Maandamano ya CHADEMA kesho yasitishwa ghafla na IGP baada ya awali kukubalika

Tunaandamana na hatutaogopa vitisho vya polisi. Kazi yao ni kulinda amani na siyo kutoa taarifa kwamba amani itavunjwa!! Hii nchi wameigeuza ni bedroom yao, wanaamua wanavyotaka! Sasa kesho hatuachi kuandamana; Mh. Freeman ataanzia Philips, Mh. Slaa ataanzia Mbauda! Wabunge zaidi ya 30 na Madiwani zaidi ya 100 kutoka Manyara, Moshi, Hai, Rombo, Moshi Vijijini, Arusha, Arumeru etc watahudhuria! Hatuwezi kudhulumiwa kwa kutumia mgongo wa uvunjifu wa amani! Hakuna amani itakayovunjika! Labda polisi waivunje wao!

The strategy employed ni ya kijinga, zuia maandamano, chadema watalazimisha, tuwapige mabomu, mkutano wao utaharibika, tutumie media kuonyesha chadema wavunjifu wa amani! Upuuzi mtupu!
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ametangaza kusitisha maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendelieo CHADEMA yaliyokua yaongozwe na FREEMAN MBOWE na DR WILBROAD SLAA kwa kile alichokieleza kua ni taarifa za kiinteligensia kwamba kutakua na uvunjifu wa amani.
KWENU WADAU

Kama kweli wamepata fununu hizo basi IGP yuko sahihi kabisa kusimamisha maandamo kwa interest za nchi yetu kuhakikisha amani yetu inaendelea
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ametangaza kusitisha maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendelieo CHADEMA yaliyokua yaongozwe na FREEMAN MBOWE na DR WILBROAD SLAA kwa kile alichokieleza kua ni taarifa za kiinteligensia kwamba kutakua na uvunjifu wa amani.
KWENU WADAU

.
Intellegence? Nchi imefisadiwa mpaka imebaki mfupa mtupu hakuna cha intellegensia wala ndugu yake. Ila wakisikia tu jambo linafanywa na upinzani hata kama ni haki yao ya kikatiba utasikia hawa wavivu wa kufikiri wanakuja na upuuzi wao walioupata kwenye vijiwe vya gahawa wanakuja nao hadharani kwamba ni habari za kiintellegensia.
Shame shame shame every where in our country.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ametangaza kusitisha maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendelieo CHADEMA yaliyokua yaongozwe na FREEMAN MBOWE na DR WILBROAD SLAA kwa kile alichokieleza kua ni taarifa za kiinteligensia kwamba kutakua na uvunjifu wa amani.
KWENU WADAU


majambazi wanapora mali za watu, sijawahi kusikia taarifa za kiintelijensia

mafisadi wanakwapua mabilioni kila leo, sijawahi kusikia taarifa za kiintelijensia

ccm walichakachua ushindi wa slaa, sikuwahi kusikia taarifa za kiintelijensia.

lakini wananchi wakitaka kuandamana utasikia hizi crap za polisi wetu.

taarifa za kiintelijensia au mumeagizwa na kina EL?? mafisadi?
 
Its too shame for police.Intelligence report could help them to stand firm and cut it off before happening on the ground.No need to have police force in tz.Why??
 
Kama Chadema ni wanapinduzi na mageuzi wa kweli basi wathubutu kama Cuf walivyothubutu.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ametangaza kusitisha maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendelieo CHADEMA yaliyokua yaongozwe na FREEMAN MBOWE na DR WILBROAD SLAA kwa kile alichokieleza kua ni taarifa za kiinteligensia kwamba kutakua na uvunjifu wa amani.
KWENU WADAU

Hawa ni watawala punguwani na vipofu wa fikra.
wanadhani wanaweza kuiokoa CCM iliyooza na inayokufa kwa kuzuia CHADEMA isijiimarishe au kutekeleza majukuma ya kulikomboa taifa! kamwe hilo hawaliwezi.

Na ni kwanini hawaizuii CCM, Chama chao cha mafisadi? wao mbona wanafanya wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kubebwa na wauza unga, wabebaji, na IGP na kundi lake la inteligensia ya kisanii hawana kauli yoyote?

