Maandamano ya CHADEMA Yaungwe Mkono na Kila Mwenye Kuiependa nchi-Magige Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya CHADEMA Yaungwe Mkono na Kila Mwenye Kuiependa nchi-Magige Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Feb 27, 2011.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu.

  Leo tulitembelea Kaburi la Hayati Baba wa taifa na kufanikiwa kukutana na Mama Maria pamoja na watoto wake wawili,Magige na Makongoro. Walitupokea vizuri sana.Pamoja na mambo yote yaliyofanyika kuna jambo moja tu nililolipenda zaidi.Maneno mazuri ya Magige kwa chama cha CHADEMA kuhusu maandamano. Amesema hivi ukiwa huna taarifa utapinga sana wanachokifanya CHADEMA kama ambavyo yeye alikuwa akipinga mwanzoni hasa Wabunge wa CHADEMA walivyotoka nje ya Bunge kutomsikiliza Rais Kikwete lakini baadaye amejifunza kwamba CHADEMA wanafanya kitu chema na akatoa mfano wa maandamano yanayoendelea sasa kuwa yanaumuhimu mkubwa sana hivyo akatoa rai kuwa kila mwenye kuipenda nchi hii basi lazima aunge mkono harakati hizi za CHADEMA.Amekiri kuwa yeye ni CCM damu lakini anaunga mkono harakati hizi za CHADEMA.

  Vile Vile ameitakia CHADEMA ushindi wa Urais mwaka 2015 kwa kutaka wajitokeza wapiga kura Milioni Kumi na Mbili halafu CHADEMA ipate Kura Milioni Sita na CCM Milioni Nne.

  Nawasilisha
  Kutoka Kitangiri Mwanza

  Reagia E Mtema
  Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nafikiri kuna hoja ya kufanyiwa kazi hapo...

  Ni kweli kunahitajika nguvu na mkakati wa kuhamasisha haya maandamano na kupata mwitikio wa mkubwa zaidi... kuna uwezakano wa kufanya vizuri kuliko ilivyo sasa!
   
 3. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wakuu.

  Leo tulitembelea Kaburi la Hayati Baba wa taifa na kufanikiwa kukutana na Mama Maria pamoja na watoto wake wawili,Magige na Makongoro. Walitupokea vizuri sana.Pamoja na mambo yote yaliyofanyika kuna jambo moja tu nililolipenda zaidi.Maneno mazuri ya Magige kwa chama cha CHADEMA kuhusu maandamano. Amesema hivi ukiwa huna taarifa utapinga sana wanachokifanya CHADEMA kama ambavyo yeye alikuwa akipinga mwanzoni hasa Wabunge wa CHADEMA walivyotoka nje ya Bunge kutomsikiliza Rais Kikwete lakini baadaye amejifunza kwamba CHADEMA wanafanya kitu chema na akatoa mfano wa maandamano yanayoendelea sasa kuwa yanaumuhimu mkubwa sana hivyo akatoa rai kuwa kila mwenye kuipenda nchi hii basi lazima aunge mkono harakati hizi za CHADEMA.Amekiri kuwa yeye ni CCM damu lakini anaunga mkono harakati hizi za CHADEMA.

  Vile Vile ameitakia CHADEMA ushindi wa Urais mwaka 2015 kwa kutaka wajitokeza wapiga kura Milioni Kumi na Mbili halafu CHADEMA ipate Kura Milioni Sita na CCM Milioni Nne.

  Nawasilisha
  Kutoka Kitangiri Mwanza

  Reagia E Mtema
  Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
  ?Safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa na Bado itafika wakati tutavuna kura za wana ccm wengi.kaza buti mama tuko nyuma yako.
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mmmmh,anaturudisha nyuma huyu mtu!

  Mwaka jana walojiandikisha walikuwa mil19,....wakapiga kura mil8.

  2015 watu wenye sifa za kupiga kura wanaweza kuwa mil25 hivi,yeye anataka mil12 tu ndo wajitokeze,....yaani huo ndo uhamasishaji kweli?
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mh Regia,
  In 2015 naanzia kaudiwani kuleeee Uyui ili tuichukue halmashauri ya wilaya ile, msiusahau mkoa wa TBR maana ndio CCM inapojivunia. Piteni kidogo kule muwahuishe wanyamwezi.
  Nakupongeza kwa kuwa mstari wa mbele kutuhabarisha yanayojiri huko ziarani kwenu, bravo.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Aksante kwa taarifa Regia.

  Tunahitaji watu wengi sana wa dizaini ya Magige...Asomaye na afahamu hapo, kuwa kuvaa kijani si hakikisho la kura!

  Kinachotakiwa sasa hivi ni mabadiliko, whether vyama fulani vitajipaka rangi mpya, au kuzuia mabadiliko ndani ya Bunge, hakuna kitakachoweza kupenya kwenye Bongo za wananchi na kubadilisha fikra zao...

