Maandamano ya CHADEMA kesho yasitishwa ghafla na IGP baada ya awali kukubalika

BARKMEI

Member
Dec 20, 2010
29
1
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ametangaza kusitisha maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendelieo CHADEMA yaliyokua yaongozwe na FREEMAN MBOWE na DR WILBROAD SLAA kwa kile alichokieleza kua ni taarifa za kiinteligensia kwamba kutakua na uvunjifu wa amani.
KWENU WADAU
 
katiiba inaruhusu lakini wananchi kufanya maandamano ya amani hii serikali ya ajabu sana kwani tukifanya watatufanya nini?
 
Na wakiingia mtaani watafanyaje.. polisi wakianza kuwapiga si ndo watakuwa wao ndo wamevunja amani na si Chadema? hii ni catch-22 kajifunga IGP mwenyewe... ila hana upeo wa kuona hilo...
 
Kwani hao akina mwema kazi yao nini? si kulinda amani? Kwa nini sasa wasijotokeze kwenda kulinda amani katika maandamo hayo au ni uzembe wa kazi?
Kila kitu taarifa za kiinteligensia.. nafikiri wakati umefika ili tujeu hizo taarifa wamezitoa wapi au kwa nini wasiwafikishe mahakamani hao wanaotaka kuleta fujo bila kuathiri haki ya msingi ya maandamano ya amani...?
Kama hawawezi kazi wafutwe na tukabidhiwe sisi hapa ili tuwaoneshe namna ya kuilinda amani bila mtafaruku.. full stop...inafaa pia wajue wenzao ma mataifa mengine hulindaje amani bila kuathiri haki za msingi za raia wengine.... mataifa mengine hawatumii neo hilo la ki.puuzi la taarifa za kinteligensia.. wanaolitumia ni wavivu wa kazi na wavivu wa kufikiri na watu wasio wabunifu katika kazi zao.. ya nini kuendelea kepokea mshahara vili hali kazi hawaifanyi
 
Huu sasa ni u dikteta kama ule wa Mugabe miaka ileee!! Hawa polis si wanalipwa mishara kutokana na kodi zetu? sasa iweje washindwe kulinda amani? kama vipi mi naona kamanda mwema ajiuzulu!!
Ahaa tumechoka siye waturuhusu tukamwage ugali
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ametangaza kusitisha maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendelieo CHADEMA yaliyokua yaongozwe na FREEMAN MBOWE na DR WILBROAD SLAA kwa kile alichokieleza kua ni taarifa za kiinteligensia kwamba kutakua na uvunjifu wa amani.
KWENU WADAU

hivi mbona siku zote kisingizio ni taarifa za kiintelijensia? Kama wamesema ni maandamano ya Amani sasa kazi ya polisi si ni kulinda waandamanaji dhidi ya hao wanaotaka kuvunja amani? This country bwana is very sick.
 
Kama kutakua na uvunjifu wa amani sio ndio good reason ya kupiga mafuruku maandamano? hizo taarifa za kiintelijinsia zina happen during maandamano tu? mbona wakati wa radar, richmonduli, dowans, epa, maremeta, deep green, tanzania gold refinery, ufasadi's, jambazi's attacks, somalian's pirates, somalian's transit to South Africa,n.k huwa hawapati hizo tarifa za kiintelenjensia? Shame on you, you lie in front of everyone, can't wait for you guys to cheat GOD and DEATH
 
Mkutano upo kama kawa so twendeni kwenye mkutano tukamwage ugali wao si wamemwaga mboga!!!

KAULI YA MWEMA HII HAPA.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP,Said Mwema Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake(Makao Makuu ya Jeshi Hilo)Jijini Dar es Salaam Jiii ya Leo Kuhusu jeshi hiloKusitisha Kwa Maandamano yaliyokua yamepangwa kufanyika Kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)mkoani arusha kwa sabababu za kiusalama na habari za kiintelijensia kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha zilizotelewa na IGP Mwema Zimesema kwmaba Mkutano wa Chadema hapo Kesho Utaendelea Kama Ulivyopangwa Bila Maandamano na kwamba jeshi la Polisi litaimarisha ulinzi wa uhakika kwenye maeneo ya kuzunguka eneo ka mkutano huo kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo muda wote
SOURCE:
http://http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/
 
Hizi taarifa za ki-intelijensia za akina Mwema ni OXYMORON police intelligence ni concept inayokinzana yaani kujicontradict.. police are not intelligent have no intelligence... ashakum si matusi....
Na we Topical acha kuwa armchair police... ingia we mtaani uwapige wananchi muone jinsi gani wananchi walivyochoka!
 
Back
Top Bottom