Maandamano ya CHADEMA kesho yasitishwa ghafla na IGP baada ya awali kukubalika

IGP Mwema ametangaza kuwa maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kesho HAYARUHUSIWI lakini MKUTANO, RUKSA. Source ITV taarifa ya habari saa 2 usiku.
 
IGP Mwema ametangaza kuwa maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kesho HAYARUHUSIWI lakini MKUTANO, RUKSA. Source ITV taarifa ya habari saa 2 usiku.


Maandamano yamegawanywa katika sehemu kuu 2.

Kundi la kwanza litaanza maandamano kutokea Sombetini kuelekea NMC

Kundi lingine litaanzia Ngulelo kuelekea NMC.

Mwema aache ubabe maandamano ya CHADEMA ni ya amani. Mbona ya CUF kashindwa kuyazuia?
 
Nami nimemsikia kupitia TBC taifa,ila nashindwa kufahamu ni kwa nini wanayaogopa maandamano!Lakini hakijaharibika kitu,cha msingi CHADEMA wajipange vizuri na kuutumia ipasavyo mkusanyiko huo kutema cheche hata kuitia nyufa kwenye lile jumba jeupe mpaka jk aone hapatoshi.
 
Hata mm nimesikia kupitia chanel 10 but mkutano ruksa watu wafikaje bila kutembea? Huko kutembea kwenda knye mkutano ndio maandamano yenyewe!
 
Mkutano upo kama kawa so twendeni kwenye mkutano tukamwage ugali wao si wamemwaga mboga!!!

KAULI YA MWEMA HII HAPA.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP,Said Mwema Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake(Makao Makuu ya Jeshi Hilo)Jijini Dar es Salaam Jiii ya Leo Kuhusu jeshi hiloKusitisha Kwa Maandamano yaliyokua yamepangwa kufanyika Kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)mkoani arusha kwa sabababu za kiusalama na habari za kiintelijensia kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha zilizotelewa na IGP Mwema Zimesema kwmaba Mkutano wa Chadema hapo Kesho Utaendelea Kama Ulivyopangwa Bila Maandamano na kwamba jeshi la Polisi litaimarisha ulinzi wa uhakika kwenye maeneo ya kuzunguka eneo ka mkutano huo kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo muda wote
SOURCE:
http://http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/

Hivi Tanzania lini tutabadilika? Sijui haki ya watanzania ipo wapi?
 
....Taarifa za intelejensia mai a.....ss !! Hivi mbona watu wanaiba kila siku, kila mahali kama hayo mamilioni ya bank including juzi juzi hapo CRDB, watu wako akina Nzowa wanavusha madawa kila kukicha, na hata faru ambaye yule shemejio alijivunia kuwa watalindwa kuliko yy bado ameuawa, na huna taarifa za intelejensia ?
 
huyu mwema anaifanya hii nchi kama inatawaliwa kijeshi hana lolote aende zake uko
 
Sasa wanasema maandamano hapana, hao watu watakaohudhuria mkutano watafikaje?

Nipeni tafsiri sahihi ya Maandamano!
 
Huu sasa ni u dikteta kama ule wa Mugabe miaka ileee!! Hawa polis si wanalipwa mishara kutokana na kodi zetu? sasa iweje washindwe kulinda amani? kama vipi mi naona kamanda mwema ajiuzulu!!
Ahaa tumechoka siye waturuhusu tukamwage ugali

Sio kwenda kumwaga ugali peke yake na mboga pia inabidi tuzimwage tuone watakula nini.Lazima wananchi wajue madhambi yao.
 
Hivi kati ya Mwema na Mkwere nani kamwolea mwenzake? Huu ushemeji kama wa kiduwanzi vile!
 
Back
Top Bottom