Maandamano ya CHADEMA yaanza kutoa matunda, makali ya maisha sasa kupunguzwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya CHADEMA yaanza kutoa matunda, makali ya maisha sasa kupunguzwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 17, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  yale maandamano ya chadema sasa yameanza kutoa matunda baada ya Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya M Kikwete kuagiza msamaha wa kodi katika bidhaa mbalimbali utolewe lengo likiwa ni kupunguza ukali wa maisha kwa watanzania,ikumbukwe vizuri kwamba ukali wa maisha ilikuwa ni ajenda kubwa ya chadema hivi karibuni na sasa kero hiyo na nyinginezo sasa zitaanza kuwa na ahueni kama sio kwisha kabisa,

  habari kamili kama ilivyoripotiwa na magazeti ya leo

  RAIS Jakaya Kikwete ameingilia kati bei ya bidhaa kupanda nchini, hivyo kuiagiza Wizara ya Fedha na Uchumi kupunguza mfumuko wa bei. Amesema ikiwezekana, wizara itoe msamaha wa kodi ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha.

  Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana, mjini Dar es Salaam, alipotembelea makao makuu ya wizara hiyo na taasisi zilizo chini yake, ambapo alizungumza na watendaji. Alisema licha ya wizara kufanya vizuri katika makusanyo ya kodi, inapaswa kuangalia namna ya kupunguza mfumuko wa bei, ili kutoa nafuu ya maisha kwa Watanzania.

  "Ikiwezekana angalieni namna ya kupunguza kodi, ingawa hilo linaweza kutupunguzia mapato lakini inafaa kufanya hivyo ili kutoa ahueni ya maisha kwa wananchi," alisema.

  Katika ukusanyaji kodi, alisema wizara imefikia lengo la serikali, ambapo Desemba, mwaka jana ilikusanya zaidi ya sh. bilioni 500. Hata hivyo, alisema ni vyema ikageukia katika kuinua uchumi wa nchi, hususan kupunguza mfumuko wa bei ili mwananchi wa kawaida apate nafuu ya maisha.

  Aliitaka pia wizara kujikita katika kuzipa nguvu sekta zenye mchango mkubwa katika ukuaji uchumi.

  MADENI YA WASTAAFU
  Rais Kikwete ameitaka wizara hiyo kumaliza malipo ya madeni ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), ili serikali iondokane na mzigo wa kudaiwa na wazee hao.

  Alisema juhudi kubwa zimefanywa na wizara katika kuwalipa wastaafu hao na kwamba, waliosalia ni wachache.


  Kutokana na hilo, alisema ni vyema
  wakalipwa haraka ili kuondokana na mzigo wa kudaiwa.

  "
  Hili la wastaafu wa Afrika Mashariki nalo limalizeni, hatuwezi kuendelea nalo siku zote, walipeni," alisema.

  MALIPO YA WALIMU

  Akizungumzia malipo ya walimu, rais Kikwete aliitaka wizara kuwa na utaratibu mzuri wa kuwalipa, hususan wanaoripoti vituoni kwa mara ya kwanza, ili kuepusha usumbufu wa kudai stahili zao.

  Kwa mujibu wa rais Kikwete, wizara imeweza kurekebisha kwa kiasi kikubwa kasoro ya ucheleweshaji mishahara ya watumishi wa umma.

  Hata hivyo, alisema bado tatizo la walimu wapya kutolipwa kwa wakati linaendelea, hivyo linapaswa kushughulikiwa ili lisijirudie.

  Alirejea agizo la kuzuia uhamisho wa watumishi, pale inapokuwa hakuna maandalizi, ikiwemo fedha. Alisema ofisa yeyote wa serikali atakayehusika kufanya hivyo bila maagizo achukuliwe hatua za kinidhamu, ikiwemo kukatwa mshahara.

  Kuhusu maslahi ya watumishi wa serikali, aliiagiza wizara hiyo kuangalia uwezekano wa kuwadhamini wafanyakazi katika taasisi za fedha ili wapate mikopo kwa urahisi.

  Rais Kikwete alisema ili kuwasaidia watumishi hao kujiongezea kipato, ni vyema wizara ikaandaa utaratibu wa kuwadhamini katika taasisi za fedha, hususan wale wenye muda mrefu wa kuendelea kuitumikia serikali.

  Aliagiza kuharakishwa mchakato wa kupatikana Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali, atakayehusika na usimamizi wa fedha za halmashauri, ili kukabiliana na ubadhirifu.

  Rais Kikwete alisema Naibu Mhasibu Mkuu atahusika moja kwa moja katika usimamizi wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri.

  Wizara pia imetakiwa kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani na idara za serikali, ili wafanye kazi kwa uhuru bila kuingiliwa.

  "Wakaguzi wa ndani wasiwe wanawajibika kwa makatibu wakuu, kwa kuwa wao nao ni miongoni mwa wanaochunguzwa, hivyo wakiwa wanawajibika kwao watakosa uhuru wa kufanya kazi vizuri," alisema.

  ZIARA TRA

  Akiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), rais Kikwete alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa uongozi wa mamlaka hiyo.

  Katika hatua nyingine, akiwa mlangoni akitoka ofisi hizo, alilazimika kusimama kuwasikiliza watu waliokuwa wakipaza sauti kumuomba asikilize kilio chao.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Joseph Mwakalinga, aliyejitambulisha kuwa mfanyabiashara ya magari kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, alimuomba rais kuingilia kati suala la kutozwa ushuru mara mbili.