  Too bad!...there comes a time in life, when a man has to seek for an alternate way of ideology.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  hujui hata maana ya mfano?
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Are You Serious unataka kugombea?nikuorodheshe maana ninahusika na kutambua Wagombea Watarajiwa.
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mie sijajua kama nitagombea ubunge au udiwani,in any case razima iwe Tarime kama jimbo au Tarime Mjini kama kata
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mami Mpevu na Regia,

  Hapa tupo wote kabisa. Chadema tembeleeni Tabora walau mara mbili kwa mwaka. Muweke njia ya watu wengine kutaka kugombea huko. Tatizo ni kuwa sisi Wanyamwezi ni woga sana na umasikini uliopo, CCM na uongozi wake huko kwenye Mizizi, wanawaadhibu vikali sana wale waote wanaotaka kujitenga na CCM.

  Unakuta Mwenyekiti wa kijiji/mji kama Kipalapala, anakuwa kama Mungu mtu. Watu wanamuogopa hadi huwezi kuamini. Wanajenga vijela vyao na kutumia Sungusungu kuadhibu watu watakaowapinga. Usiombe ukamatwe na wakupeleke Iselamagazi (Sehemu za kutesea, kama walizokuwa wakitumia Askari wa Mirambo waitwao Walugaluga ikiwa na maana Sehemu ya Kumwaga Damu).

  Tumbaku na Asali ndiyo zao kuu pekee. Kiwanda ya kusindika asali kilijifia kama sikosei na kiwanda cha nyuzi kina suasua maana umeme wenyewe wa kuchota kwenye Mabeda (kwa waliosoma Mazengo, ilikuwa kawaida Form one kuambia mkachote umeme kwenye mabakuli ya kulia msosi). Hata kiwanda cha kuchambulia tumbaku, mijinga ilichukua pesa na kikajengwa Morogoro.

  Njooni jamani Tabora ili muweke njia ya watu kugombea kwa kupitia Chadema. Njooni muwatowe woga maana huku Tabora, CCM ndiyo wanatumia kuchachua kura za Urasi si kawaida maana kwenye uchaguzi, wako wenyewe tu. Wanajiandikia idadi wanaotaka wao.

  WAHINI TABORA na mkiweza basi JENGENI HATA MAKAO MAKUU YA CHADEMA yawe TABORA.
   
 11. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante regia,
  but yuko wapi mtu wa habari wa chadema au mawasiliano?nadhani ni tumbo.mbona hatumuoni akitujuza zaidi ya wewe kuwa unatujuza pamoja na kuwa waziri wa kazi na ajira?!tunasisitiza,mwenye kazi aifanye kazi yake!! Thank you for informing us anyway!
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  HIZI NI TAARIFA NZURI SANA.
  kweli huu ni wakati wa CDM kufanya mavuno
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  lakini unajua ni wangapi waliopiga kura?
   
 14. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Huu ni ushauri mzuri sana na ninaomba CDM wauchukue na kuwa implimented kulingana na ratiba zao.
  Ila umenishitua mkuu, hivi hii karne bado kuna maaneo watu bado wanateswa na sungusungu kiasi hicho??
  kama kweli basi tz bado kuna kazi kubwa
   
 15. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  • Mama Maria aongoza sala

  na Sitta Tumma na Janeth Josiah, Musoma

  FAMILIA ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, imekitabiria Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa kishindo wa kuongoza nchi mwaka 2015.

  Familia hiyo ya mwasisi wa taifa imesema ukomo wa serikali ya CCM umefika ambapo inaamini Uchaguzi Mkuu wa urais ujao, CHADEMA itaibuka kidedea.

  Kauli hiyo ya familia ya Mwalimu Nyerere, ilitolewa jana na mtoto wa tatu wa Baba wa Taifa, Magige Nyerere, akiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati viongozi wa CHADEMA Taifa walipozuru nyumbani kwa mwasisi huyo Butiama, Musoma, mkoani Mara, ambapo waliweka mashada katika kaburi hilo na Mama Maria kuongoza sala.

  Alisema anaamini wapigakura mwaka 2015 watakuwa milioni 12 na kati ya hao, CHADEMA itapata kura milioni sita na CCM itaambulia kura milioni nne.

  Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo wa Baba wa Taifa kwa sasa nchi iko katika joto kubwa la kisiasa.

  "Lazima tuseme ule ukweli uchaguzi mkuu uliopita CHADEMA haikuweza kuongoza dola, lakini mwaka 2015 wapigakura watakuwa milioni 12 na milioni sita zitaenda CHADEMA na milioni nne CCM.

  "Hali ilivyo sasa, joto la kisiasa hapa nchini liko juu na wananchi wameonekana kufanya mageuzi ya kiuongozi," alisema Magige Nyerere mbele ya mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere.

  Huku akimfananisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mdogo wake, Makongoro Nyerere, ambaye naye alikuwapo alisema, "Nakiri kuwa mimi ni CCM, lakini nafurahia kazi na siasa yenu…naomba uendelee hivyo na hata ukiwa bungeni kama kiongozi wa upinzani."

