Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

ni kweli mfa maji haachi kutapa tapa
hawa jamaa maji tayari yako shingoni na hawana pa kukimbilia
ngoja ninywe kahawa kidogo ubongo uchangamke:coffee:
Pls Ruta take this one too:coffee:
 
Nimeona watu wanataka tuandae maandamano kama ya Misri, haya pia yanawezekana ila tujiandae kweli wanasema mfa maji haachi kutapatapa watatupiga mabomu ili tukivumilia wao watafikiri kutukimbia na hapo tumeshinda. Tuanzie kwa haya mabomu ya Gongo la mboto tuitishe maandamano; acheni woga. Maana sasa kila aliyeko mahali akikasilika anaumiza wenzake; wanajeshi wameachia mabomu, madaktari nao wakificha dawa, maabara wanatuma kimeta, umeme, maji nao???? tusisubiri kuumizana tuwaumizeni watawala kwa kuwafukuza ikulu bora tuongozwe na jeshi kama Misri
 
Ndio maana ya serikali TATU. to put it in a right angle.

Ruta usilazimishe fikra zako. By the way si za kweli. Unahitaji uwe na kaueewa kidogo tu .
 
Hapo sasa ndipo pa kushika tusiachie, tuandaeni mahali pa kukutania Dodoma au Mwanza square maana DSM maisha yatakuwa magumu kiuchumi tutashindwa. Tujipange wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima. Hii nchi yetu sote tusiwaachie wale hawa washenzi peke yao; tuondoeni woga tuingie mitaani watakimbia tu tena walivyo waoga hawamalizi siku tatu wameng'oka msiogope
 
Watakaovunja amani ya Tanzania ni CCM kwa upendeleo, wizi, ubinafsi, uchoyo, roho mbaya ya viongozi wao.
 
Pinda lazima awe na hofu kwa sababu hakuachaguliwa na wananchi.Aliachakachua akadai amepita bila kupingwa. Lkn Masha aliwaumbua wale wote waliodai kupita bila kupingwa.

Tafadhali nipashe sikusikia Masha alisema nini juu ya waliopita bila kupingwa.
 
Ma handsome kweli hawa. Wakienda kufungua kisima. Image za wote maji yawezageuka sumu kama maneno yao
 
Raisi kikwete tafadhali sana ili kupunguza hasira za wananchi;
1 Wawajibishe bila huruma hawa kina mwinyi na mwamnyange haraka
hawa uliwateua mwenyewe na kuwapa dhamana kwa sababu zako.
Sasa wamevurunda unasubiri nini?
Wazalamo walonga 'kumkoma nyani giladi'(ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni)

2 Shinikiza mkutano wa katiba mwenyewe wala usiwasikilize wapambe nuksi hao watakuzamisha hao.

Kikulacho kii nguoni mwako!
kazi kwako mwanangu.
 
Tuandae freedom square yetu tuwaondoshe madarakani hawa ccm na kikwete waliuochoka kufikiri, hawana dira wala sera za kutuongoza tuseme basi
JIHADHARINI. serikali ya CCM ilishawahi mara kadhaa kukandamiza maandamano kwa mtutu wa bunduki, na baada ya kuona mafanikio ya Gadaffi, haitosita kutumia ndege za kivita na vifaru kuwamaliza "wapinzani". Kwa kutaka kuendelea madarakni, wako tayari watawale mafuru ya vichwa kama anavyofanya mshiriki wake mkubwa - Gadaffi.
 
Maandamano makubwa CHADEMA Mwanza

*Ni kupinga malipo Dowans, kupanda gharama za maisha

Na Waandishi Wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuanza kutekeleza agizo la Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kufanya maandamano na
mikutano kesho, ikiwa ni ishara ya kupinga mambo kadhaa, ikiwemo mgawo na ongezeko la bei ya umeme kwa kuwa yameongeza ugumu wa maisha ya kila siku kwa Mtanzania.

Kwa mujibu wa viongozi wa juu wa CHADEMA, Mwenyekiti wa taifa, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa pia watazungumzia matukio kadhaa yanayotokea nchini ikiwemo suala la milipuko katika kambi za jeshi, hasa tukio la karibuni la mlipuko katika kambi ya Gongolamboto.

“Kwa kifupi niseme tunatarajia kuanza kampeni yetu ya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima wiki hii kama tulivyoahidi. Tunaanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa na kituo cha kwanza kitakuwa Mkoa wa Mwanza na baadaye mikoa mingine. Tutazungumzia mambo mengi yenye maslahi kwa taifa letu,� alisema Dkt. Slaa.

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya kufanya kusanyiko bila kibali inayowakabili viongozi kadhaa na wanachama wa Chama hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Dkt. Slaa alisema watatumia mikutano hiyo kuwaeleza wananchi
ukweli wa tukio la mauaji ya Arusha ili kuzuia upotoshaji unaofanywa na serikali kupitia vyombo na idara zake mbalimbali.

Wakati serikali kupitia jeshi la polisi na mamlaka zingine imekuwa ikielezea tukio hilo na kukitupia lawama chama hicho kwa vurugu zilizosababisha mauaji hayo Januari 5, mwaka huu, CHADEMA nao kwa upande wao wamedai kukusanya ushahidi ukiwemo wa kielektroniki kuthibitisha kuwa mauaji hayo yalipangwa na kutekelezwa na polisi kwa makusudi kwa shiniko la wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa pande wake, Bw. Mbowe alisisitiza kuwa CHADEMA haitapumzika katika kudai mabadiliko na mambo ya msingi yanayohusu maisha ya Watanzania na kutamba kuwa hakuna nguvu yoyote, iwe ya dola, mabomu wala risasi itakayozuia hamu ya mabadiliko inayotakiwa na umma wa watanzania.

“Hakuna njia ya kuzuia mabadiliko yanayotakiwa wa umma, CHADEMA kama tulivyoanza tutaongoza kampeni kudai mabadiliko yenye tija na maslahi kwa nchi bila kujali tofauti za kiitikadi za vyama. Maisha magumu yanayowakabili Watanzania kwa sasa haubagui, wote wamepigika sawa sawa. Lazima tuungane sote kudai maisha bora
tunayoahidiwa kila siku bila utekelezaji,� alisema, Bw. Mbowe.

Akifafanua alisema mateso wanayopata Watanzania yanasababishwa na viongozi walioko madarakani kukosa utashi wa kisiasa kuyakabili na kutolea mfano mfumuko wa bei unaosababisha bidhaa kupanda bei kila kukicha wakati uwezo wa kununua kwa mwananchi wa kawaida ukipungua huku viongozi wakipita na kutamba kuwa uchumi umekua na
kuimarika.

“Watanzania hawahitaji uchumi unaokuwa kwenye makaratasi na takwimu za wataalamu. Kinachotakiwa ni ukuaji huo kuonekana katika maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida na hii inahusu uwezo wa kununua bidhaa na mahitaji muhimu. Uchumi utakuaje wakati mtu hana uhakika wa bei ya sukari dukani kwani inapanda kila siku licha
kujengwa viwanda vingi vya sukari nchini kuliko kipindi kingine chochote?.

"Mwaka 2005 wakati rais Kikwete anaingia madarakani, bei ya kilo moja ya sukari ilikuwa sh. 600. Lakini kiasi hicho kwa sasa kinauzwa kati ya sh. 1,700 hadi 2,000 ambayo ni karibia ongezeko la asilimia 150 ndani kipindi cha miaka sita tofauti na kipindi cha awamu ya tatu chini, Bw. Benjamin Mkapa ambapo bei ya bidhaa
ilidhibiti kwa karibu miaka yote kumi aliyokaa madarakani.

"Pamoja na sukari baadhi ya bidhaa zingine za mahitaji ya kila siku zilizopanda bei mara dufu na bei za zamani na mpya kwenye mabano ni pamoja na paketi moja ya kiberiti (sh. 20 hadi 50), kipande cha sabuni (sh. 100 hadi 350), pakiti moja ya chumvi (sh. 50 au 100 hadi sh. 200 au 300), kilo moja ya nyama ya ng’ombe (sh.
2,000 hadi 4,000 au 5,000). Hii ni mifano michache kwani orodha ni ndefu," alisema.

Wakati hali ikiwa hivyo, makusanyo ya serikali kutokana kodi mbalimbali imeongezeka kutoka sh. bilioni 250 kwa mwezi hadi zaidi ya bilioni 400 na hivyo kuipa nguvu hoja kuwa tatizo siyo fedha bali utashi wa viongozi na mipango ya vipaumbele vya taifa katika matumizi ya serikali na haya ni baadhi ya mambo ambayo CHADEMA wameahidi kufafanua na kuyahainisha katika kampeni yao nchi nzima.

Hivi karibuni akitoa taarifa ya CC kwa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alisema kuwa mbali ya kuwahimiza wana-CHADEMA, wabunge na wananchi kwa ujumla kuendelea kupinga kwa nguvu zote malipo ya Dowans, CC ya chama hicho pia iliagiza sekretarieti kuanza maandalizi ya maandamano ya nchi nzima kupinga ongezeko la bei ya umeme, gesi na malipo kwa Dowans yatakayoanzia jijini Mwanza, Februari 24, mwaka huu.

"Kamati kuu imesikitishwa na kupanda holela kwa bei ya nishati muhimu ya umeme na gesi, pamoja na kushindwa kwa serikali ya CCM katika kuwekeza kikamilifu katika sekta ya nishati hapa nchini," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumza na Majira jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Bw. Erasto Tumbo, alisema wataanza kwa maandamano jijini Mwanza, yatakayofuatiwa na mkutano katika viwanja vya Furahisha, kisha katika wilaya za mkoa huo.

"Kesho yake tutasambaa na kufanya mikutano katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza. Mikutano hiyo itafanyika pia kwa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, baada ya Mwanza, itafuata Shinyanga, kisha Mara halafu Kagera, kwa staili hiyo hiyo ya kufanya mkutano makao makuu ya mkoa kisha katika wilaya zote za mkoa husika," alisema Bw. Tumbo.

Aliongeza "tunawaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi katika kila eneo husika, tutafanya maandamano ya amani, tayari tumeshatoa taarifa kwa polisi, hivyo hatuna mgogoro nao tena, na kwa sababu tumetoa muda mrefu bila shaka taarifa za kiintelijensia watakuwa wameshafanyia kazi ili kuhakikisha kuwa raia na mali zao wanalindwa."

Wakati huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha, imeamuru kesi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA isijadiliwe nje ya mahakama hata kama inawahusu viongozi wakuu wa kitaifa wa chama hicho.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha, Bw. Charles Magesa alisema hayo jana wakati akizungumzia hoja zilizotolewa mahakamani hapo na mawakili wa upande wa utetezi na upande wa washtakiwa.

Bw. Magesa alikubaliana na hoja ya wakili wa upande wa utetezi na kutoa onyo kwa wale wote wanaoeleza masuala ya mahakamani nje ya mahakama.

“Mahakama hii, inatoa onyo kuacha mara moja kwa mtu yoyote kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani, kwani wanaofanya hivi wanajua wazi sheria zinakataa na hata wale wanaotoa vielelezo kwenye vyombo vya habari, nao waache mara moja, kwa kuwa wanavunja sheria,� alisema Bw. Magesa.

Imeandikwa na Tumaini Makene, Peter Saramba na Glory Mhiliwa

Maandamano makubwa CHADEMA Mwanza

*Ni kupinga malipo Dowans, kupanda gharama za maisha

Na Waandishi Wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuanza kutekeleza agizo la Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kufanya maandamano na
mikutano kesho, ikiwa ni ishara ya kupinga mambo kadhaa, ikiwemo mgawo na ongezeko la bei ya umeme kwa kuwa yameongeza ugumu wa maisha ya kila siku kwa Mtanzania.

Kwa mujibu wa viongozi wa juu wa CHADEMA, Mwenyekiti wa taifa, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa pia watazungumzia matukio kadhaa yanayotokea nchini ikiwemo suala la milipuko katika kambi za jeshi, hasa tukio la karibuni la mlipuko katika kambi ya Gongolamboto.

“Kwa kifupi niseme tunatarajia kuanza kampeni yetu ya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima wiki hii kama tulivyoahidi. Tunaanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa na kituo cha kwanza kitakuwa Mkoa wa Mwanza na baadaye mikoa mingine. Tutazungumzia mambo mengi yenye maslahi kwa taifa letu,â€� alisema Dkt. Slaa.

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya kufanya kusanyiko bila kibali inayowakabili viongozi kadhaa na wanachama wa Chama hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Dkt. Slaa alisema watatumia mikutano hiyo kuwaeleza wananchi
ukweli wa tukio la mauaji ya Arusha ili kuzuia upotoshaji unaofanywa na serikali kupitia vyombo na idara zake mbalimbali.

