Averos
JF-Expert Member
- Aug 6, 2010
- 993
- 695
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi wilayani Songea, mkoani Ruvuma limezuia kufanyika kwa maandamano ya amani yaliyoitishwa na Chadema wilayani humo jana yenye lengo la kupinga uamuzi wa mkuu wa wilaya hiyo, Thomas Oley Sabaya, wa kuwanyima vocha za pembejeo za kilimo wakulima wa kata tisa kati ya kata 21 za Halmashauri ya Manispaa ya Songea zikiwemo kata 5 zinazoongozwa na Madiwani wa Chadema.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za Chama hicho zilizopo Mfaranyaki mjini hapa, Mwenyekiti Chadema mkoa wa Ruvuma, Joseph Fuime, alisema kuwa Chadema wilaya ya Songea walipanga kufanya maandamano ambayo yalikuwa na madhumuni ya kupinga uchakachuaji wa vocha za pembejeo za wakulima uliofanywa na mkuu wa Wilya Sabaya
Fuime ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mjini kupitia Chadema, alisema kuwa taarifa ya kufanya maandamano hayo ilitolewa tangu Januari 7, mwaka huu kwa mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Songea, lakini ameshangaa kuona mkuu huyo wa polisi amethibitisha kufanya maandamano hayo kwa madai kuwa tatizo la wakulima kunyimwa vocha linashughulikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma.
Ameeleza zaidi kuwa pamoja na Polisi kuzuia maandamano hayo kupitia barua yao iliyowafikia jana na kusainiwa na OCD Peter Kubezya yenye kumb,Na,SO/A.3/6/54, Chadema iliruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara ambao ulifanyika kwenye soko la Samaki la zamani karibu na Shule ya Msingi Mfaranyaki
Alieleza zaidi kuwa sababu zilizotolewa na OCD Peter Kubezya ni dhaifu na zilizozeeka na kwamba Dk. Ishengoma alipaswa kuchukua hatua za haraka kuwakomboa wakulima toka pale tatizo lilipojitokeza Desemba 15, mwaka jana lililofanywa kwa makusudi na DC Sabaya ambapo maamuzi ya ajabu ya kukiukwa kikao cha wadau wa kilimo kilichofanyika Novemba 12, mwaka jana ambacho kiliazimia kuwa wakulima wa kata za Manispaa ya Songea wakachukulie vocha za mbolea ya ruzuku kwenye maeneo yao wanayoishi ambapo kuna kamati za pembejeo za kata ambazo zinawafahamu wakulima husika
Fuime alisema kuwa Polisi wanapaswa kulinda raia na mali zao na kwamba hawapaswi kutumia uwepo wao kuwadhulumu wananchi haki zao, ikiwemo ya kupewa mbolea katika kata zinazoongozwa na madiwani wa Chadema za Mjini, Lizaboni, Majengo, Bombambili na Misufini na kata nyingine nne za Matarawe, Mjimwema, Ruvuma na Seedfarm.
Idadi kubwa ya skari polisi walikuwa wamemwagwa kwenye eneo la mkutano na wengine wakiwa wanazunguka kwenye magari yao wakiwa na silaha mbalimbali toka saa 5:00 asubuhi kabla ya mkutano uliopangwa kuanza saa 10: alasiri.
Hata hivyo, jitihada za kumpata OCD Kubezya hazikuweza kufanikiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alipohojiwa kwa njia ya simu alikana jeshi lake kuzuia maandamano hayo, lakini katika barua yake aliyoiandikia Chadema ambayo gazeti hili limefanikiwa kupata nakala yake, OCD Kubezya amempelekea nakala Kamuhanda, DC Sabaya na Afisa Usalama wa wilaya.
NIPASHE