  Viongozi hao wa CHADEMA na msafara wao walizuru nyumbani kwa Nyerere majira ya saa 5:55 asubuhi kwa lengo la kumsalimia mjane wa Baba wa Taifa.

  Kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alimuomba Mama Maria kukiunga mkono chama hicho na kukiombea mema.

  "Mama tumekuja kukusalimia na familia yako…CHADEMA tunaomba mtuombee na mtuunge mkono," alisema Mbowe kisha Mama Maria kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelezo hayo.

  Akitoa nasaha zake mbele ya kaburi la Nyerere, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema mchakato wa Nyerere kuwa Mtakatifu mwenye kheri bado haujakamilika, hivyo raia wawe na uvumilivu.

  Alisema nchi ya Uganda imepiga hatua juu ya mchakato huo, hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.

  Kuhusu maandamano ya CHADEMA nchi nzima, Magige Nyerere alisema," Awali nilipatwa na wasiwasi mkubwa, lakini nimebaini kumbe ni maandamano mazuri; yaendelee."

  Hata hivyo, mtoto huyo wa Baba wa Taifa alisema maandamano hayo ni vema yakaendelea kwa amani, ili kufikisha ujumbe husika katika mamlaka husika.

  Wakiwa wilayani Tarime jana Mbowe alimtaka Rais Kikwete kuacha mara moja kuwajaza hofu Watanzania juu ya kuwepo mipasuko ya kidini. Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa kabla ya mkutano, alihoji sababu ya Rais Kikwete kushindwa kuwakamata na kuwasweka ndani wanaoleta chokochoko za kidini.

  Viongozi hao wa CHADEMA kesho wataendelea na ziara yao katika mkoa wa Shinyanga kwa kufanya maandamano makubwa ya kuwashukuru wananchi kwa kuwapa kura na kuwataka wananchi wapinge hatua ya serikali ya kutaka kuilipa kampuni ya Dowans.

  Source: Tanzania Daima litakalotoka kesho tarehe 28/02/2011
   
 16. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Men,hujasoma post yangu au unataka nikwambie walipiga kura watu mil19 na unajua kabisa nec walisema ni mil8.kadhaa?
  Wawe wamechakachua au hawa kuchakachua,takwimu za sasa ni zile walizo tupatia wao!
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wow.Jitahidi basi ufanye maamuzi tuanze kujipanga mapema.Biashara asubuhi jioni mahesabu.
   
 18. A

  Alfa Romeo Member

  #18
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  With such an endorsement from Mwl Nyerere's family,we have something to cheer about!
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Sikonge.Salaam.

  Karibu sehemu nyingi tu ya Tanzania kuwa Mpinzani ni aibu na kichekesho.Viongozi wengi wa CCM ni Miungu na Ukiwa Mpinzani hata haki zako mbalimbali za msingi unapoteza.Ukiwa mdau wa Mabadiliko You cab a change kwenye hilo eneo.Sio lazima mpaka viongozi waje kutembelea mara kwa mara,wewe unaweza kufanya hivyo kazi.Kuwa na Makao Makuu sehemu fulani hakumaanishi ndio watu wataamka sana.Makao Makuu kwa sasa yapo Kinondoni Dar lakini sidhani kama kina wako active kulinganisha na baadhi ya maeneo tulipopata Wabunge.Ni lazima mjitokeze watu ngazi za chini mkafanya kazi kwa bidii katika kukisimika chama.Tunaweza tukafanya ziara huko mara mbili kwa mwaka kama ulivyopendekeza lakini tukiondoka tunaondoaka na chama chetu kama nyie hamtakuwa tayari na mnatgemea mpka viongozi wa kitaifa waje ndio waamshe.Tulifanya Sangara very Serously Mkoa wa Dodoma lakini Kura zake kwenye uchaguzi Mkuu zinasikistisha.

  Mkoa wa Morogoro haijawahi kufanyika Ziara hata moja ya Kitaifa lakini majimbo Matatu yalifanya Vizuri ingawa hayakushinda,Jimbo la Morogoro Mjini,Mvomero na Kilombero.Tena Kilombero limekuwa Jimbo la Nane kwa kupata kura nyingi likiongozwa na Jimbo la Ubungo.Fanyeni kazi tutawaunga mkono kila mmoja atimize wajibu wake kwa pamoja tutafika.
   
 20. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mh,
  Am an energetic young man aged 30 years, kwa taarifa yako ni kwamba babu yangu alikuwa ni diwani kupitia chama tawala kata ya IBIRI. Mzee wangu huyu aliuawa kwa kupigwa risasi na kuuawa mwaka Dec 2008 kwa visasi vya kisiasa kupitia chama tawala. Ndio maana inanisukuma nikawakomboe wanyamwezi wenzangu kule. Mengi nitaongea nawe kwa privacy, ili mikakati ichukue nafasi.
   
Loading...