Kwanza wale watawala wa jeshi lake ambao mzee Mengi alimzidi IGP inteligensia na kumpa majina ya makamanda wake wabebaji na washiriki waku wa biashara ya unga, IGP atatueleza nini?

Yeye afadhali ajitulize kimya huko kunako sentro, au akamlinde Shem popote aendapo na sio kuhujumu umma.
 
Mimi nashangaa sana, ujambazi umeshamiri watu hatuishi kwa usalama watu wanakufa waliomuua jaji mwaikasu mpaka leo hawajapatikana huyu mwema hapati taarifa za kiintelijensia kwenye mambo yanayomgusa mtanzania isipokua ya chadema na cuf? Mbona ya ccm yanaruhusiwa? Huu ni ushenzi sisi tuingie mtaani tuone kitakachokua tumechoka kuwaacha kikwete na familia yake ya wakina mwema kututawala kama wafungwa, huuni uhaini kabisa
 
Shemeji mwema elimu yako hipo wapi? Itumie. Wacha kuendeshwa kaka fimbo ulichapwa wewe shule. Uer not in good history ya nchi hii hukufanya zuri lolote sijaona kiukweli. Hivi una tv home kwako? Uoni wenzetu uraya mbona maandamano yapo jamani ehh.
 
Tunaandamana na hatutaogopa vitisho vya polisi. Kazi yao ni kulinda amani na siyo kutoa taarifa kwamba amani itavunjwa!! Hii nchi wameigeuza ni bedroom yao, wanaamua wanavyotaka! Sasa kesho hatuachi kuandamana; Mh. Freeman ataanzia Philips, Mh. Slaa ataanzia Mbauda! Wabunge zaidi ya 30 na Madiwani zaidi ya 100 kutoka Manyara, Moshi, Hai, Rombo, Moshi Vijijini, Arusha, Arumeru etc watahudhuria! Hatuwezi kudhulumiwa kwa kutumia mgongo wa uvunjifu wa amani! Hakuna amani itakayovunjika! Labda polisi waivunje wao!

The strategy employed ni ya kijinga, zuia maandamano, chadema watalazimisha, tuwapige mabomu, mkutano wao utaharibika, tutumie media kuonyesha chadema wavunjifu wa amani! Upuuzi mtupu!

umeeleweka vizuri kamanda.
Na kama kuna mtu ataibuka na kuleta maswali yasiyo na msingi basi atakuwa hakutahiriwa hospital au alikeketwa.
 
Wakati Richmond ikiwa ghost company - hakuna taarifa za kiintelijensia ( i repeat Ki.i.n.t.e.l.i.j.e.n.s.i.a)
,, ,, ,, Meremeta inakula nchi - ,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,, !!!!!!
,, ,, ,, Buzwagi scandal - ,,,,,,, ,,,,,,,,,,
,, ,, ,, Kigoda imechota BOT - ,,, ,,, ,,,,,,,,,,
,, ,, ,, Dowans nani mmiliki - ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,, EPA BOT -,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,, Mikataba mibovu ya madini -,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,, Kura zinaibiwa na wao -,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
WANANCHI WANATAKA KUANDAMANA KWA AMANI kudai haki zao, ---- tumepata TAARIFA za ki.ignorant.ia kuwepo kwa uvunjifu
wa AMANI...!!!!!??????:frusty::frusty::smash::smash::A S 114::A S 114::puke::puke::nono::nono:
 
Kama kweli wamepata fununu hizo basi IGP yuko sahihi kabisa kusimamisha maandamo kwa interest za nchi yetu kuhakikisha amani yetu inaendelea

Amani itaendelea kuwepo, huku unatakiwa uchangie malipo ya Dowans ya 185-bil....
Sasa kama si usakala ni nini?
Mmedanganywa na Amani matokeo yake nchi inabakia na Chakavu tu.
Wenzenu wanachukua rasilimali zenu, na nyie mmebaki kulingia amani tu.

Hv ni nchi gani Duniani ambayo inajivunia amani huku wajanja wachache wakibeba mali za taifa na wengine kuchota mpk kodi wanazotozwa wananchi?

