Maandamano ya Amani kupinga uwepo wa Mgodi wa Kuchimba dhahabu wa Golden Pride Project Nzega

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega inakualika kwenye Maandamano ya Amani kupinga uwepo wa Mgodi wa Kuchimba dhahabu wa Golden Pride Project, Nzega, kwa kuwa hauna faida kwa Nzega na kwa Taifa, Unaharibu mazingira, Umegubikwa na usiri mkubwa, Wachimbaji wadogo na wakazi wa maeneo mgodi huu ulipo hawajalipwa fidia mpaka leo, wananchi wa Nzega hawapati fursa za ajira wala tenda mbalimbali mgodini humo, unatumia maji mengi zaidi ya wenyeji, unachafua na kuharibu vyanzo vya maji, uongozi na wamiliki wa mgodi hawana ubinadamu na huruma kwa wenyeji wa Nzega na hata nchi yetu kwa ujumla n.k.

Maandamano haya yatafanyika Mnamo Tar 3/4/2011 mjini Nzega. Njia zitakazotumika, mahali pa kuanzia na kumalizia maandamano haya mtatangaziwa baada ya makubaliano na Polisi (W) ya Nzega. Tutazidi kutoa taarifa zaidi.

Nyote mnakaribishwa kuunga mkono jitihada hizi za kudhibiti wizi wa Raslimali za Taifa na uharibifu mkubwa unaofanyika!

Wakatabahu,
Ndg. HK.
 
Kwanini msiende Bungeni na kutoa hizo hoja kwani ni uchochezi dhidi ya serikali, yataharatisha usalama na kutishia "amani na utulivu". Uchaguzi ulishaisha subirini hadi 2015.
 
Mnataka kuleta uvunjifu wa amani na kuwatisha wawekezaji ili waone Tanzania si sehemu salama ya uwekezaji, tafadhalini tunawaomba muitunze amani na utulivu ttulioachiwa na wahasisi wa Taifa hili.

Kwanza wananchi wana kazi nyingi hawana huo muda wa maandamano. ni matumaini yangu taarifa za kiitelijensia zitakubaliana na mimi. uchaguzi umekwisha tuache siasa tufanye kazi ( usiniulize mimi kama kazi zipo hau hazipo ).
 
Ni wiki sasa tokea nizungumzie kusahaulika kwa portion ya barabara toka Nzega kwenda Tabora.

Na hatimaye kukosekana kwa miundombinu ama kuwepo isiyokidhi mahitaji kulingana na wakati uliopo kwa mkoa wa Tabora leo mnaniambia kuna Golden Pride Project Nzega...how come mji mchakavu uliosahaulika unaweza kutoa so called Golden Project? Inawezekanaje?

Una manufaa gani kwa wana Nzega na Tabora? Hiyo reseach walioteshwa ama walipita kwenye huu uchochoro wa vumbi kuelekea kuripoti mkoani ama walipaa kwa helikopta hadi kwenye shamba la bibi? Kwanini serikali ya CCM haina aibu?

Kwanini hawna haya? JK na Golden Proposal zako utaondoka kwa golden shame! Alama za nyakati zinabashiri hivi!
 
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega inakualika kwenye Maandamano ya Amani kupinga uwepo wa Mgodi wa Kuchimba dhahabu wa Golden Pride Project, Nzega, kwa kuwa hauna faida kwa Nzega na kwa Taifa, Unaharibu mazingira, Umegubikwa na usiri mkubwa, Wachimbaji wadogo na wakazi wa maeneo mgodi huu ulipo hawajalipwa fidia mpaka leo, wananchi wa Nzega hawapati fursa za ajira wala tenda mbalimbali mgodini humo, unatumia maji mengi zaidi ya wenyeji, unachafua na kuharibu vyanzo vya maji, uongozi na wamiliki wa mgodi hawana ubinadamu na huruma kwa wenyeji wa Nzega na hata nchi yetu kwa ujumla n.k.

Maandamano haya yatafanyika Mnamo Tar 3/4/2011 mjini Nzega. Njia zitakazotumika, mahali pa kuanzia na kumalizia maandamano haya mtatangaziwa baada ya makubaliano na Polisi (W) ya Nzega. Tutazidi kutoa taarifa zaidi.