Wakati serikali kupitia jeshi la polisi na mamlaka zingine imekuwa ikielezea tukio hilo na kukitupia lawama chama hicho kwa vurugu zilizosababisha mauaji hayo Januari 5, mwaka huu, CHADEMA nao kwa upande wao wamedai kukusanya ushahidi ukiwemo wa kielektroniki kuthibitisha kuwa mauaji hayo yalipangwa na kutekelezwa na polisi kwa makusudi kwa shiniko la wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa pande wake, Bw. Mbowe alisisitiza kuwa CHADEMA haitapumzika katika kudai mabadiliko na mambo ya msingi yanayohusu maisha ya Watanzania na kutamba kuwa hakuna nguvu yoyote, iwe ya dola, mabomu wala risasi itakayozuia hamu ya mabadiliko inayotakiwa na umma wa watanzania.

“Hakuna njia ya kuzuia mabadiliko yanayotakiwa wa umma, CHADEMA kama tulivyoanza tutaongoza kampeni kudai mabadiliko yenye tija na maslahi kwa nchi bila kujali tofauti za kiitikadi za vyama. Maisha magumu yanayowakabili Watanzania kwa sasa haubagui, wote wamepigika sawa sawa. Lazima tuungane sote kudai maisha bora
tunayoahidiwa kila siku bila utekelezaji,� alisema, Bw. Mbowe.

Akifafanua alisema mateso wanayopata Watanzania yanasababishwa na viongozi walioko madarakani kukosa utashi wa kisiasa kuyakabili na kutolea mfano mfumuko wa bei unaosababisha bidhaa kupanda bei kila kukicha wakati uwezo wa kununua kwa mwananchi wa kawaida ukipungua huku viongozi wakipita na kutamba kuwa uchumi umekua na
kuimarika.

“Watanzania hawahitaji uchumi unaokuwa kwenye makaratasi na takwimu za wataalamu. Kinachotakiwa ni ukuaji huo kuonekana katika maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida na hii inahusu uwezo wa kununua bidhaa na mahitaji muhimu. Uchumi utakuaje wakati mtu hana uhakika wa bei ya sukari dukani kwani inapanda kila siku licha
kujengwa viwanda vingi vya sukari nchini kuliko kipindi kingine chochote?.

"Mwaka 2005 wakati rais Kikwete anaingia madarakani, bei ya kilo moja ya sukari ilikuwa sh. 600. Lakini kiasi hicho kwa sasa kinauzwa kati ya sh. 1,700 hadi 2,000 ambayo ni karibia ongezeko la asilimia 150 ndani kipindi cha miaka sita tofauti na kipindi cha awamu ya tatu chini, Bw. Benjamin Mkapa ambapo bei ya bidhaa
ilidhibiti kwa karibu miaka yote kumi aliyokaa madarakani.

"Pamoja na sukari baadhi ya bidhaa zingine za mahitaji ya kila siku zilizopanda bei mara dufu na bei za zamani na mpya kwenye mabano ni pamoja na paketi moja ya kiberiti (sh. 20 hadi 50), kipande cha sabuni (sh. 100 hadi 350), pakiti moja ya chumvi (sh. 50 au 100 hadi sh. 200 au 300), kilo moja ya nyama ya ng’ombe (sh.
2,000 hadi 4,000 au 5,000). Hii ni mifano michache kwani orodha ni ndefu," alisema.

Wakati hali ikiwa hivyo, makusanyo ya serikali kutokana kodi mbalimbali imeongezeka kutoka sh. bilioni 250 kwa mwezi hadi zaidi ya bilioni 400 na hivyo kuipa nguvu hoja kuwa tatizo siyo fedha bali utashi wa viongozi na mipango ya vipaumbele vya taifa katika matumizi ya serikali na haya ni baadhi ya mambo ambayo CHADEMA wameahidi kufafanua na kuyahainisha katika kampeni yao nchi nzima.

Hivi karibuni akitoa taarifa ya CC kwa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alisema kuwa mbali ya kuwahimiza wana-CHADEMA, wabunge na wananchi kwa ujumla kuendelea kupinga kwa nguvu zote malipo ya Dowans, CC ya chama hicho pia iliagiza sekretarieti kuanza maandalizi ya maandamano ya nchi nzima kupinga ongezeko la bei ya umeme, gesi na malipo kwa Dowans yatakayoanzia jijini Mwanza, Februari 24, mwaka huu.

"Kamati kuu imesikitishwa na kupanda holela kwa bei ya nishati muhimu ya umeme na gesi, pamoja na kushindwa kwa serikali ya CCM katika kuwekeza kikamilifu katika sekta ya nishati hapa nchini," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumza na Majira jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Bw. Erasto Tumbo, alisema wataanza kwa maandamano jijini Mwanza, yatakayofuatiwa na mkutano katika viwanja vya Furahisha, kisha katika wilaya za mkoa huo.

"Kesho yake tutasambaa na kufanya mikutano katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza. Mikutano hiyo itafanyika pia kwa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, baada ya Mwanza, itafuata Shinyanga, kisha Mara halafu Kagera, kwa staili hiyo hiyo ya kufanya mkutano makao makuu ya mkoa kisha katika wilaya zote za mkoa husika," alisema Bw. Tumbo.

Aliongeza "tunawaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi katika kila eneo husika, tutafanya maandamano ya amani, tayari tumeshatoa taarifa kwa polisi, hivyo hatuna mgogoro nao tena, na kwa sababu tumetoa muda mrefu bila shaka taarifa za kiintelijensia watakuwa wameshafanyia kazi ili kuhakikisha kuwa raia na mali zao wanalindwa."

Wakati huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha, imeamuru kesi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA isijadiliwe nje ya mahakama hata kama inawahusu viongozi wakuu wa kitaifa wa chama hicho.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha, Bw. Charles Magesa alisema hayo jana wakati akizungumzia hoja zilizotolewa mahakamani hapo na mawakili wa upande wa utetezi na upande wa washtakiwa.

Bw. Magesa alikubaliana na hoja ya wakili wa upande wa utetezi na kutoa onyo kwa wale wote wanaoeleza masuala ya mahakamani nje ya mahakama.

“Mahakama hii, inatoa onyo kuacha mara moja kwa mtu yoyote kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani, kwani wanaofanya hivi wanajua wazi sheria zinakataa na hata wale wanaotoa vielelezo kwenye vyombo vya habari, nao waache mara moja, kwa kuwa wanavunja sheria,â€� alisema Bw. Magesa.

Imeandikwa na Tumaini Makene, Peter Saramba na Glory Mhiliwa

Risasi za moto, mabomu zapigwa kuizima Chadema Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:27

arushalema.jpg
Moses Mashalla na Musa Juma, Arusha
MPAMBANO kati ya Jeshi la Polisi na wafuasi wa Chadema jana umetikisa tena Jiji la Arusha baada ya chombo hicho cha dola kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi kuwatanya mashabiki hao waliokuwa wakimsindikiza ofisini mbunge wao, Godbles Lema, akitokea mahakamani.

Tukio hilo limekuja takribani mwezi mmoja baada ya mpambano mkali kati ya polisi na wafuasi wa chama hicho chenye ngome kubwa ya kisiasa katika Ukanda wa Kaskazini, ambao ulisababisha mauaji ya watu wawili na majeruhi.

Jana mnamo saa 5:30 asubuhi, wakati wafuasi hao walipokuwa wakitokea kwenye Mahakama ya Hakimu Mfawidhi mkoani Arusha kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wakuu wa chama hicho, walianza kutembea barabarani wakiwa na mbunge wao huku wakimsindikiza kwa umbali wa kilomita tatu.

Wakiwa na mbunge huyo katika msafara wao, wafuasi hao walitembea kuanzia nje ya Mahakama Kuu na kupitia Barabara ya Uhuru, kisha kuingia Barabara ya Boma mkabala na ofisi za Mkuu ya Mkoa wakielekea kwenye ofisi za mbunge huyo.

Katika msafara huo wa kumsindikiza mbunge wao, wafuasi hao walisikika wakiimba nyimbo mbalimbali kumshutumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisema, "Waziri mkuu Pinda kaudanganya umma" pamoja na kumkataa Meya wa Arusha wakisema, "Hatumtaki Meya wa Arusha."

Hata hivyo, wakati wafuasi hao wakiwa katika barabara ya Boma mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Zuberi Mwombeji, walifika na magari mawili waliyoyatumia kuyakinga kwa mbele gari la mbunge huyo pamoja na wafuasi wao, kisha kuanza kufyatua risasi za moto hewani na mabomu ya machozi kuwatawanya.

Matumizi hayo ya risasi za moto na mabobu yalifanyika baada ya polisi kuona wafuasi hao walikaidi amri halali, iliyowataka kutawanyika kwa amani.

Katika tukio hilo, kiongozi huyo wa polisi alisikika akiamuru vijana wake akisema, "Pigeni pigeni," ndipo askari hao walianza kufyatua mabomu ya machozi na kurusha risasi za moto hewani.

Rekodi za Mwananchi ziliweza kuthibitisha kwamba, katika tukio hilo ilisikika milio sita ya mabomu ya machozi iliyolenga kuwatimua wafuasi hao wa Chadema huku polisi wakitumia magari hayo mawili moja likiwa na namba PT 1844 .

Hali hiyo iliwalazimisha wafanyabiashara waliokuwa karibu na eneo hilo kufunga maduka yao huku ofisi za Manispaa ya Arusha, zikifungwa kwa muda na baadhi ya watu wakionekana wakitoka nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kushuhudia huku wengine wakikimbia ovyo.

Raia wa kigeni watimua mbio

Raia mbalimbali wa kigeni walionekana wakitimua mbio nje ya Hoteli ya New Safari iliyopo mkabala na eneo hilo, huku baadhi ya wakazi wakihaha kutafuta maji kwa ajili ya kujinusuru na moshi wa mabomu ya machozi.

Hata hivyo, Lema alifika na baadhi ya wafuasi wa Chadema katika ofisi zake ndani ya jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambako baada ya polisi kutoweka, wafuasi wa chama hicho walisimama nje ya jengo hilo na kuanza kuimba nyimbo za uhuru, huku wakitoa kauli za kulilaani Jeshi la Polisi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu muda mfupi baada ya vurugu hizo, Lema alilaani polisi kuwasambaratisha wafuasi waliokuwa wakimsindikiza kuelekea ofisini kwake baada ya kutoka mahakamani akidai hapakuwa na ulazima wa kupiga risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.

Lema aonya mpasuko mkubwa kutokea

Hata hivyo, Lema alidai endapo viongozi wa Serikali wasipokubali ukweli na kushidwa kuutatua mgogoro wa Arusha huenda wakaiingiza nchi katika machafuko.

Akizungumzia sakata la kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuwa Waziri Mkuu kuwa aliudanganya umma, Lema alisema watakula sahani moja na kiongozi huyo.

"Nchi itaingia kwenye machafuko yasiyo na ulazima kama Tunisia endapo viongozi wetu serikalini wasipokubali ukweli na kutafuta namna ya kuutatua mgogoro huu,na suala la Waziri Mkuu bado tunakula naye sahani moja,"alisema Lema.

Polisi wajitetea kutumia mabomu

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa alisema polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutokana na mazingira ya tukio hilo.

Mpwapwa alifafanua kwamba, baada ya kuona wafuasi hao wakitoka nje ya Mahakama hiyo kwa mfumo wa maandamano huku wakizidi kuongezeka barabarani walizazimika kutumia njia hiyo ili kuwatawanya, lakini akakanusha jeshi hilo kutumia risasi za moto.

Aliweka bayana kwamba, ni uvumi wa mitaani kuwa wao walitumia risasi za moto, huku akisisitiza hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo na iwapo wafuasi hao wangetoka mahakamani hapo kama walivyoingia basi polisi wasingetumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

"Tumelazimika kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi kwa sababu walikua wakitoka mahakamani kwa mfumo wa maandamano huku wakisema, "Peoples Power."

"Kama wasingetumia mfumo huo kama walivyoingia sisi tusingepiga mabomu, lakini hatukutumia risasi za moto huo ni uvumi tu,"alisisitiza Mpwapwa.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili baadaye jana, zilisema tayari polisi imemfungulia jalada Godbless Lema kwa kuandamana bila kibali.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimetangaza kuanza maandamano kesho ikiwa ni mkakati wake kupinga kupanda bei ya umeme, malipo kwa kampuni tata ya kufua umeme ya Dowans na kushinikiza uwajibikaji baada ya mlipuko wa mabomu Kambi ya JWTZ, Gongo la Mboto.

Akizungumza nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, aliwaambia mamia ya wafuasi wa chama hicho baada ya kesi inayomkabili yeye na wafuasi wengine kuahirishwa, akisema katika maandamano hayo pia watazungumzia mauaji wa Arusha.

"Tunawashukuru sana kwa kuja mahakamani kutuunga mkono. Kama tulivyoahidi, yale maandamano ya nchi nzima yataanza Mwanza kesho kutwa (kesho) na baada ya hapo tutaenda mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema baada ya kumaliza Mkoa wa Mwanza watakwenda katika mikoa ya Mara, Shinyanga na Kagera huku akibainisha kuwa watakaa Kanda ya Ziwa kwa siku 10.
 
Nionavyo mimi hata JK kule Ivory Coast Mheshimiwa Gbagbo atamwita JK pembeni na kumuuma sikio na kumweleza kwa upole kabisa ya kuwa................................shut up JK.................because.............I still know what you did in your own country to stay in power.............If I, Gbagbo, stole that election you too did the same, boy...................................................
 
shut up JK..[/B]...............because.............I still know what you did in your own country to stay in power[/COIf I, Gbagbo, stole that election you too did the same, boy...................................................[/QUOTE]

"Yes, I did the samething, but my people are foolish and the forget easly compared to yours. My opponents are still weak and others have unconditional marriage with us,
and u sir!?"
 
Polisi waridhia maandamano ya Chadema

Wednesday, 23 February 2011

dk%20slaa%2021.jpg

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

Frederick Katulanda, Mwanza

Polisi mkoani Mwanza wameridhia maandamano yaliyoandaliwa na Chadema, kupinga malipo ya fidia kwa Kampuni ya Dowans, kuongezeka kwa gharama za maisha na kupanda kwa gharama za umeme.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi alisema tayari wamekwishakamilisha maandalizi ya maandamano hayo, yatakayofanyika leo kuanzia saa 8: 00 mchana na kufuatiwa na mkutano wa hadhara.

Maandamano ya Mwanza yanafanyika takriban miezi miwili tangu kutokee mauaji ya raia waliopigwa risasi na polisi mkoani Arusha, wakati walipokuwa wakizuia maandamano ya Chadema mkoani humo.

Katika tukio hilo la Januari 6, mwaka huu watu kadhaa walijeruhiwa, polisi wa Arusha walimwaga damu za watu kadhaa, walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chadema.

Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano ya Chadema, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Said Mwema ambaye awali aliyapiga marufuku baada ya kuwa yameruhisiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.

Jana Mushumbusi alisema maandamano ya Mwanza yatahitimishwa kwa mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini hapa kuanzia saa10:00 jioni.

Tayari Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amewasili jijini hapa kwa lengo la kushiriki maandamano hayo ya kwanza kufanyika Mwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, Oktoba 31 mwaka jana.

Dk Slaa aliwasili jijini Mwanza jana mchana. Viongozi wengine wa Chadema wanaotarajiwa kushiriki maandamano na baadaye mkutano ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Mushumbusi alisema mbali na viongozi wa taifa wa Chadema, wabunge wote wa chama hicho wanatarajiwa kuhudhuria maandamano hayo.

Aliwataka wapenzi, wanachama na Watanzania wote kwa ujumla wanaochukia ufisadi kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza kushiriki.

"Sisi maandalizi yetu yamekamilika na viongozi wote wa kitaifa wa chama na wabunge wote wa Chadema wamethibitisha kuhudhuria maandamano yetu ambayo yataanzia Kituo cha Mabasi cha Buzuruga, Nyakato na kupita Barabara ya Mwanza-Musoma, Nyerere, Kenyatta na kuingia Barabara ya Uwanja wa Ndege kwenda hadi katika Viwanja vya Furahisha," alifafanua katibu huyo wa Chadema.

Mushumbusi alisema kutokana na wao kufanya maandamano ya amani, chama chake kimeandika barua ya taarifa kwa Jeshi la Polisi na kuzingatia sheria ya kutoa taarifa kwa jeshi hilo saa 48 kabla ya kuandamana na wala siyo kuomba kibali.

"Barua ya kuwataarifu Jeshi la Polisi kuhusiana na maandamano tuliwakabidhi tangu Februari 20, mwaka huu na Jeshi la Polisi limekubaliana na maandamano yetu na njia ambazo tutapitia, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi, tutaendelea na maandamano yetu kama yalivyopangwa," alieleza Mshumbisi.

Katibu huyo alisema lengo la maandamano yao ni kupinga vitendo vya ufisadi, malipo ya Sh94 bilioni ya tozo kwa ajili ya kampuni ya Dowans, kupinga kupanda na kuongezeka kwa bei ya umeme nchini na kuongezeka kwa gharama za maisha.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu maandamano hayo, alisema jeshi lake limejipanga na kusema hawana tatizo na maandamano hayo na kwamba watahakikisha wanatoa ulinzi mkali kulinda watu wasio na nia njema kutumia mwanya huo kuzusha vurugu.

"Hatuna tatizo na maandamano, haya tumeridhia na kukubaliana ni wapi watapita, tumejipanga kwa ulinzi ili kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na salama kwa watu wengine na mali zao," alieleza Kamanda Sirro.

Wachunguzi wa mambo waliozungumzia maandamano hayo walisema huenda yakapata ushiriki wa watu wengi kutoka na mada ziliyopangwa kuzungumzwa, kuwagusa watu wengi.
 
Risasi za moto, mabomu zapigwa kuizima Chadema Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:27

arushalema.jpg
Moses Mashalla na Musa Juma, Arusha
MPAMBANO kati ya Jeshi la Polisi na wafuasi wa Chadema jana umetikisa tena Jiji la Arusha baada ya chombo hicho cha dola kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi kuwatanya mashabiki hao waliokuwa wakimsindikiza ofisini mbunge wao, Godbles Lema, akitokea mahakamani.

Tukio hilo limekuja takribani mwezi mmoja baada ya mpambano mkali kati ya polisi na wafuasi wa chama hicho chenye ngome kubwa ya kisiasa katika Ukanda wa Kaskazini, ambao ulisababisha mauaji ya watu wawili na majeruhi.

Jana mnamo saa 5:30 asubuhi, wakati wafuasi hao walipokuwa wakitokea kwenye Mahakama ya Hakimu Mfawidhi mkoani Arusha kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wakuu wa chama hicho, walianza kutembea barabarani wakiwa na mbunge wao huku wakimsindikiza kwa umbali wa kilomita tatu.

Wakiwa na mbunge huyo katika msafara wao, wafuasi hao walitembea kuanzia nje ya Mahakama Kuu na kupitia Barabara ya Uhuru, kisha kuingia Barabara ya Boma mkabala na ofisi za Mkuu ya Mkoa wakielekea kwenye ofisi za mbunge huyo.