Puuumbaaav
 
Kwa taarifa toka viongozi wakuu wa Chadema Maandamano yapo pale pale pamoja na biti la IGP> source TZ daima soma below information

CHADEMA kuwasha moto Arusha leo
ban.blank.jpg


Waandishi wetu​

amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinatarajiwa kuwasha moto wa madai ya haki kwa kufanya maandamano makubwa ya amani jijini Arusha, yatakayoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, na katibu mkuu wake, Dk. Willbrod Slaa. Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka Arusha jana jioni alisema maandamano hayo yatakayohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi ulio kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni.
Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka jijini Arusha jana jioni alisema CHADEMA itaanza rasmi kuitumia nguvu ya umma kupinga kile alichokiita "uhuni uliofanywa na CCM na serikali yake kujipa ushindi wa lazima katika uchaguzi wa umeya kinyume na matakwa ya sheria halali za nchi.
"Mwanza hakujafanyika uchaguzi kwa sababu ya dhuluma, Kigoma na Arusha uchaguzi ulikuwa batili kabisa. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) tumemsihi sana aingilie kati lakini ameendelea kushirikiana na chama chake (CCM) kuinyima CHADEMA haki ya kuongoza. Tunakwenda kulaani kwa nguvu zote uchakachuaji wa maamuzi ya wananchi" alisema Mbowe.
Aidha, alisema chama hicho kitaitumia fursa hiyo pia kutoa rasmi msimamo wake kuhusu madai ya Katiba mpya yaliyoanzishwa na chama hicho baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani Oktoba mwaka jana.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeruhusu kufanyika kwa maandamano hayo pamoja na mkutano wa hadhara baada ya kujaribu kuyazuia mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kuwepo kwa dalili za uvunjifu wa amani.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye, jana katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini hapa alithibitisha kuwa polisi imeruhusu maandamno na mkutano wa hadhara wa chama hicho kufanyika, huku akisisitiza kuwa wameamua hivyo baada ya CHADEMA kufuata taratibu zote zilizotakiwa.
Kamanda huyo alisema polisi imejipanga kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na hakutatokea vurugu ama uvunjifu wa amani.
Pia alitoa wito kwa watakaoshiriki katika maandamano hayo pamoja na mkutano huo wa hadhara kuwa watulivu na wawe na lengo moja la kutaka kusikia kile ambacho kitazungumzwa katika mkutano huo na wakimaliza waondoke kurejea nyumbani kwa amani.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza na inayotia shaka, mkuu wa jeshi hilo nchini (IGP), Said Mwema, naye aliitisha mkutano wake jana jioni jijini Dar es Salaam akisema polisi imezuia maandamano hayo kwa hofu ya uvunjifu wa amani akidai kuwa amepewa taarifa za kiintelijensia kutoka kwa kamanda wa Arusha.
Badala yake IGP Mwema alisema CHADEMA inaruhusiwa tu kufanya mkutano wa hadhara bila kufanya maandamano kwa madai kuwa kuna uwezekano wa kutokea vurugu.
"Kwa kadiri tulivyofuatilia kuhusiana na maandamano ya CHADEMA tumeona kuna dalili za kutokea uvunjifu wa amani na usalama, ila mkutano ambao wameomba tumewapa ruhusa wafanye na tutaongeza ulinzi zaidi ili kuhakikisha unakuwa wa amani" alisema Inspekta Mwema.
Tamko hilo la IGP Mwema limepingwa vikali na Mbowe pamoja na mwenyikiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, ambao walisisitiza kwamba maandamano pamoja na mkutano wa hadhara vyote vitafanyika kama vilivyopangwa kwani taratibu zote zilifuatwa na chama hicho.
"Hatukusudii kufanya uvunjifu wowote wa amani, tutafanya maandamano ya amani na mkutano mkubwa wa hadhara kama tulivyopanga ¦ hatukubaliani na huo uamuzi wao wa kutuzuia wakati awali walishakubali. Waelewe kuwa nasi ni viongozi wenye haki na mamlaka kamili ya kuwatumikia wananchi. Taarifa ya polisi ya kudharau vyama vya upinzani si haki. Sisi si wajinga hadi tusababishe uvunjifu wa amani.
"Wanajua jiji zima la Arusha litashinikiza uchaguzi huru wa umeya ndio maana wanataka kuzuia ¦.sisi haturudi nyuma, tunasonga mbele" alisema Mbowe kisha aliongeza:
"Kama ni magereza watutayarishie, kama ni risasi watutayarishie ¦ hatuwezi kuletewa viongozi wetu wa kuchaguliwa nchi nzima halafu wao watutishe. Tutaionyesha nguvu ya umma Arusha kesho (leo).
Awali maandamano hayo pamoja na mkutano vilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana na kuzuiwa na jeshi la polisi kutokana na kile kilichoelezwa kutofuatwa kwa taratibu za kuomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara na pia kipindi hicho hakikuwa muafaka kwa masuala ya ulinzi na usalama.
Mbowe alisema jeshi la polisi halina sababu hata moja ya msingi ya kuzuia maandamano na mkutano huo kwani tayari alishafanya mazungumzo na msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa pamoja na IGP mwenyewe na kukubaliana wasubiri hadi mwaka mpya upite ndipo wafanye hivyo.
"Wasimamie mambo kwa misingi ya sheria zilizopo na siyo za kutungwa leo" alisema Mbowe.
Akizungumzia mkang anyiko huo wa polisi, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, alisema kuwa ofisi yake ina barua kutoka polisi inayoruhusu kufanyika kwa maandamano na mkutano wa hadhara.
"Nimepigiwa simu na waandishi wengine wakiniuliza kama tuna taarifa hiyo. Jibu ni tumeruhusiwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanya maandamno na mkutano wa hadhara na chama kimeshajiandaa na maandalizi yote yamekamilika, sina barua ya kuzuia maandamano" alisema Mwigamba.
Jana kutwa nzima katika mji wa Arusha kulikuwa kunapita gari la matangazo kutangaza kuwepo kwa maandamano hayo na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo ambayo yataanza saa nne asubuhi katika maeneo matatu tofauti.
Maandamano hayo yataanzia katika eneo la Philips katika barabara itokayo Moshi kuingia Arusha na kundi jingine litaanzia eneo la Sakina katika barabara itokayo Nairobi kuingia Arusha, huku mengine yakianzia eneo la Mbauda katika barabara itokayo Babati kuja Arusha na yote kumalizikia katika viwanja maarufu vya NMC eneo la Unga Limited.
Kufuatia uhamasishaji mkubwa uliofanywa na viongozi wa CHADEMA, huenda maandamano hayo yakavunja rekodi kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi kutokana na mji wa Arusha toka wakati wa uchaguzi wa mwaka jana kuwa katika vuguvugu kubwa la kisiasa za mageuzi na wananchi wengi kuwa mashabiki wa CHADEMA.
 
Muda wa ukombozi dhidi ya hao mabeberu wachache ni sasa.
Kila la kheri wana CDM huko Arusha, tupo pamoja
 
Vizuri...

'MAANDAMANO YA AMANI' KWA WANANCHI SI ZAWADI TOKA KWA JESHI LA POLISI.

Ni masikitiko makubwa yalioje kwa MTU KUANDAA SHEREHE YA KUKATA NA SHOKA KAMA HUYU NDUGU HAPA JUU eti kwa sababu tu daktari wake kaonyesha nia ya KUAHIRISHIA KIFO walau kwa muda ilhali anajua kwamba ugonjwa wa kansa aliouletea taifa hauna dawa!!!

Karibu kwenye hafla ya UPONYAJI KANSA YA UFISADI KULE MJINI ARUSHA hapo kesho asubuhi. Hakuna kurudi nyuma tena. Said Mwema akishinwa kazi aliokabidhiwa na katiba ya sasa na asichelewe zaidi kutueleza.

Kuandama si ZAWADI KWA WATANZANIA KUTOKA KATIKA JESHI LETU LA POLISI. Wananchi tutalinda wenyewe maandamano haya ya amani Arusha kesho.
 
Back
Top Bottom