Maandamano ya kumpokea Lwakatare Bukoba ni kesho kutwa!

DJ Baraka

Senior Member
May 15, 2013
177
82
Kamanda wa polisi mkoani kagera philp kalangi amemaliza press cof hivi punde na kueleza kuwa jeshi hilo limetoa kibali kwa CHADEMA kufanya maandamano na mkutano wa kumpokea mwenyekiti wa CHADEMA M Kagera hapo kesho kutwa june 19,2013 katika uwanja wa uhuru.

amesema ulinzi,utaimarishwa na kuwaomba wafuasi wa CDM kuwa makini kwa kueleza sera zao na kufunga mkutano saa 12:00 jioni.

Jimbo la Bukoba linaongozwa na Balozi Khamis Kagasheki wa CCM tangu 2005.
 
Tatizo ni kuwa wana Bukoba wengi wapo kwa Kagasheki na Lwakatare hana mvuto kwa sasa pale bukoba
 
Chezea nshomile wewe? lolote linaweza tokea,tena kwa sasa ambapo kuna mvutano wa Kagasheki na Meya nafikiri Lwakatare anauza tu
 
Siasa za BK tuulize siye! Hivi unajua katika kesi ya kupinga matokeo ya Kagasheki Lwakatare alishindwa kesi na mahakama kuamuru amlipe Kagasheki milioni 200. Na unajua Kagasheki alikutana na Lwakatare wakakubaliana kwa siri kwamba aachane nazo(kwa makubaliano ya siri).Hivi unajua Lwakatare na Kagasheki lao moja?
Pole sana
 
Tatizo ni kuwa wana Bukoba wengi wapo kwa Kagasheki na Lwakatare hana mvuto kwa sasa pale bukoba
Ukipiga hesabu kwa mlengo huo daima utapata majibu yasiyo sahihi. Suala la Lwakatare linakwenda mbele na juu zaidi kupita siasa na itikadi. Ni suala la Uongo dhidi ya Ukweli, Haki dhidi ya Dhuluma, Uhuru wa kweli dhidi ya Uhuru wa mateka, na hadhi/heshima yetu dhidi ya Siasa chafu.
 
No data no right to speak, Una takwimu za lini zinazodhihirisha kuwa watu wengi wanamuunga mkono kagasheki au we ni gamba? Tuulize sisi tulioko Bukoba kukupe takwimu za nani zaidi kati ya kagasheki na rwakatale.
 
Safi sana,ponti za msingi,hapo tupo wote,mimi ninachopoinga kwa nguvu zangu zote na ndiyo ukweli ni kwamba kwa siasa za Bukoba Lwakatare hauzi tena! kwa suala unalosema hata mimi nipo huko,CCM imetufikisha pabaya sana lakini kwa kumtumia NDUMILA KUWILI kama lwakatare ni kujidanganya tu
 
No data no right to speak, Una takwimu za lini zinazodhihirisha kuwa watu wengi wanamuunga mkono kagasheki au we ni gamba? Tuulize sisi tulioko Bukoba kukupe takwimu za nani zaidi kati ya kagasheki na rwakatale.

Time will tell!
 
Hii habari imeitishwa hado press conference ili tu kuikuza na kufifsha ya Arusha. Inataka kuonyesha kuwa POLISI wanashirikiana vizuri sana na CHADEMA.
 
Nawatakia kila lililo la heri hiyo siku ya maandamano makamanda na wakazi wa Bukoba.......Itumieni vema siku hiyo kuidhihirishia serikali ya CCM kuwa mmechukizwa sana na kile walichomtendea kamanda wetu
 
No data no right to speak, Una takwimu za lini zinazodhihirisha kuwa watu wengi wanamuunga mkono kagasheki au we ni gamba? Tuulize sisi tulioko Bukoba kukupe takwimu za nani zaidi kati ya kagasheki na rwakatale.

ili kuweka kumbukumbu sawa unatakiwa kusema kagasheki na mlisha watu sumu
 
Nawatakia kila lililo la heri hiyo siku ya maandamano makamanda na wakazi wa Bukoba.......Itumieni vema siku hiyo kuidhihirishia serikali ya CCM kuwa mmechukizwa sana na kile walichomtendea kamanda wetu

ivi kwann mnakumbatia wauwaji? Amewatenda tena juzi arusha hampati akili tu?
 
Nawashauri watu wa bukoba siku hiyo wajihadhari wasije wakalishwa sumu na zaidi wapige yowe wakimuona
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom