Maandamano ya Chadema ni haki yao kama ilivyo kwa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya Chadema ni haki yao kama ilivyo kwa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Dec 26, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninashangazwa na wanasiasa na wapambe wa CCM wanaowawekea vikwazo na kuwanyoshea kidole Chadema eti waachane na mpango wa maandamano kwa madai kuwa watanzania hawana utamaduni huo. Naipongeza Chadema kwa kuandaa maandamano ya kupinga ongezeko la asilimia 18.5 ambao wengi wamehusisha ongezeko hilo na ufisadi wa Dowans na Richmond. Haya ni maandamano muhimu sana ya kupinga sera dhalimu za CCM zinazowaumiza wananchi. Kazi ya vyama vya siasa ni kuuza sera. Kwa kuandaa maandamno ya kupinga ongezeko hilo, Chadema inawaunga mkono vilivyo wananchi wa Tanzania ambao wanaumizwa sana na sera za kinyonyaji za CCM. Haya ni maandamano muhumu sana kwetu sisi wananchi. Kitu cha kushangaza ni kuwa CCM huundaa maandamano ya kuunga mkono hotuba za wanasiasa wao akiwemo mwenyekiti wa taifa wa CCM. Ni hivi karibuni tu CCM walitangaza maandamano kupitia TBC1 na kuyafuta baada ya dakika tano. Chadema wasirudie kosa la kuacha kuwaongoza na kuwahimiza wananchi kupinga udhalimu wa CCM kama walivyofanya kwa kuahirisha maandamano ya kupinga uchakachuaji wa kura za urais. Kwa kuahirisha maandamano CCM wamepata kichwa cha kuendelea kuwanyima watanzania haki yao ya kuongozwa na viongozi waliowachagua. Kilichotoa Arusha cha CCM kubaka demokrasia katika uchaguzi wa Meya wa Arusha kisingetokea kama Chadema wangeitisha maadamano mapema ya kupinga urais wa kura za kuchakachua. Wenzetu wa Ivory Coast karibu wanafanikiwa kumrudisha rais waliyemchagua kwa vile wameungwa mkono na jumuia ya kimataifa ikiwemo jumuia ya nchi za Afrika Magharibi. Kilichotokea Arusha ni mwendelezo wa wimbi la CCM kuvunja utawala wa sheria. Wakati CCM wakitenda kinyume na utawala wa sheria, waziri mkuu Mizengo Pinda yeye anauona utawala wa sheria kwa kuunga mkono watanzania wawalipe mafisadi wa Dowans. Tuwaunge mkono Chadema katika maandamano ya kuwatetea wananchi kwa sababu ni chama cha siasa sawa na CCM. Chadema wanahaki ya kuandamana kama CCM wanavyoandaa maandamano kuunga hotuba za wanasiasa wao.
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Pasi[o haki hapana amani . Ukizuia maandamano wana wanaendelea kujadili majumbani na kuchafua amani
   
 3. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hili wazo la maandamano,coz naamini ni moja ya njia ya kuamsha hasira za wananchi dhidi ya utawala dhalimu wa ccm.Wamezidi kutufanya mabwege,kupitia maandamano haya na mengine yote yatakayo andaliwa kupinga udhalimu wao tuwafahamishe kuwa we are no longer mabwege.Shime watz wenzangu tujitokeze kwa wingi ktk maandamano haya.Narudia wito wangu kwa TUCTA,kuwa wao wangeitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima ili kufikisha ujumbe kwa jk na mafisadi wenzake kuwa tumechoshwa na michezo yake ya kuigiza kwenye masuala nyeti ya taifa letu!WAO WANA PESA,SISI TUNA MUNGU...!
   
Loading...