Nyote mnakaribishwa kuunga mkono jitihada hizi za kudhibiti wizi wa Raslimali za Taifa na uharibifu mkubwa unaofanyika!

Wakatabahu,
Ndg. HK.
Hayo maandamano yatapokelewa na nani Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa au Pinda.
 
Nyie vipi tena? Maandamano hayo yanaandaliwa na CCM?

Mbunge wa Nzega si ni CCM? Huyu mbunge anataka kutuharibia sifa yetu kubwa Wanyamwezi?

Sasa tukishaanza kuilaumu CCM, CCM itapata wapi tena KURA za kuiba mwaka 2015?

Pia haya maandamano si YANAHATARISHA amani ya Tanzania?

Mkome kabisa, mshindwe na mlegee kwa jina la CCM ya MAFISADI.

Mtuache tu sisi Wanyamwezi na Usingizi wetu na Wageni wakiongozwa na RA na waibe sana.
 
Wana jamvi tulizeni munkari, taarifa ya kiitelijensia zinaonyesha hatukakuwa na uvunjifu wa amani kwenye haya maandamano, Uvunjifu wa amani ni kwa maandamano ya Chadema tu. CCM nao wameshtukia dili, wanaona maandamano yanauza siku hizi.

Haya ni ya kutetea maslahi ya wana Nzega yanaandaliwa na Muheshimiwa H. Kigwangallah Mb Nzega. Atakayepokea maandamano atajulikana baadae.
 
Kwa mbunge Nzega. Ndg Hamis Andrew Kigwangallah, ninavyokufahamu wewe ni jembe na intelligent toka A'level ulipokuwa kaka mkuu na mcheza volleyball na engineer wa mgomo Muhimbili.

Umekosea chama kaka, omba msaada kwa dr. George Maro aliyeko mwanza, cdm damu
 
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega inakualika kwenye Maandamano ya Amani kupinga uwepo wa Mgodi wa Kuchimba dhahabu wa Golden Pride Project, Nzega, kwa kuwa hauna faida kwa Nzega na kwa Taifa, Unaharibu mazingira, Umegubikwa na usiri mkubwa, Wachimbaji wadogo na wakazi wa maeneo mgodi huu ulipo hawajalipwa fidia mpaka leo, wananchi wa Nzega hawapati fursa za ajira wala tenda mbalimbali mgodini humo, unatumia maji mengi zaidi ya wenyeji, unachafua na kuharibu vyanzo vya maji, uongozi na wamiliki wa mgodi hawana ubinadamu na huruma kwa wenyeji wa Nzega na hata nchi yetu kwa ujumla n.k.

Maandamano haya yatafanyika Mnamo Tar 3/4/2011 mjini Nzega. Njia zitakazotumika, mahali pa kuanzia na kumalizia maandamano haya mtatangaziwa baada ya makubaliano na Polisi (W) ya Nzega. Tutazidi kutoa taarifa zaidi.

Nyote mnakaribishwa kuunga mkono jitihada hizi za kudhibiti wizi wa Raslimali za Taifa na uharibifu mkubwa unaofanyika!

Wakatabahu,
Ndg. HK.

Hili nalo limesababishwa na Mh. Anna Makinda kwa sababu Mh Mbunge alikusudiwa kuwasilisha hoja binafsi ijadiliwe Bungeni nadhani itakuwa imetupiliwa mbali kuzuia Serikali isikosolewe
 
Huyu MB wa ccm anabeep tu. Hakuna maandamano serious yanatolewa taarifa mwezi mzima kabla. Anataka serikali imfuate na kumpa kitu kidoga ili asitishae nia yake ya maandamano. Mtaniambia kama yatafanyika!!! Na ikitokea hivyo basi nitaamini ukombozi umefika.

Vinginevyo na yeye aeleweke kwamba anataka kuiondoa serikali madarakani. MH Kigwangalla kama kweli una nia ya dhati tunataka tuone hayo maandamano yanafanyika, usituletee usanii hapa. wewe si ni ccm??
 
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega inakualika kwenye Maandamano ya Amani kupinga uwepo wa Mgodi wa Kuchimba dhahabu wa Golden Pride Project, Nzega, kwa kuwa hauna faida kwa Nzega na kwa Taifa, Unaharibu mazingira, Umegubikwa na usiri mkubwa, Wachimbaji wadogo na wakazi wa maeneo mgodi huu ulipo hawajalipwa fidia mpaka leo, wananchi wa Nzega hawapati fursa za ajira wala tenda mbalimbali mgodini humo, unatumia maji mengi zaidi ya wenyeji, unachafua na kuharibu vyanzo vya maji, uongozi na wamiliki wa mgodi hawana ubinadamu na huruma kwa wenyeji wa Nzega na hata nchi yetu kwa ujumla n.k.

Maandamano haya yatafanyika Mnamo Tar 3/4/2011 mjini Nzega. Njia zitakazotumika, mahali pa kuanzia na kumalizia maandamano haya mtatangaziwa baada ya makubaliano na Polisi (W) ya Nzega. Tutazidi kutoa taarifa zaidi.

Nyote mnakaribishwa kuunga mkono jitihada hizi za kudhibiti wizi wa Raslimali za Taifa na uharibifu mkubwa unaofanyika!

Wakatabahu,
Ndg. HK.

hapa napo kuna jambo!!!
 
Wadau wa maendeleo ya Taifa, karibuni kwetu Nzega mtuunge mkono katika harakati za kusitisha uchukuaji holela wa Raslimali unaoendelea.

Leo tumewasilisha rasmi taarifa za njia, muda na siku kwa Mkuu wa Polisi (W) tukiomba watupatie ulinzi siku ya maandamano.

Maandamano jamani ni njia mojawapo tu ya kupaza sauti ili wasosauti wasikike! Kama mtu unadai fidia ya ardhi yako iliyokwapuliwa kwa miaka zaidi ya 15 na haulipwi, sasa unafanyaje? Unakuja kwa Mbunge wako anafuatilia hapati majibu ya kuridhisha, sasa naye anafanyaje?

Si ni bora mkaandamana pamoja kwa unyonge wenu, mkapaza sauti zenu kwa pamoja, labda mtasikika??? [solidarity forever]. Kama mtu unaomba nyaraka muhimu za mgodi unayimwa, na mgodi uko kwako, na wananchi wanalalamika hawaoni matunda ya mgodi, hawapati faida yoyote ile, hawapati ajira wala tenda kwenye mgodi, sasa hapo unafanyaje?

Ni bora mkaandamana walau mkaonesha kuwa hamuutaki na wala hamuukubali mgodi huo, period!
 
Ili tutoke hapa tulipo tunahitaji uchochezi na chokochoko nyingi dhidi ya Serikali kuliko utulivu. Hongera bwn mbunge kwa kuendeleza harakati zetu za uchochezi, onyo: usiingie mitini.
 
Wadau wa maendeleo ya Taifa, karibuni kwetu Nzega mtuunge mkono katika harakati za kusitisha uchukuaji holela wa Raslimali unaoendelea.
Leo tumewasilisha rasmi taarifa za njia, muda na siku kwa Mkuu wa Polisi (W) tukiomba watupatie ulinzi siku ya maandamano. Maandamano jamani ni njia mojawapo tu ya kupaza sauti ili wasosauti wasikike! Kama mtu unadai fidia ya ardhi yako iliyokwapuliwa kwa miaka zaidi ya 15 na haulipwi, sasa unafanyaje? Unakuja kwa Mbunge wako anafuatilia hapati majibu ya kuridhisha, sasa naye anafanyaje? Si ni bora mkaandamana pamoja kwa unyonge wenu, mkapaza sauti zenu kwa pamoja, labda mtasikika??? [solidarity forever]. Kama mtu unaomba nyaraka muhimu za mgodi unayimwa, na mgodi uko kwako, na wananchi wanalalamika hawaoni matunda ya mgodi, hawapati faida yoyote ile, hawapati ajira wala tenda kwenye mgodi, sasa hapo unafanyaje? Ni bora mkaandamana walau mkaonesha kuwa hamuutaki na wala hamuukubali mgodi huo, period!

Tupo pamoja mh. Hofu yangu hao ndugu zako ccm hawatakawia kukusue kwani najua unawajua vizuri jiandae kupata upinzani. Na safari yako kisiasa ikiwa ngumu kabla ya kumaliza 5yrs.
 
Back
Top Bottom