Katika msafara huo wa kumsindikiza mbunge wao, wafuasi hao walisikika wakiimba nyimbo mbalimbali kumshutumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisema, "Waziri mkuu Pinda kaudanganya umma" pamoja na kumkataa Meya wa Arusha wakisema, "Hatumtaki Meya wa Arusha."

Hata hivyo, wakati wafuasi hao wakiwa katika barabara ya Boma mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Zuberi Mwombeji, walifika na magari mawili waliyoyatumia kuyakinga kwa mbele gari la mbunge huyo pamoja na wafuasi wao, kisha kuanza kufyatua risasi za moto hewani na mabomu ya machozi kuwatawanya.

Matumizi hayo ya risasi za moto na mabobu yalifanyika baada ya polisi kuona wafuasi hao walikaidi amri halali, iliyowataka kutawanyika kwa amani.

Katika tukio hilo, kiongozi huyo wa polisi alisikika akiamuru vijana wake akisema, "Pigeni pigeni," ndipo askari hao walianza kufyatua mabomu ya machozi na kurusha risasi za moto hewani.

Rekodi za Mwananchi ziliweza kuthibitisha kwamba, katika tukio hilo ilisikika milio sita ya mabomu ya machozi iliyolenga kuwatimua wafuasi hao wa Chadema huku polisi wakitumia magari hayo mawili moja likiwa na namba PT 1844 .

Hali hiyo iliwalazimisha wafanyabiashara waliokuwa karibu na eneo hilo kufunga maduka yao huku ofisi za Manispaa ya Arusha, zikifungwa kwa muda na baadhi ya watu wakionekana wakitoka nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kushuhudia huku wengine wakikimbia ovyo.

Raia wa kigeni watimua mbio

Raia mbalimbali wa kigeni walionekana wakitimua mbio nje ya Hoteli ya New Safari iliyopo mkabala na eneo hilo, huku baadhi ya wakazi wakihaha kutafuta maji kwa ajili ya kujinusuru na moshi wa mabomu ya machozi.

Hata hivyo, Lema alifika na baadhi ya wafuasi wa Chadema katika ofisi zake ndani ya jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambako baada ya polisi kutoweka, wafuasi wa chama hicho walisimama nje ya jengo hilo na kuanza kuimba nyimbo za uhuru, huku wakitoa kauli za kulilaani Jeshi la Polisi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu muda mfupi baada ya vurugu hizo, Lema alilaani polisi kuwasambaratisha wafuasi waliokuwa wakimsindikiza kuelekea ofisini kwake baada ya kutoka mahakamani akidai hapakuwa na ulazima wa kupiga risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.

Lema aonya mpasuko mkubwa kutokea

Hata hivyo, Lema alidai endapo viongozi wa Serikali wasipokubali ukweli na kushidwa kuutatua mgogoro wa Arusha huenda wakaiingiza nchi katika machafuko.

Akizungumzia sakata la kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuwa Waziri Mkuu kuwa aliudanganya umma, Lema alisema watakula sahani moja na kiongozi huyo.

"Nchi itaingia kwenye machafuko yasiyo na ulazima kama Tunisia endapo viongozi wetu serikalini wasipokubali ukweli na kutafuta namna ya kuutatua mgogoro huu,na suala la Waziri Mkuu bado tunakula naye sahani moja,"alisema Lema.

Polisi wajitetea kutumia mabomu

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa alisema polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutokana na mazingira ya tukio hilo.

Mpwapwa alifafanua kwamba, baada ya kuona wafuasi hao wakitoka nje ya Mahakama hiyo kwa mfumo wa maandamano huku wakizidi kuongezeka barabarani walizazimika kutumia njia hiyo ili kuwatawanya, lakini akakanusha jeshi hilo kutumia risasi za moto.

Aliweka bayana kwamba, ni uvumi wa mitaani kuwa wao walitumia risasi za moto, huku akisisitiza hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo na iwapo wafuasi hao wangetoka mahakamani hapo kama walivyoingia basi polisi wasingetumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

"Tumelazimika kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi kwa sababu walikua wakitoka mahakamani kwa mfumo wa maandamano huku wakisema, "Peoples Power."

"Kama wasingetumia mfumo huo kama walivyoingia sisi tusingepiga mabomu, lakini hatukutumia risasi za moto huo ni uvumi tu,"alisisitiza Mpwapwa.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili baadaye jana, zilisema tayari polisi imemfungulia jalada Godbless Lema kwa kuandamana bila kibali.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimetangaza kuanza maandamano kesho ikiwa ni mkakati wake kupinga kupanda bei ya umeme, malipo kwa kampuni tata ya kufua umeme ya Dowans na kushinikiza uwajibikaji baada ya mlipuko wa mabomu Kambi ya JWTZ, Gongo la Mboto.

Akizungumza nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, aliwaambia mamia ya wafuasi wa chama hicho baada ya kesi inayomkabili yeye na wafuasi wengine kuahirishwa, akisema katika maandamano hayo pia watazungumzia mauaji wa Arusha.

"Tunawashukuru sana kwa kuja mahakamani kutuunga mkono. Kama tulivyoahidi, yale maandamano ya nchi nzima yataanza Mwanza kesho kutwa (kesho) na baada ya hapo tutaenda mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema baada ya kumaliza Mkoa wa Mwanza watakwenda katika mikoa ya Mara, Shinyanga na Kagera huku akibainisha kuwa watakaa Kanda ya Ziwa kwa siku 10.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

1234

+1 #55 GILLIARD 2011-02-24 09:11 Mandamano yasio na madhara kwa Taifa na Wananchi kwa ujumla ni haki ya Kikatiba.
Jeshi la Polisi linaongozwa na watu hawana elimu ya kutosha nendeni kozi mujiongezee elimu.

Quote

+1 #54 fredy chokela 2011-02-24 07:34 Wewe kamanda wa polisi wa Arusha hata kama kufanya kazi hujui si uige kutoka kwa kamanda wa polisi Mwanza Silo, huoni leo Chadema wanaandamana Mwanza huku wakipewa ulinzi wa polisi kwanini wewe unaona suluhisho ni kuwapiga mabomu wananchi?? au kwakuwa unajua wa kukuajibisha hayupo, siku ya mwizi ni arobaini nafikili yako itafika tu!!!
Quote

0 #53 ndombolo 2011-02-24 01:54 Hivi hawa polisi hili neno 'people's power' linawatisha nini? Mafisadi wanaogopa sana nguvu ya watu, basi wajue penda wasipende inakuja na hawataweza kuizuia. Viongozi wamejaa woga na wasiwasi maana wameona wananchi tumewashitukia na hatuko tayari tena kudanganywa. Watatumia polisi na jeshi lakini 'people's power' lazima ishinde tu. Wamekataa kuangalia na kujali masilahi yetu wananchi, sasa tutawaonyesha kwamba sisi ndiyo tumeshika kwenye mpini na wao makali.
Quote

+1 #52 Thomas mlowe 2011-02-23 21:10 hayo ndio mambo lazima haki itendeke hapo hadi kieleweke hivi hao POLISI wanajua maana ya maandamano?mi na dhani hawana kazi hao polisi yaani nawaunga mkono CHADEMA daini haki mana tambueni kuwa hata nyerere alifanya hivyo bila kudai haki ya kuwa nchi yake inataka kuwa huru tusinge kuwa na uhuru,mana ningependa hao polisi wangeenda vitani hawana kazi,mana wanacho dai ni HAKI YAO waacheni jamani.
Quote

+2 #51 ponnela Ephraim 2011-02-23 19:56 Sioni kabisa umaana wa kutumia silaha za moto kwa kutuliza maandamano ya watu ambao wanafanya pasipo vurugu zozote.Labda niwakumbushe Polisi kwamba kazi yao ni kulinda amani na Raia wake,na siyo kusababisha vurugu kama walivyofanya Arusha kwa mara nyingine.Raia daini haki zenu pasipo kuleta vurugu zozote na vilevile kumsindikiza mtu mkiwa katika kikundi sio kuandamana.
Quote

+1 #50 mie 2011-02-23 19:09 Hizo HERUFI KUBWA zinakera. andika tu kawaida kama una hoja tutaisoma. binafsi nikioma comment iliyojaa maherufi kubwa nairuka kwani nahisi mwandishi hajiamini mpaka apayuke
Quote

+1 #49 Mtanzania 2011-02-23 18:52 NIA YANGU NI NJEMA, TUMUONDOE KIKWETE MADARAKANI BASI!!!! ANAENDA IVORY COAST NDIKO WALIKOMCHAGUA?? BADALA YA KUSHUGHULIKIA YA ARUSHA ANAHANGAIKIA YA WATU?! ITAMTOKEA PUANI. AMINI AMIN NAWAAMBIENI, JOGOO HATAWIKA KABLA JK HAJATUUZA WATANZANIA.
Quote

+1 #48 Kifaru 2011-02-23 17:53 TUPAMBANE MPAKA KIELEWEKE!"LETS PROTEST TILL REGIME WILL STEP DOWN".
Quote

0 #47 TARIMO 2011-02-23 17:51 huyo naye anayesema hmna kazi ya kufanya hiyo pia ni kazi ya kuleta maendeleo wanatetea haki yao ya msingiNYIE NAYE ROPOKA KUHUSIANA NAWATU WA ARUSHA MKOME KABISA TENA MNYAMAZE KIMYA,
Quote

0 #46 TARIMO 2011-02-23 17:43 KWANI WAMEANDAMANA? NYINYI MNAJUA MAANA YA MAANDAMANO? WAO WAMEMSINDIKIZA MBUNGE WAO KAMA HAMJUI MAANA YA MAANDAMANO MSEME MUAMBIWE SIO KUONGEA OVYO OVYO
Quote

-4 #45 mwana 2011-02-23 16:51 Quoting kachike:
HONGERA POLISI KWA KAZI NZURI.HAO CHADEMA WAKIRUDIA KUANDAMANA NYIE FANYENI KAZENI YENU,NAAMINI MNA MABOMU YA MACHOZI NA MAJI YA KUWASHA YA KUTOSHA.WATU WA ARUSHA TUNATAKA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA YA AMANI.ANAEONA HANA KAZI ZA KUFANYA ZAIDI YA MAANDAMANO NA SIASA ZISIZOKWISHA ATAFUTE PA KWENDA. HUYO MEYA WA CCM NI MTU WA ARUSHA NA NI MTANZANIA.KWANI MEYA WA ARUSHA LAZIMA ATOKE CHADEMA?SUBIRINI HADI 2015.

ishu siyo diwani. ni utaratibu. kuandmana ni haki. wewe ni fisadi? pole lakini tutakendelea kuwafichua na wenzako wote.

Quote

-4 #44 arusha 2011-02-23 16:45 Quoting Debora:
Quoting Caroline:
Ndugu zangu za Arusha acheni maandamano yasiyokuwa na maana. Acheni kupoteza muda mwingi kwa ajili ya ushabik. Hivi huo muda wa malumbano mnautoa wapi? hamna kazi za kufanya. Jamani wakati wa malumbano/kampeni za kisiasa umekwisha kilichobaki ni kukaa na kutafari ni nini cha kufanya kwa maendeleo yenu na ya nchi kwa ujumla. Angalieni mtapoteza maisha yenu pamoja na viumbe visivyokuwa na hatia (watoto). Wakati wahusika wakiona vita vimepamba moto wanchapa zao mwendo wanaondoka kabisa nchini nyie mtauwana wenyewe, acheni kufanya nchi iwe Dafuu

Nakubaliana nawe shosti kuwa tutafakari jinsi ya kuleta maendeleo ya nchi yetu, na ndicho tunachokifanya sasa hivi.
Ndiyo maana tunajadili jinsi ya kuikomboa nchi yetu na raslimali zake kutoka kwenye mikono michafu ya mafisadi wa ndani na nje.

Kumbuka kuwa kukusanyika na kuandamana ni haki ya kikatiba.
Karibu Shosti tushirikiane kutetea haki zetu na raslimali za nchi yetu...