  Mwakalinga alisema TRA huwatoza kodi wanapoingiza gari kutoka Zanzibar, licha ya kuwa lilikwishalipiwa visiwani humo.

  Rais Kikwete aliwataka kuunda umoja na aliahidi kukutana nao wiki hii ili kusikiliza matatizo yao.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tutaendelea kuwabana tu hawa wamelala usingizi wa pono wakiota ndoto za kifalme. ndo maana ukiwakosoa wanakimbilia kusingizia uhaini
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA bado tunataka maandamano zaidi nchini ili gharama ya maisha yapungue zaidi pamoja na kwamba tayari matunda ya kazi yenu imeanza kuonekana nchini.

  Mwezi Aprili ndio huo hivyo maandamano zaidi yaendelee kwa ajili ya kushinikiza kutungwa kwa Katiba Mpya kwa kushrikisha wananchi moja kwa moja na kwa kupitia bungeni, wananchi sisi kujipangia wenyewe ratiba ya mabadiliko yoto tunayoyahitaji nchini kuweza kukamilishwa kabla ya uchaghuzi mkuu 2015 na pia kudai Tume Huru ya Uchaguzi nchini.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Punguzo lolote la kodi litamnufaisha mfanyabiashara wa kati na siyo mlaaji wa mwisho. Mtakumbuka VAT ilipungua toka 20% hadi 18% nani mwenye ushahidi wa bidhaa yoyote iliyopungua bei? Watoa huduma kama Tanesco, Internet ndio pekee ambao punguzo lilionekana.
   
 5. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  umeona eeh?
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unashauri maandamano yaendelee ili serikali iweze kuamka kutoka usingizini na nchi iweze kupiga hatua zaidi au yasitishwe?
   
 7. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Our president is again creating another tax evasion loopholes by suggeting to TRA kupunguza kodi.
  Kwa nini asipunguze unnecessary expinditures ktk wizara zake? Kama kuacha kununua magari ya anasa nk.
   
 8. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye nyekundu parekebishe kidogo niweze kujibu swali lako
   
 9. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni mwendelezo wa aliyoyahaidi tu, kama ni maandamano yamemshurutisha kama unavyodai mbona mnaandamana kwa mengi yote ameshayafanya?

  Kwa wakati wake na ratiba zake za chama na serikali ndio anafanya kutimiza aliyotuahidi wananchi wake. Hizo ni chuki binafsi kwa rais
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Samahani ndugu kwani wewe ndio yule ushomile Salva Rweyemamu, anaemdanganya mkwere kila siku pale magogoni? maana alishawahi kumdanganya eti foleni kubwa za magari Dar es salaam ndio dalili ya maisha bora, kumbe barabara chache na miundombinu mibovu.

  Huyu Mkwere hata kama tutamvumilia amalize hii miaka mitano ingawa siamini hivyo, basi kikombe walichopitia akina Chiluba, Bakili Muluzi na Jaques Chiraq wa France, akihepukiki kwake. lazima amalizie uzee wake jela.

  No merci to the criminal
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  aaanze na kupunguzwa kwa bei ya umeme
   
 12. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  do u think your suggestions will work out?
   
 13. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PAmoja na kuendelea kupigilia misumari kwenye kero wanazo zikabili wananchi, Pia Ningependa CDM Wawaeleze Wananchi yale maeneo muhimu ya Katiba ambayo yanahitajika kubadiliswa wakionyesha faida na hasara zake. KWa kufanya Hivyo Maandamano yatakuwa elimu kubwa kwa Mtanzania wa maisha ya chini hasa wale wasio na elimu ya uraia.
  mbarikiwe na bwana
   
 14. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  i agree with you
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kheeee Kheeee Kheeeee, What a waste!!!
   
 16. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Jamani eh, hiki kitakuwa ni kichekesho cha mwaka. TRA wala taasisi nyingine yoyoyte haiwezi kupunguza kodi. Kodi zinawekwa kisheria kupitia bunge. Ni bunge pekee linaloweza kufuta au kupunguza viwango vya kodi. Waziri husika anaweza kurekebisha viwango kama sheria iliyopitishwa na bunge inamruhusu kufanya hivyo. Hivyo JK kuzunguka maofisini anatoa maagizo kuhusu kodi ni ama rais wetu amechoka au ni msanii wa kutupwa.
   
 17. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  so what should be done? mbona hamkosi kukosoa,akifanya hivi mnasema angefanya vile,pengine angefanya vile mnavotaka pia msingekosa sababu bado mngesema atafanya vile??
   
 18. s

  seniorita JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Maandamano ndio dawa pekee na nguvu ya mwananchi; a forum to say or demonstrate our frustrations; else there is no way they can hear and address critical areas of life kwa Mtanzania wa kawaida maana kutokuwa na umeme, kupanda kwa gharama za umeme na chakula etc, sio issues za matajiri na watawala; they can afford even to lunch in France and shop and come back the same day wakati sisi walalahoi hata mlo mmoja wa maana shida....bado eti tunanyamaza kimya?
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Tuanze kushangilia "maisha bora kwa kila mtz asa yamewezekana'.....hahahahahahahaahaaaaaaaaaaaaaaaaaa......kikwete safi sana aisee kumbe kikwete noma eeeeeeeee.............hakuna kulipa kodi tena teheteheteheeeeeeeeeeeeee.....
   
 20. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  MKWERE KASHIKWA PABAYA:juggle::smash:
   
Loading...