Maandamano ya Amani- Wafanyakazi wote.

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Hatufanyi mgomo tunaandamana tu.

Tunaandamana Kudai NSSF NA PPF zetu.
 
Wazo zuri mkuu...nakuunga mkono sasa kama walio mgodini tunapigwa redundancy halafu leo utuambie hatupati hela zetu kweli hili la kufikisha 60yrs litaleta shida...
 
kweli kabisa hawajamaa sio kabisa umbumbumbu wao katika kutumia hela zetu wanataka watupe mzigo sisi
 
Serikali hii dhulumati na dhalimu lazima kuandamana kwa amani ama kwa shari
 
Hili lilipaswa kuanza na wananchama wapya wanaojiunga sasa. Lakini kwa wale wa zamani mkataba wao ulipaswa kuachwa jinsi ulivo, au kuwalipa chao then wajiunge upya kwa mkataba huu mpya wa kusubiri mpaka ukaribie kufa ndio wakupe chako
 
Wazo zuri mkuu...nakuunga mkono sasa kama walio mgodini tunapigwa redundancy halafu leo utuambie hatupati hela zetu kweli hili la kufikisha 60yrs litaleta shida...

mkuu mi npo kakola uku kahama,watu hawana morali ya kazi kbsa.
 
Wakuu mi nmechanganykiwa kbsa,yani nna m70 nssf nltka kdgo ziongezke nifanye mambo yngu,eti leo wanaleta mambo haya huu si usenge kwli,?
 
kweli kabisa hawajamaa sio kabisa umbumbumbu wao katika kutumia hela zetu wanataka watupe mzigo sisi

kwani wanajua wanacho fanya kwani kutokana na maradhi haya UKIMWI..KIPINDU ...TB...BP..SUKAR...KINDUTUR...NK..kati ya watu 100 ni watu 22 tu ndio watafika hiyo miaka 60 walilo baki ote wataku HAYATI kwahiyo hakutakua na mdai watu watakula ki ulainiiiiiiiiiiiiii:lllllll #ila kelo ni ubunifu unaotakiwa ndio huo........poleni walegwa mi CHIMO....
 
wajameni nimetuna kwa hasira hapa naomba tuingie front tuukatae huu udhalimu....
 
Wanatumiwa vibaya hawa walianza na madaktari sasa wanawafuata wasio na ajira za kudumu wakiweza watawapandishia PAYEE kwa wote huu ni wehu
 
Naombeni mawazo yenu Tuanzeje? achaneni na hao TUCTA. tuji mobilise wenyewe kwanza.

Mnaonaje tukapanga Tar ya kukutana pale CHADEMA Square?
 
Mi nataka tuu niulize hivi hawa jamaa wana mkataba na Mungu kuwa wafanyakazi wote wa tanzania watafikisha miaka 55 ya kustaafu kwao kazi au ni kitu gani maana haina maana umpangie mtu eti sikupi mafao yako mpka ufikishe miaka 55
Je wameongea na Sir God wakajua kuwa nitafikisha hiyo miaka
Mipango ya watu wengi ambao walitegemea wapate mafao yao wafanyie mambo mengine imevurugwa vya kutosha na hii sheria yao ya ajabu
 
Mlachake sijui hawa walioipitisha hii sheria walifikiria abaout wazee ambao wanasotea mafao yao miaka na miaka kwa kuwa records hazionekani
Na je kama nimeacha kazi kampuni tano na baadhi ya hizo kampuni zishafilisika na kufungwa na naenda kudai mafao yangu baada ya hiyo miaka na kuna records ambazo inabidi nizifuatilie kwa yule mwajiri wangu na ndo hivyo kampuni ishakufa wananisaidiaje au ndo nishapoteza mafao
 
Last edited by a moderator:
Yaani huu ni use** kwakweli, mimi nina hasira, hivi nchi hii tutafanywa wajinga hadi lini, wanaJF mlioko Mwanza na sisi tuandae maandamano

Mlachake sijui hawa walioipitisha hii sheria walifikiria abaout wazee ambao wanasotea mafao yao miaka na miaka kwa kuwa records hazionekani
Na je kama nimeacha kazi kampuni tano na baadhi ya hizo kampuni zishafilisika na kufungwa na naenda kudai mafao yangu baada ya hiyo miaka na kuna records ambazo inabidi nizifuatilie kwa yule mwajiri wangu na ndo hivyo kampuni ishakufa wananisaidiaje au ndo nishapoteza mafao
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Naombeni tujimobilise. Tucta na wengine watakuja baadae.
 
Hatufanyi mgomo tunaandamana tu.

Tunaandamana Kudai NSSF NA PPF zetu.

Lakini mkuu, hebu tuwe serious kidogo jamani. Haya mambo ndo yanatufanya tuwe na mkanganyiko usio kuwa wa lazima. Mimi leo asubuhi nimemsikiliza huyo the so called mkurugenzi wa SSRA akiwa ITV. Pamoja na kujikanyaga kanyaga sana lakini nimepata point kama mbili.
1. Kuhusu fao la kujitoa, anasema taarifa ilipotoshwa. Kwamba utaratibu/utekelezaji wa sheria hiyo bado haujaanza
2. Wanaandaa kanuni ambazo zitazingatia wafanyakazi wa mikataba n.k

NAOMBA KUWASILISHA
 
Back
Top Bottom