SINA CHA KUONGEZA. UMEMJIBU KISOMI. HAKI INAOMBWA AU INADAIWA? INADAIWA, CHADEMA TUKAZE BUTI. HATA NYERERE ALIFANYA HIVI. MANDELA ALIFUNGWA MASIKA 27, WENGINE WALIKUFA, POLISI WATUUWE WOTE KAMA WANATAKA KUPOTEZA HAKI. VINGINENYO ITAPATIKANA TU. ALUTA CONTINUE

Quote

0 #43 Debora 2011-02-23 15:50 Quoting Caroline:

-6 #42 kachike 2011-02-23 15:26 HONGERA POLISI KWA KAZI NZURI.HAO CHADEMA WAKIRUDIA KUANDAMANA NYIE FANYENI KAZENI YENU,NAAMINI MNA MABOMU YA MACHOZI NA MAJI YA KUWASHA YA KUTOSHA.WATU WA ARUSHA TUNATAKA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA YA AMANI.ANAEONA HANA KAZI ZA KUFANYA ZAIDI YA MAANDAMANO NA SIASA ZISIZOKWISHA ATAFUTE PA KWENDA. HUYO MEYA WA CCM NI MTU WA ARUSHA NA NI MTANZANIA.KWANI MEYA WA ARUSHA LAZIMA ATOKE CHADEMA?SUBIRINI HADI 2015.
Quote

+2 #41 makongo 2011-02-23 15:05 Sheria zipo ili zifuatwe siyo zivunjwe bila sababu yoyote. wanahabari ni wajibu wenu kutoa elimu ya sheria na umuhimu wake siyo kuegemea upande wowote hapa ni kwetu lazima pawe salama hata kama upendi.
Quote

1234
Refresh comments list
 
Risasi za moto, mabomu zapigwa kuizima Chadema Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:27

arushalema.jpg
Moses Mashalla na Musa Juma, Arusha
MPAMBANO kati ya Jeshi la Polisi na wafuasi wa Chadema jana umetikisa tena Jiji la Arusha baada ya chombo hicho cha dola kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi kuwatanya mashabiki hao waliokuwa wakimsindikiza ofisini mbunge wao, Godbles Lema, akitokea mahakamani.

Tukio hilo limekuja takribani mwezi mmoja baada ya mpambano mkali kati ya polisi na wafuasi wa chama hicho chenye ngome kubwa ya kisiasa katika Ukanda wa Kaskazini, ambao ulisababisha mauaji ya watu wawili na majeruhi.

Jana mnamo saa 5:30 asubuhi, wakati wafuasi hao walipokuwa wakitokea kwenye Mahakama ya Hakimu Mfawidhi mkoani Arusha kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wakuu wa chama hicho, walianza kutembea barabarani wakiwa na mbunge wao huku wakimsindikiza kwa umbali wa kilomita tatu.

Wakiwa na mbunge huyo katika msafara wao, wafuasi hao walitembea kuanzia nje ya Mahakama Kuu na kupitia Barabara ya Uhuru, kisha kuingia Barabara ya Boma mkabala na ofisi za Mkuu ya Mkoa wakielekea kwenye ofisi za mbunge huyo.

Katika msafara huo wa kumsindikiza mbunge wao, wafuasi hao walisikika wakiimba nyimbo mbalimbali kumshutumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisema, “Waziri mkuu Pinda kaudanganya umma” pamoja na kumkataa Meya wa Arusha wakisema, “Hatumtaki Meya wa Arusha.”

Hata hivyo, wakati wafuasi hao wakiwa katika barabara ya Boma mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Zuberi Mwombeji, walifika na magari mawili waliyoyatumia kuyakinga kwa mbele gari la mbunge huyo pamoja na wafuasi wao, kisha kuanza kufyatua risasi za moto hewani na mabomu ya machozi kuwatawanya.

Matumizi hayo ya risasi za moto na mabobu yalifanyika baada ya polisi kuona wafuasi hao walikaidi amri halali, iliyowataka kutawanyika kwa amani.

Katika tukio hilo, kiongozi huyo wa polisi alisikika akiamuru vijana wake akisema, "Pigeni pigeni," ndipo askari hao walianza kufyatua mabomu ya machozi na kurusha risasi za moto hewani.

Rekodi za Mwananchi ziliweza kuthibitisha kwamba, katika tukio hilo ilisikika milio sita ya mabomu ya machozi iliyolenga kuwatimua wafuasi hao wa Chadema huku polisi wakitumia magari hayo mawili moja likiwa na namba PT 1844 .

Hali hiyo iliwalazimisha wafanyabiashara waliokuwa karibu na eneo hilo kufunga maduka yao huku ofisi za Manispaa ya Arusha, zikifungwa kwa muda na baadhi ya watu wakionekana wakitoka nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kushuhudia huku wengine wakikimbia ovyo.

Raia wa kigeni watimua mbio

Raia mbalimbali wa kigeni walionekana wakitimua mbio nje ya Hoteli ya New Safari iliyopo mkabala na eneo hilo, huku baadhi ya wakazi wakihaha kutafuta maji kwa ajili ya kujinusuru na moshi wa mabomu ya machozi.

Hata hivyo, Lema alifika na baadhi ya wafuasi wa Chadema katika ofisi zake ndani ya jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambako baada ya polisi kutoweka, wafuasi wa chama hicho walisimama nje ya jengo hilo na kuanza kuimba nyimbo za uhuru, huku wakitoa kauli za kulilaani Jeshi la Polisi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu muda mfupi baada ya vurugu hizo, Lema alilaani polisi kuwasambaratisha wafuasi waliokuwa wakimsindikiza kuelekea ofisini kwake baada ya kutoka mahakamani akidai hapakuwa na ulazima wa kupiga risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.

Lema aonya mpasuko mkubwa kutokea

Hata hivyo, Lema alidai endapo viongozi wa Serikali wasipokubali ukweli na kushidwa kuutatua mgogoro wa Arusha huenda wakaiingiza nchi katika machafuko.

Akizungumzia sakata la kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuwa Waziri Mkuu kuwa aliudanganya umma, Lema alisema watakula sahani moja na kiongozi huyo.

“Nchi itaingia kwenye machafuko yasiyo na ulazima kama Tunisia endapo viongozi wetu serikalini wasipokubali ukweli na kutafuta namna ya kuutatua mgogoro huu,na suala la Waziri Mkuu bado tunakula naye sahani moja,”alisema Lema.

Polisi wajitetea kutumia mabomu

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa alisema polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutokana na mazingira ya tukio hilo.

Mpwapwa alifafanua kwamba, baada ya kuona wafuasi hao wakitoka nje ya Mahakama hiyo kwa mfumo wa maandamano huku wakizidi kuongezeka barabarani walizazimika kutumia njia hiyo ili kuwatawanya, lakini akakanusha jeshi hilo kutumia risasi za moto.

Aliweka bayana kwamba, ni uvumi wa mitaani kuwa wao walitumia risasi za moto, huku akisisitiza hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo na iwapo wafuasi hao wangetoka mahakamani hapo kama walivyoingia basi polisi wasingetumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

“Tumelazimika kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi kwa sababu walikua wakitoka mahakamani kwa mfumo wa maandamano huku wakisema, “Peoples Power.”

"Kama wasingetumia mfumo huo kama walivyoingia sisi tusingepiga mabomu, lakini hatukutumia risasi za moto huo ni uvumi tu,”alisisitiza Mpwapwa.

Back
Top Bottom