Maandamano ya ajabu - polisi wapelekewa maiti

JESHI la Polisi Mkoani Mara jana lililazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wananchi wa Bunda mkoani Mara ambao walikuwa wamechukua jeneza la mtu ambaye alidaiwa kufa kwenye mazingira ya kutatanisha.

Tukio hilo limetokea jana jioni mkoani humo. Wananchi wa eneo hilo, kwa nyakati tofauti, walidai kuwa baada ya kuifunua maiti hiyo iliyokuwa ndani ya jeneza walikuta ikitoa machozi, hali ambayo ilizua hofu kwa waombolezaji na kudai kuwa kuna mkono wa mtu.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti hiyo ilianza kutoa machozi mara baada ya mama mdogo wa marehemu huyo kufika eneo hilo na kuanza kuiangalia na ndipo ilipoanza kudondosha machozi.


Kutokana na kitendo hicho, ndugu wa marehemu hawakukubaliana nacho ndipo walipotaka hatua za kisheria zifuatwe ili wamfahamu aliyehusika na tukio hilo.


Hali hiyo ilisababisha baadhi ya waombolezaji kufanya maandamano huku wakiwa wamebeba maiti yao kwenye mkokoteni hadi kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi.


Polisi baada ya kuona umati wa watu umezingira katika kituo chao huku wakileta vurugu walilazimika kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi.


Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja mama mdogo huyo alitoweka katika mazingira gani.
Kwa hivyo huyo mama mdogo ndo mtuhumiwa??
NCHI hii bana ina mambo.............
 
yAANI SIJUI TUTAELIMIKA LINI HUU UJINGA NDIO UNATUFANYA TUENDELEE KUAMINI UCHAWI MPKA LEO,KILA TUNDU LA MWANADAMU HUTOA MAJI MTU ANAPOKUFA NDIO MAANA HOSPITALI HUFANYA LAST OFFICE HUZIBA MATUNDU YOTE KWA PAMBA MDOMO MACHO PUA MASKIO ,UKE NA NJIA YA HAJA KUBWA WANATAKIWA KUPEWA ELIMU TUU

...ukute hapo kuna mjinga mmoja tu alimaka: "He! Mbona maiti anatoa machozi!!" Kosa. Kila mtu akadakia na hakuna alitaka kwenda against na jumuiya kwa kushauri maiti ipelekwe hospital ikapimwe vizuri. Ukute pia huyo wa kwanza kumaka hivyo ana uadui wa siku nyingi na huyo mama mdogo! yaani, tabu tupu wabongo.

 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom