Maandamano ya CHADEMA Arusha: Mabomu yarindima, raia wauawa na viongozi wakamatwa

Pamoja na kutunyima kuandamana maadam mkutano utakuwepo ni nafuu, lakini hii ni kuwanyima wananchi wa Arusha haki yao ya kimsingi kuandamana na kwenda kuwapokea viongozi wao waliowapigia kura. Chadema wameshasema wao wanaandama kwa amani sasa wewe Andengenye si uwaachie waandamane? kama maandamano hayo yatakua ni ya kuvunja amani basi fanya kazi yako! sio kututisha kuanzia asubuhi watu tunashindwa kufanya kazi ni ving'ora na maasikari kila kwenye kona ya mji? Shame on you mnaovunja demokrasia ya kuwapa watu uhuru na haki yao ya kimsingi:frusty:
 
Arusha sasa hivi mvua inanyesha.....madhara yake kwenye hili vuguvugu bado si wazi sana......................................
 
Maandamano ni noma! maana vifaa vilivyopita hapa(uhuru road) kwa ajili ya kuzuia maadamano vinatisha!

Nimempigia rafiki yangu Arusha: Ni mabomu matupu mji mzima na vijana wa Chadema nao wame kaa kingangari!
 
Hivi punde polisi wa kuzuia fujo wamelipua mabomu ya machozi, hali sio nzuri hapa mjini.....

Sidhani kama tutafika kwa namna hii, kweli wanatuogopa peoples power!!!!!!!
 
Mh!nashukuru mkuu kwa taarifa,endelea kutujuza kila kitu kinachoendelea!Kufikia democrasia ya kweli Afrika itachukua muda sana!!
 
Hii serikali ya ajabu kweli, inataka kutumia nguvu kubwa kuzuia maandamano ya amani kisha hali inachafuka. wacha wavuruge mambo hapo Arusha kisha Mataifa ya nje wawatangazie raia wao kuwa Arusha ni mji hatari kufanya utalii kwa vile hakuna usalama. Umasikini juu ya umasikini, kisa lazima Meya awe wa CCM
 
Si walitoa kibali cha maandamano/mkutano. Sasa mabomu ya nini tena?? Tanzania kufikia demokrasia itachukuwa muda sana na sia Afrika maana wenzetu washa anza kupiga hatua sisi bado tuna subiri muda. Eti bado tunaulizana kwa nini sasa???
 
Polisi wakati wote ndiyo wenye kuleta vurugu! Wananchi mara nyingi hawaanzishi vurugu bali polisi wanawachokoza wananchi na kuwaonea lakini haya yote mwenye kuhusika atatoa hesabu!!!! It is not too far from now!!!!!!
 
Unaweza twambia tatizo hasa lililosababisha mabomu hayo.

Je maandamano bado yanaendelea? na je kunauwezekano huo mkutano ukafanyika leo huko Arusha? Naomba utujuze mkuu.
 
Back
Top Bottom