofautiana na wewe, elimu ndiyo hiyo iliyokufanya ww hata ukafikiria wazo ulilolitoa, elimu ndiyo ilikuondolea woga wa kuthubutu kuchallenge serikali iwe msituni, hadharani, etc ndo maana leo tunafikiria namna nzuri ya kuichallenge serikali kuhusu ufisadi...ni elimu hiyo mkuu...tukekuwa waoga hatungefanya hata hili!...mkuu hii ni hatua nzuri!

Tunajali zaidi kazi zetu kuliko maisha ya badaye ya watoto wetu! Tumefungwa macho na vijisenti vidogo bila kugundua we can create new employment if change!

Kazi zetu zipi, wengi ya wanaharakati wapo sector binafsi so sitegemei serikali directly ila serikali inatutegemea sisi through kodi binafsi na biashara au shughuli zetu!

The whole problem is about us, and not the people in the streets![/
Not true mkuu, tatizo ni mass education ambayo ingetupa mass support katika hili, out of 40MIL Tanzanians usishangae kuona ni less than 2mil ndio graduates, na less than 10mil wana higher school education, less than 15mil ni form fours!

Mbaya zaidi, less than 5mil Tanzanians ndio wenye elimu sahihi ya uraia na wanatambua haki zao za msingi!

Na hapa kwa maoni yangu the kind of demonstrations that we need here, ni hizo hapo chini mbazo mkuu Kaniki kaelezea, sasa aina hiyo unahitaji kuwa na support kubwa ya vyama vya kiraia, wananchi wengi waliochoshwa na hali iliyopo na wapo tayari kwa lolote lile litakalotokea!....hali tuliyonayo sasahivi wananchi hawaja hamasika kivile, so tunahitaji kutoa elimu ya kutosha kwa watu wetu kabla ya kuwa na maandamano yatakayokidhi malengo yetu! vinginevyo maandamano hayo yataendup kussoprt ufisadi badala ya kupinga (kama alivyosema Mwiba)!

Mbona hujabuy idea ya petition mkuu?

Wazo sio bomba. Labda maandamano yawe kama madagascar au Thailand. Vinginevyo bora kuwaiga mungiki. Wajua tatizo letu wa TZ twaogopa kumwaga damu. Kumbukeni Majimaji, Mkwawa na majasiri wetu wa jadi. Nchi ni yetu hii tuipiganie.

Mkuu Kaniki tupo pamoja!
 
Back
Top Bottom